rais wangu piga kazi. hachana na mbwembwe hizo. Serikali haiendeshwi kwa madongo madongo kama hayo. Kwani wao wanaujua mzigo raais alionao? watu wafanyekazi. Siasa mpaka 2020
Tatizo ni kwamba hii siyo nchi ya mtu mmoja. MUACHENI AFANYE KAZI! Hakuna anayetaka wala hakuna anayeweza kumzuia Rais kufanya kazi, ila yeye ndiyo hataki wengine wafanye kazi. Hataki vyama vya siasa vifanye kazi wala hataki mihimili ifanye kazi yake kwa mujibu wa katiba.
Yaani unawezaje kumzuia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufanya kazi? wewe ni nani? Inavyoonekana Amiri jeshi huyu wa sasa wa Tanzania ana hofu kiasi kwamba hata chama cha siasa kisichokuwa na jeshi wala silaha, anakiogopa. Hii nchi ina Taasisi na mifumo mbalimbali ambayo yote inatakiwa kufanya kazi. Kuna taratibu za kikatiba za watu kukosoa na kupongeza, na kwa ujumla kutoa mawazo yao. Kuna mihimili ya Bunge, Mahakama, na Serikali, ambayo kila moja ina kazi yake na majukumu yake.
Amiri Jeshi wetu ni mwoga sana kiasi hataki mihimili mingine ifanye kazi yake kwa kujitegemea na uhuru kwa mujibu wa Katiba. anataka awe yeye tu. Na hata alivyosema hakuna siasa mpaa 2020, mwenyewe ameendekeza siasa tena za kijinga, kwa kukwapua wabunge waliochaguliwa na wananchi, na kuwalazimisha warudi tena kwenye uchaguzi! Ndiyo kuchapa kazi huko? kutuingiza hasara za kijinga?
Na bado ana mashitaka mengi tu. hiki kitendo cha kuruhusu ubaguzi wa kiitikadi, kiasi kwamba viongozi wanadiriki kutamka hadharani kwamba ukichagua mtu wa CCM ndio mtapata maendeleo, wakati fedha ni zetu sisi wote, Serikali ni mgawaji tu, huo ni UHAINI. Na ni DHAMBI KUBWA SANA. MAGUFULI ANATAKIWA KUTUBU.
Mwisho, kauli ya Maaskofu siyo ya kubeza. wameitoa iikiwa miaka miwili imepita ya serikali hii. hawakuwa na haraka, wengi wamewalaumu kwa kukaa kimya muda mrefu. wamejitafakari kabla ya kuitoa. Magufuli ajipange, ajipime. Kuwabeza viongozi wa dini pale wanaposimama kwenye UKWELI, NI JAMBO LA HATARI SANA.