Waraka kwa Rais Samia kuhusu vilio vyetu sisi Wahandisi tulioajiriwa kama Walimu

Waraka kwa Rais Samia kuhusu vilio vyetu sisi Wahandisi tulioajiriwa kama Walimu

Technical school hadi uwe na cheti cha ualimu ushamba wa wapi huo kosa waboreshe hizo shule ziweze kutoa fani mbalimbali kisasa zaidi wao wamelala vyeti havileti maendeleo sijui hao viongozi wenu walisomea wapi ?
 
Kwa mwezi kama laki nne , dah! Changamoto sana. Tunasafari ndefu kuwa sela nzuri ya ajira
Alafu na taasisi yetu ya ERB haijatilia mkazo, ukisoma mwongozo utaona tunavyopaswa kulipwa malipo mazuri zaidi, kama sijakosea Ukiwa PEng unapaswa kulipwa zaidi ya Dollar 250 kwa siku.

Waliokuwa na mishahara mizuri walau Wazungu, nakumbuka wakati nafanya nao kazi kwenye project yao moja walikuwa wakinilipa 50,000 kwa siku

Ila ukija kwa wenzetu Wachina na Wahindi ndiyo disaster 🙆
 
Nimefurahishwa Sana na kusikia rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr Samia Suluhu Hassan ni mtembeleaji mzuri wa jukwaa hili la Jamii forum na tunaamini atatusikia juu ya hiki kilio chetu

Sisi Wahandisi tulioajiriwa kama walimu katika shule za ufundi Tanzania ,

Bwiru boys secondary school
Mwadui secondary school
Moshi tech secondary school
Mtwara tech secondary school
Tanga tech secondary school
Iyunga tech secondary school
Ifunda tech secondary school
Musoma tech secondary school
Chato tech secondary school

Tuliajiriwa December 2020,
tunaenda Mwaka wa 3 huu kazini hatujathibitishwa, wala kupewa barua za ajira na hivyo kukosa baadhi ya stahiki za kiutumishi,

Swala letu tumelipeleka Kwa Wakurugenzi, Ma RAS mpaka katibu mkuu Tamisemi lakini hakuna majibu yeyote,

Wakurugenzi na TSC wanasema hawawezi kututhibitisha kazini kwakuwa hatuna sifa za ualimu, hadi tukasomee post graduate diploma in education.

Kwenye shule za ufundi kuna watu mfano kama laboratory technician wameajiriwa na wapo chini ya Mkurugenzi, na wamethibishwa kazini na sio walimu inakuaje Kwa Wahandisi (Engineers) ambapo Tangazo la ajira la September 7 2020 kipengele cha IV, hakikusema kwamba tukiajiriwa twende tukasome?

Lakini huku kweny halmashauri wanatudai twende tukasome tena Kwa gharama zako
Huu ni utaratibu wa wapi?

Tumejaribu kuandika barua Kwa katibu Mkuu Tamisemi tena sio moja lakini hakuna hata moja iliyojibiwa zaidi tu ya kusikia Kwa maafisa utumishi wakisema Tamisemi kuna utaratibu maalumu wanaouandaa, mwaka wa pili huu bila kuona chochote

Huku wale walimu tulioajiriwa nao, wakithibitishwa kazini na kutuzidi Kwa maana ya seniority

Tumekuwa tukipitia vipindi vigumu vya manyanyaso, msongo wa mawazo na kukosa Hali au morali ya kazi

Tunafanya majukumu ya kiualimu kama kushika zamu, kuandaa lesson plan ect bila ya mkataba wa ajira unaokuonesha majukumu ya kazi yako, au kujua kazi yako ni temporary au permanent

Ni heri ingewekwa wazi kama ajira zetu ni za mkataba Kwa maana ya temporary na wangespecify duration, ingetusaidia sana, Kwa maana Wakurugenzi wamekuwa hawapitishi barua za transfer ukipata sehemu nyingine wala hawapitishi barua za maombi ya kazi za utumishi ili twende kwenye Kada zetu tulizozisomea Kwa maana huku tulipo hawatutambui

ikikupendeza Mheshimiwa Rais tunakuomba Sana utusaidie kupata haki zetu Kwa maana ya kuthibitishwa kazini na kupatiwa barua ya ajira ili tuweze kufanya kazi Kwa Amani kwenye mioyo yeti na kuongeza weledi wa kazi

Kwani ni haki ya mtumishi akimaliza probation period ya mwaka mmoja kuthibitishwa kazini na kupewa barua ya ajira,

Naomba
Kuwasilisha
Dalili ya mvua ni mawingu mnatakiwa kutoka haraka huko almashauri hakuna issue

yaani engineer unaenda kushika chalk kizalendo kabisa ila hakuna mwenye mpango na wewe huko sio pa kufanya kazi.

Hizo ni dharau na kusababishana depression zisizo za msingi.
 
Kwaiyo Mkuu unaruhusu watu kuumia Kwa sababu ya kuwa na Perception kubwa?

Je kudai haki unayoamini ni yako ni vibaya?

Kwaiyo tuendelee kuwa hivi hivi? Bila kueleza linalotusibu?

Ni kweli mtaani ni pagumu lakini nafikiri isiwe excuse ya kuhalalisha ukandamizaji.
Utakuwa umeninukuu vibaya Mkuu, naomba unisome tena kwenye post iliyopita.
 
Alafu na taasisi yetu ya ERB haijatilia mkazo, ukisoma mwongozo utaona tunavyopaswa kulipwa malipo mazuri zaidi, kama sijakosea Ukiwa PEng unapaswa kulipwa zaidi ya Dollar 250 kwa siku.

Waliokuwa na mishahara mizuri walau Wazungu, nakumbuka wakati nafanya nao kazi kwenye project yao moja walikuwa wakinilipa 50,000 kwa siku

Ila ukija kwa wenzetu Wachina na Wahindi ndiyo disaster 🙆
Kuna wenzenu walikuwa nafanya kazi mradi mmoja mkubwa ila wasimamizi wachina graduated engineer wanalipwa laki na kumi na nae kwa wiki..

From there nilijua maana halisi ya ile point maaruf ya kikoloni "African cheap labour"
 
Dalili ya mvua ni mawingu mnatakiwa kutoka haraka huko almashauri hakuna issue

yaani engineer unaenda kushika chalk kizalendo kabisa ila hakuna mwenye mpango na wewe huko sio pa kufanya kazi.
Usimkatishe tamaa huyo Mhandisi/Mkufunzi. Kupitia huko alipo anaweza kufanyiwa recategolization akarudi kwenye taaluma yake ya Uhandisi
 
Kuna wenzenu walikuwa nafanya kazi mradi mmoja mkubwa ila wasimamizi wachina graduated engineer wanalipwa laki na kumi na nae kwa wiki..

From there nilijua maana halisi ya ile point maaruf ya kikoloni "African cheap labour"
Hao jamaa wahuni sana kwenye malipo, they don't care kabisa. Ingawa hili linafanyika kwa kuwa Mamlaka zimelala
 
Nimekuelewa
Dalili ya mvua ni mawingu mnatakiwa kutoka haraka huko almashauri hakuna issue

yaani engineer unaenda kushika chalk kizalendo kabisa ila hakuna mwenye mpango na wewe huko sio pa kufanya kazi.

Hizo ni dharau na kusababishana depression zisizo za msingi.
 
Aisee [emoji119]
Kuna wenzenu walikuwa nafanya kazi mradi mmoja mkubwa ila wasimamizi wachina graduated engineer wanalipwa laki na kumi na nae kwa wiki..

From there nilijua maana halisi ya ile point maaruf ya kikoloni "African cheap labour"
 
Hata sijajua leseni ya kufundishia unaipataje?

Naomba Tips Mkuu
Utaratibu hapo ni utatakiwa kuwa na Mkataba na mwajiri, then utajaza Fomu Na. RT 4 ambayo ndio fomu ya maombi ya leseni pamoja na Fomu Na. RS 3 ambayo ni fomu ya kuwekwa kwenye rejesta.

Changamoto ninayoiona hapo ni kama hauna mkataba wa ajira, ila kama unao utakuwa umeruka kiunzi kikubwa.

Kama utaona changamoto cheki na Wakili aliye karibu akufanyie hiyo kazi. Tofauti na hapo itabidi ukomae kibingwa ndugu yangu.

Kila la kheri.
 
Pole mkuu nje ya mada, sisi tulioajiriwa Nirc kama Agriculture engineer (civil) tukipata nafasi ya kuamia taasisi nyingine itabidi tufanye recategorization?
 
Hapo ndiyo utaipenda serikal... Hata muishinikize vipi haiwezi kufanya mnavyotaka ninyi... Niwashauri pamoja na kuandika barua ombeni kikao kazi na Katibu Mkuu TAMISEMI mtapatiwa majibu mazuri zaidi... Kuna sehem umeandika kuna utaratibu maalum mmeambiwa unaandaliwa, amini huo utaratibu upo, maana serikal haiwezi kuajiri watu na kuwaacha hewani... Sikuzote taratibu za serikal si za haraka hupitia chanels mbalimbali... Ushauri mwingine kama kuna mtu ana afford kwenda kusoma Postgraduate akasome ni mwaka 1 tu... All in all serikal ni sikivu sikuzote
 
Asante Kwa ushauri wako Mkuu, tumekusikia

Re-categorization kwani unatoka kutoka uhandisi kwenda kada nyingine?

Kama sio basi ni transfer Tu utafanya
Pole mkuu nje ya mada, sisi tulioajiriwa Nirc kama Agriculture engineer (civil) tukipata nafasi ya kuamia taasisi nyingine itabidi tufanye recategorization?
 
Nimefurahishwa Sana na kusikia rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr Samia Suluhu Hassan ni mtembeleaji mzuri wa jukwaa hili la JamiiForums na tunaamini atatusikia juu ya hiki kilio chetu.

Sisi Wahandisi tulioajiriwa kama walimu katika shule za ufundi Tanzania.

Bwiru Boys Secondary School
Mwadui Secondary School
Moshi Tech Secondary School
Mtwara Tech Secondary School
Tanga Tech Secondary School
Iyunga Tech Secondary School
Ifunda Tech Secondary School
Musoma Tech Secondary School
Chato Tech Secondary School

Tuliajiriwa December 2020, tunaenda Mwaka wa 3 huu kazini hatujathibitishwa, wala kupewa barua za ajira na hivyo kukosa baadhi ya stahiki za kiutumishi.

Swala letu tumelipeleka Kwa Wakurugenzi, Ma RAS mpaka katibu mkuu Tamisemi lakini hakuna majibu yeyote. Wakurugenzi na TSC wanasema hawawezi kututhibitisha kazini kwakuwa hatuna sifa za ualimu, hadi tukasomee post graduate diploma in education.

Kwenye shule za ufundi kuna watu mfano kama laboratory technician wameajiriwa na wapo chini ya Mkurugenzi, na wamethibishwa kazini na sio walimu inakuaje Kwa Wahandisi (Engineers) ambapo Tangazo la ajira la September 7 2020 kipengele cha IV, hakikusema kwamba tukiajiriwa twende tukasome?

Lakini huku kweny halmashauri wanatudai twende tukasome tena Kwa gharama zako. Huu ni utaratibu wa wapi? Tumejaribu kuandika barua Kwa katibu Mkuu Tamisemi tena sio moja lakini hakuna hata moja iliyojibiwa zaidi tu ya kusikia Kwa maafisa utumishi wakisema Tamisemi kuna utaratibu maalumu wanaouandaa, mwaka wa pili huu bila kuona chochote.

Huku wale walimu tulioajiriwa nao, wakithibitishwa kazini na kutuzidi Kwa maana ya seniority. Tumekuwa tukipitia vipindi vigumu vya manyanyaso, msongo wa mawazo na kukosa Hali au morali ya kazi. Tunafanya majukumu ya kiualimu kama kushika zamu, kuandaa lesson plan ect bila ya mkataba wa ajira unaokuonesha majukumu ya kazi yako, au kujua kazi yako ni temporary au permanent.

Ni heri ingewekwa wazi kama ajira zetu ni za mkataba Kwa maana ya temporary na wangespecify duration, ingetusaidia sana, Kwa maana Wakurugenzi wamekuwa hawapitishi barua za transfer ukipata sehemu nyingine wala hawapitishi barua za maombi ya kazi za utumishi ili twende kwenye Kada zetu tulizozisomea Kwa maana huku tulipo hawatutambui.

Ikikupendeza Mheshimiwa Rais tunakuomba Sana utusaidie kupata haki zetu Kwa maana ya kuthibitishwa kazini na kupatiwa barua ya ajira ili tuweze kufanya kazi Kwa Amani kwenye mioyo yeti na kuongeza weledi wa kazi.

Kwani ni haki ya mtumishi akimaliza probation period ya mwaka mmoja kuthibitishwa kazini na kupewa barua ya ajira.

Naomba
Kuwasilisha
Kama nyie siyo walimu ilikuwaje mkaajiriwa

Pili kwaani mtumishi asiye mwalimu hathibitishwi mpaka akasome?
 
Back
Top Bottom