BodGanleonid
JF-Expert Member
- Nov 14, 2022
- 3,021
- 4,330
Aisee [emoji848]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ndio point. Sheria ipo hivyo, mnajisumbua tu., soneni miezi 9 PGD, Mbona mna akili.hadi tukasomee post graduate
Masuala ya Utumishi hayaendi kwa utashi wa mtu, kuwa na akili na kama hujui kitu tulia, tumia muda wako kusoma comments za wanaoelewa nawe ujifunze.
Mleta Post nakushauri masuala yafuatayo:
1. Angalia Cheo chako cha muundo ulichoajiriwa, kisha tafuta muundo wa Kada yako uone utaratibu uliowekwa wa kupanda madaraja kutoka ngazi moja na nyingine.
2. Kuthibitishwa kazini ( kwa mujibu wa Sheria) ni kuanzia miezi 8 hadi mwaka baada ya kuajiriwa, na pale unapoona hujapewa barua baada ya muda huo kuisha Sheria inaelekeza kwamba wewe tayari unethibitishwa by pressumption.
3. Mwajiri wako alipaswa kukupa barua ya sababu ya kutokukuthibitisha kazini baada ya mwaka kuisha, kama hajafanya hivyo ni kwamba alishakuthibitisha isipokuwa hajakupa barua.
4. Kwenda kusoma postgraduate diploma ya ualimu maana yake unataka uhame kutoka kada ya uhandisi na kuingia kada ya ualimu, ukirejea uajiriwe na uanze upya( kataeni upuuzi huo) na anayewashauri hivi ni Afisa Utumishi asiye na akili au Afisa Elimu wa magumashi.
5. Kwakuwa mna miaka 3 kazini, bado mwaka mmoja tu msitahili kupanda daraja hivyo msipofuatilia haraka mnaweza kupoteza haki zenu kwani hamtakuwa kwenye eligible list kwa ajili ya promo kwenye mfumo wa HCMIS.
6. Mwenye Mamlaka ya Miundo ya Utumishi wa Umma Nchini ni Katibu Mkuu_ Utumishi na ndiye aliyetoa kibali muajiriwe kwa Kada hiyo na kupelekwa Shuleni, ni katika sura hiyo kuwa malalamiko yenu lazima yaelekezwe kwake yakiwa na barua zenu za ajira.
7. OR TAMISEMI ni wizara tumizi, inawatumia Watumishi huku wakiwa si wasimamizi wa Miundo na Mishahara, kwahyo malalamiko yenu mliwasilisha kwa watu wasiojua kitu mathalan ukute ziliangukia idara ya Elimu iliyojaa walimu wenzenu kama mlio nao huko.
8. Poleni, zingatieni taratibu hizo. Barua zote mlizowahi kuandika kwenye mamlaka mlizotaja mzitunze kwa matumizi ya baadaye maana kwenye Utumishi jambo likikaa vibaya kila mtu huruka, ni vyema zaidi kama zilipokelewa kwa Dispatch.
Ahsanteni na karibuni shambani tulime
Mizega.
Kila la kheri Mkuu, Halmashauri nyingi hazina Wahandisi hasa baada ya wengi kuhamia Tarura na Ruwasa baada ya Kuanzishwa kwake hizo taasisi, kwahiyo recategolization ingefanyika nyie wote mngehamia Idara za Ujenzi za Halmashauri iwapo mna Bachelor degree za Civil EngineeringShukrani Mkuu tunaufanyia kazi
Swala la kwenda kusomea PGD lisiwe swala la ulazima liwe option maana katika walioajiriwa kuna wengine walisomea ELImu ya ufundi(vocational teachers)
Pia swala hili katibu mkuu analijua maana alishawahi fikishiwa na Abdul nondo na akasema atalifanyia kazi lkn kimya mpk leo hawa vijana hawajui hatma yao katika hio ajira wakurugenzi na maafisa utumishi wao wanawaambia wanasubiri maelekezo toka juu huu mwaka wa 3 sasa unaenda kuisha. Na Huku tume ya waalimu haiwatambui pia.
Ikiwa hawa wahandisi wazalendo wanajitoa katika kuelimisha wadogo zao
Kikubwa serikali iwathibitishe hao wahandisi kwa fani zao lakini viendelee kuwa hapo mashuleni hii itasaidia baadae mtu atapanda daraja na cheo kutokana na taaluma yake. Na hata akitaka kuhama hawezi anza upya katika idara atakayohamia na pia itawasaidia serikali pale watakapoitaji wataalam.
Pia serikali iajiri walimu wa ufundi maana kuna kozi imeanzishwa pale MUST na vijana wanamaliza mwaka huu.
Pia hawana 1)barua ya ajira 2) mkataba wa kazi 3) barua ya kituo cha kazi 4) barua ya uthibitisho kazini. Kitu ambacho kinapingana na standing orders ya utumishi wa umma.
Katibu mkuu tamisemi tatua hili tatizo watu wajue wanaitumikia vp nchi yao.
Mkuu asante Kwa ushauri wako
Embu fikiria baadhi ya watu wameajiriwa na Diploma za Engineering lakini analipwa mshara wa TGTS C3,
Ana deni la bodi ya mikopo Kwa maana wakati anaajiriwa alikua final year ya Bachelor Degree in Engineering
Amejaribu kupeleka cheti cha Bachelor Degree in Engineering, Maafisa utumishi wanasema system haikubali hadi apeleke cheti cha ualimu Kwa maana bachelor degree in education (yaani akasome tena 3 years Kwa gharama zake)[emoji24]
ana familia, amepanga nje Kwa mshahara wa around 400K
Mkuu acha tu,
Mbona yuko sahihi
1. Diploma ya engineering ndio unaanza na TGS C
2. Kama umepeleka bachelor ya engineering then DHRO anasema "Ulete education" means kwasasa han uhitaji wa engeers.
Nakushuri hama halmashauri uende kwenye halmashauri zenye uhitaji halafu huko ndio ufanyiwe recategorization.
#YNWA
Mwenye TGTS C3 atapanda daraja baada ya miaka mingapi ili awe tgts DI na mwenye TGTS C1 atapanda daraja baada ya miaka mingapi awe tgts D I Naomba maelekezo, pole Kwa changamoto nitaifanyia kaziMkuu asante Kwa ushauri wako
Embu fikiria baadhi ya watu wameajiriwa na Diploma za Engineering lakini analipwa mshara wa TGTS C3,
Ana deni la bodi ya mikopo Kwa maana wakati anaajiriwa alikua final year ya Bachelor Degree in Engineering
Amejaribu kupeleka cheti cha Bachelor Degree in Engineering, Maafisa utumishi wanasema system haikubali hadi apeleke cheti cha ualimu Kwa maana bachelor degree in education (yaani akasome tena 3 years Kwa gharama zake)[emoji24]
ana familia, amepanga nje Kwa mshahara wa around 400K
Mkuu acha tu,
Mwenye TGTS C3 atapanda daraja baada ya miaka mingapi ili awe tgts DI na mwenye TGTS C1 atapanda daraja baada ya miaka mingapi awe tgts D I Naomba maelekezo, pole Kwa changamoto nitaifanyia kazi
Lakini soma tu hio postgraduate mambo yakuendee ukikaza fuvu/kukaidi maboss utapata shida sana
Kubali tu usome yaishe mkuu
Duuuh bora kuacha hiyo kazi,.Mkuu asante Kwa ushauri wako
Embu fikiria baadhi ya watu wameajiriwa na Diploma za Engineering lakini analipwa mshara wa TGTS C3,
Ana deni la bodi ya mikopo Kwa maana wakati anaajiriwa alikua final year ya Bachelor Degree in Engineering
Amejaribu kupeleka cheti cha Bachelor Degree in Engineering, Maafisa utumishi wanasema system haikubali hadi apeleke cheti cha ualimu Kwa maana bachelor degree in education (yaani akasome tena 3 years Kwa gharama zake)[emoji24]
ana familia, amepanga nje Kwa mshahara wa around 400K
Mkuu acha tu,
Mbna mnatutishaaa, tulikimbia ualimu, then turudi huko tena kwa mlango wa nyumaa, aaaaaaahMtoa mada chukua ushauri wa Mkuu Mizega , he has written it all.
Nilitaka nishauri kuhusu recategolization lakini najua haitawezekana kufanyika kama hamna barua ya kuthibitishwa kazini