MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Nimesoma kwa mshtuko kwamba aliyekua mbunge huko Tanzania bwana Nyalandu naye amekamatwa akijaribu kukimbilia Kenya, ilhali huku tayari tunaye yule wa Arusha bwana Lema, ambaye tayari tumechimbwa mkwara na asasi za kimataifa asirudishwe kwao Tanzania maana huko wanasakwa na kuuawa, kuna yule aliyegombea urais bwana Lissu keshajiokoa kwa kuchukua hifadhi ndani ya ubalozi wa mabeberu wa Ujerumani, huyo yuko nafuu maana wale ni baadhi ya Mataifa ambayo hutoa misaada Tanzania, hivyo wana uwezo wa kusema chochote na kikasikilizwa.
Lakini sisi huku mkija, mnatuingiza kwenye hali ngumu ya ugomvi baina yetu na huyo mnayemkimbia Rais wenu John Pombe Magufuli halafu upande wa pili asasi za kijamii za kimataifa kama Amnesty International, ambao tumesharidhia sheria za kuhifadhi mkimbizi yeyote anayeitoroka nchi yake kuokoa uhai wake. Muda wowote Magufuli anaweza akafungia ndege zetu kuruka kuja huko. Hehehe
Tumieni busara kama hiyo ya Lissu, mjichomeke kwenye balozi zozote za mabeberu, huko hamtaguswa ila duh yaani hiyo Tanzania iliyokua inapokea Warundi wanaoikimbia nchi yao, leo imegeuka kuwa chanzo cha wakimbizi, poleni sana ndugu zetu, tunawaombea.
========
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, (Chadema), Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu.
www.jamiiforums.com

Lazaro Nyalandu azuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Namanga baada ya kukosa nyaraka muhimu
Mh lazaro NYALANDU amezuiliwa namanga akiwa anaelekea Kenya kutafuta hifadhi. Amezuiliwa namanga. Kufika mwakani tutabaki mimi na wewe ------ Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, (Chadema) Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga baada...