Wapinzani wa Tanzania mnaokimbilia huku Kenya mtatuchonganisha, tumieni mbinu kama za Lissu

Wapinzani wa Tanzania mnaokimbilia huku Kenya mtatuchonganisha, tumieni mbinu kama za Lissu

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Nimesoma kwa mshtuko kwamba aliyekua mbunge huko Tanzania bwana Nyalandu naye amekamatwa akijaribu kukimbilia Kenya, ilhali huku tayari tunaye yule wa Arusha bwana Lema, ambaye tayari tumechimbwa mkwara na asasi za kimataifa asirudishwe kwao Tanzania maana huko wanasakwa na kuuawa, kuna yule aliyegombea urais bwana Lissu keshajiokoa kwa kuchukua hifadhi ndani ya ubalozi wa mabeberu wa Ujerumani, huyo yuko nafuu maana wale ni baadhi ya Mataifa ambayo hutoa misaada Tanzania, hivyo wana uwezo wa kusema chochote na kikasikilizwa.

Lakini sisi huku mkija, mnatuingiza kwenye hali ngumu ya ugomvi baina yetu na huyo mnayemkimbia Rais wenu John Pombe Magufuli halafu upande wa pili asasi za kijamii za kimataifa kama Amnesty International, ambao tumesharidhia sheria za kuhifadhi mkimbizi yeyote anayeitoroka nchi yake kuokoa uhai wake. Muda wowote Magufuli anaweza akafungia ndege zetu kuruka kuja huko. Hehehe

Tumieni busara kama hiyo ya Lissu, mjichomeke kwenye balozi zozote za mabeberu, huko hamtaguswa ila duh yaani hiyo Tanzania iliyokua inapokea Warundi wanaoikimbia nchi yao, leo imegeuka kuwa chanzo cha wakimbizi, poleni sana ndugu zetu, tunawaombea.

========

Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, (Chadema), Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu.

 
ila ujue amnesty international wanafanya kazi kufatisha universal declaration of human rights la UN

ili mkimbizi wa siasa akubaliwe si kunavigezo?

yafanyie kazi hayo [emoji115][emoji115]

then sheria zetu na za kimataifa znasemaje kwa mtu aliefanya makosa dhahiri nchini kwake na kukimbilia nchi A?

niwaambie kabisa kenya mskubali
kuicheza ngoma ya upinzani wa tz kichwakichwa itawatokea puani!!!
 
daah....tanzania kunani tena?haijawahi kunijia akilini kuwa watanzania watakimbilia usalama wao nchini kenya.Naona polepole mnajitahidi mchukue sifa zetu za unyang'au na kwa kasi,hii mtatupiku tu..

Kwani si yule Lissu ambaye amekimbilia ubalozini kuna kipindi tumempa uhifadhi baada ya kulishwa risasi 38, hawa kweye awamu hii wanalo ila sasa wanataka kutuburuza kwenye ugomvi wao, nawarai hao wapinzani wao wakimbilie balozi za mabeberu, humo hawataguswa hata unywele.
 
Bila shaka mnaogopa JPM asije kupiga marufuku mahindi kuingia Kenya!

Mwambieni Kenyatta na Mabwenyenye wenzake waachie ardhi kwa Wakenya ili wazalishe mazao ya chakula vinginevyo mtaendelea kumuogopa JPM ili kubembeleza mahindi "yake"!
 
Kwani si yule Lissu ambaye amekimbilia ubalozini kuna kipindi tumempa uhifadhi baada ya kulishwa risasi 38, hawa kweye awamu hii wanalo ila sasa wanataka kutuburuza kwenye ugomvi wao, nawarai hao wapinzani wao wakimbilie balozi za mabeberu, humo hawataguswa hata unywele.
Hii ngoma wanayopigiwa na jiwe roundi hii wataicheza tu wapende wasipende hawa watani wetu. Ila wapambane huku kwao watuache kivyetuvyetu tu.hawana jema hawa ndugu zetu. Wanajileta na hatujwaita,mwisho wa siku utasikia wanatuponda humu JamiiForums wakitusema tunawachokonoa wakati wametufuata kwetu.
 
daah....tanzania kunani tena?haijawahi kunijia akilini kuwa watanzania watakimbilia usalama wao nchini kenya.Naona polepole mnajitahidi mchukue sifa zetu za unyang'au na kwa kasi hii, mtatupiku tu..
Hapana hatuwez kua kama nyie maana hakuna raia wa tz ashaonja kashkash za the Hague
 
Bila shaka mnaogopa JPM asije kupiga marufuku mahindi kuingia Kenya!!!

Mwambieni Kenyatta na Mabwenyenye wenzake waachie ardhi kwa Wakenya ili wazalishe mazao ya chakula vinginevyo mtaendelea kumuogopa JPM ili kubembeleza mahindi "yake"!!!
Akili kama hizi ndio zinafanya tanzania inarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Wapinzani wameanza kukimbia mmoja mmoja nyinyi mnajichekesha tu. Magu amekua serikali, upinzani, media, mahakama, msanii, kitengo cha polisi, yaani mwisho mtamuacha yeye na nchi tu. Hivi ulishwahi fikiria kuna hata siku moja watz wenzako watatorokea Kenya?
 
CHADEMA SANAA GROUP. Hizi sinema za Chadema waandike upya stori. Hivi nani amtishie maisha Nyalandu.
Mbona inakuuma sana Nyalandu kukimbia. Kama unaona wivu na ww kimbilia Burundi
 
akili kama hizi ndio zinafanya tanzania inarudi nyuma badala ya kwenda mbele.wapinzani wameanza kukimbia mmoja mmoja nyinyi mnajichekesha tu.magu amekua serikali,upinzani,media,mahakama,msanii,kitengo cha polisi....yani mwisho mtamuacha yeye na nchi tu...hivi ulishwahi fikiria kuna hata siku moja watz wenzako watatorokea kenya?
Hunijui kwa maisha yangu halisi wala ya hapa JF, kwahiyo hayo mahubiri yako tafuta kwa kuyapeleka!!
 
akili kama hizi ndio zinafanya tanzania inarudi nyuma badala ya kwenda mbele.wapinzani wameanza kukimbia mmoja mmoja nyinyi mnajichekesha tu.magu amekua serikali,upinzani,media,mahakama,msanii,kitengo cha polisi....yani mwisho mtamuacha yeye na nchi tu...hivi ulishwahi fikiria kuna hata siku moja watz wenzako watatorokea kenya?
hatuna shida na kukimbia kwao ila wamalizane kwanza na sheria za nchi
 
Back
Top Bottom