Mmmmh! sidhani kama iko sahihi kwamba Russia anazuia askari wake kufa. Kwani askari kufa vitani ni ajabu? Hiyo kazi ya uaskari, ni pamoja na kupambana kulilinda Taifa hata ikibidi damu imwagike.
Houthi ni kikundi kidogo cha "wababe wa vita" ndani ya nchi huru ya Yemen.
Hicho kikundi sio ndo Watawala wanaoiongoza nchi ya Yemen. Hicho sio mwakilishi wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa Yemen. Houthis wana maslahi yao tofauti na Maslahi ya Taifa la Yemen. Kundi hilo linatumia Itikadi za kidini na linafadhiliwa na Taifa la Iran ambayo ni nchi tofauti na Yemen. Sidhani kama Nchi ya Yemen iliidhinisha kwamba Iran ndo awe anamsaidia Houthi.
Ni kwa mantiki hiyo Houthis wanaonekana kama wanatembeza ubabe kutokana na kupewa uwezo wake na Iran ambayo haijawekwa wazi kwamba Yemen imeridhia jambo hilo. Je; Iran hana mipaka ya utoaji wa misaada au mbona Iran inatoa misaada lakini ni misaada ya kijeshi sio ya kibinadamu?.
Nenda kaifuatilie jeshi la Urusi lina active personnel wangapi.
Pia tunatakiwa tufikirie kama Urusi imeishiwa askari mbona kila leo inasonga mbele na kubeba maeneo!??
Kumbuka tangu 2022 Urusi ilianza kuwatumia Wagner group na baadhi ya askari wake.
Hii Kwa akili ya haraka lazima useme anaepuka vifo vya askari kuwa wengi.
Houthi kilikua chama Cha siasa kama CCM au ACT wazalendo.
Ni hao hao Houthi ambao walipitisha serikali ya mpito ya Mansour,ila ilipofikia 2013 wakati wa Mansour kutoka madarakani ili free and fair election ifanyike Mansour akagoma.
Raia wote walikua hawamtaki Mansour,mwishowe Houthi ikabidi waingie barabarani na bunduki KWA USHAWISHI WA 90% YA WAYEMENI ambao hawakuwa wakiutaka huo utawala,mbaya zaidi huo utawala wa Mansour ulikua na support ya serikali za kisunni mathalan Saudi Arabia na USA.
Iran ikatoa sapoti Kwa Houthi ikiwa na maslahi yake ya kidiplomasia.
Na ilitoa msaada wa kifedha na kijeshi kama ilivyotoa Hizbollah.
Hizbollah wana hadi taasisi za kusaidia raia kiuchumi Kusini mwa Lebanon na mtoaji wa hizo fedha ni Iran.
Utasemaje Iran anatoa misaada ya kijeshi peke yake!??
Halafu kitu ambacho mkuu hujakitambua ni kuwa 90% ya raia wa Yemeni WANAIPENDA,WANAISAPOTI NA WANAIKUBALI HOUTHI.
Houthi ndiyo inayoongoza Sanaa mji mkuu wa Yemen.
Houthi ndio serikali ya Yemen Sasa hivi.
Hiyo serikali ambayo USA na washirika wanailazimisha raia wa Yemeni HAWATAKI KUITAMBUA NA HAWAITAMBUI.