WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini


Subiri shughulikiwe na USALAMA WA KANISA na USALAMA unaujua wewe.
 
Hii Rafiki hata TBC hutokaa uisikie na kuna siku hata Youtube itafanyiwa editing ni vizuri tuaziweka vyema hizi record
Hayati Nyerere alikuwa na vision kubwa alichokisema kipo sawa kabisa.Tuseme hapana.
 
.....hao wakatoliki ndo walio muweka, unakumbuka Lowassa aliwaambia Waanglikana wenziwe kuwa sasa ni zamu yao !? ....nothing can happen, wataishia kupakana majivu tuu !
 
Kuna mzee aliwahi kuniambia Kanisa Katoliki lina inteligensia kubwa sana labda hata kushinda dola. Ikitokea hali yoyote ya sintofahamu huwa wanahusika kuhifadhi viongozi.
 
UZURI WA WAKATORIKI HAWATEGEMEI HISANI/MISAADA ILI KUJIKOMBA KAMA TAASISI NYINGINE
 
Mkuu akikujibu ntaomba uni-tag hilo jibu lake.. Maana aina ya uandishi wa comments zake, umeegemea kwenye arrogance zaidi kuliko facts..
Na mimi nimevulia hayo, naona meneno mengi swali langu la msingi hajajibu.
 
Huyu mtu ni kama hana kijipuuchungu cha mawazo, hivyo usishangae akakurupuka na kuliambia baraza hili linawashwawashwa.
 
Hapa Maaskofu na Kanisa kwa ujumla wake wasubiri Matusi kutoka kwa vijana wa awamu ya tano.


UNAWEZA KUTUAMBIA JINA LA HUYO PADRI AMBAYE JINA LAKE LIMEHIFADHIWA NA KWA NINI JINA LIKAHIFADHIWA ???

Unaweza kutuambia hii kesi iliishaje ???


PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, akionyesha bunduki aina ya AK47 kati ya silaha zilizokamatwa katika msako maalum wa ujangili.


Na Daniel Mbega, Namanyere


PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga (jina linahifadhiwa) ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa kwa ujangili na Kikosi Kazi cha Taifa katika Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa.
Padri aliyekamatwa ni wa Parokia ya Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambaye bunduki yake aina ya Rifle yenye darubini inadaiwa kutumika katika ujangili ndani pori hilo la Lwafi wilayani humo.
Taarifa za kipolisi zimeeleza kwamba, mbali ya kukamatwa kwa watu hao, pia jeshi hilo limekamata bunduki 48 za aina mbalimbali ikiwemo ya Padri huyo anayoimiliki kihalali, pamoja na risasi 764 na maganda ya risasi 101.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jacob Mwaruanda amesema kuwa baadhi ya waliokamatwa silaha zao wanazimiliki kihalali lakini zinatumika kinyume na utaratibu wa kumilikishwa kwao.
"Watu hawa bado wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Mwaruanda.
Kamanda Mwaruanda alisema kati ya bunduki 48 imo moja ya kivita aina ya AK47, bunduki 8 aina ya Rifle na risasi zake 83, Shortgun 19 na risasi zake 138, bastola 5 na risasi zake 133, magobore 15, magazine nne za bunduki aina ya Sub-Machine Gun, maganda matano ya bunduki aina ya Rifle, maganda 96 ya risasi za bunduki ya shortgun pamoja na vifaa vya kutengenezea bunduki za kienyeji na mitutu sita.
Watuhumiwa hao walikamatwa pia na nyara za serikali ambazo ni mikia sita ya tembo, nyama ya nyati kilo 20, miba ya nungunungu, ngozi moja ya paka-pori na pembe ya Nshya.


Kamanda Mwaruanda akifafanua jambo huku nyuma yake wanaonekana maofisa wa Kikosi Kazi cha Taifa pamoja na askari wa wanyamapori.


Kama Mwaruanda alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa kwamba watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja kwenye vituo vya polisi au ofisi za serikali za vijiji kabla operesheni kabambe ya kuwatafuta watu hao haijaanza.

Rukwa na Katavi ni miongoni mwa maeneo ambayo ujangili kuua tembo umeshamiri sana hasa katika mapori ya akiba ya Lwafi na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana meno ya tembo kuonekana kuwa na soko katika mikoa mingine nchini na nchi jirani.

Kamanda Mwaruanda akionyesha kigudulia ambacho hutumiwa na majangili kubebea risasi.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Davies Mushi alinukuliwa hivi karibuni kuwa kuwepo kwa soko zuri la biashara haramu ya nyara za Serikali hususan meno ya tembo ni moja ya sababu zinazochangia ongezeko la ujangili katika hifadhi hizo.
"Soko zuri la meno ya tembo lililopo katika mji wa Mpanda (Katavi), Sumbawanga (Rukwa), Tabora na maeneo mengine ya nchi linachangia sana kushamiri kwa ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, lakini tunajitahidi kufanya doria ndani ya hifadhi na kukabiliana na kasi hii iliyopo ya kuua tembo inayofanywa na majangili ambao wengi wao ni kutoka nje ya nchi," alisema Mushi.
Posted by Daniel Mbega at Wednesday, April 29, 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…