WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Na Pascal Mwanache, Dar

MAASKOFU wanaounda Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wametoa ujumbe wa Kwaresima kwa 2018, huku wakionya kuhusu kuminywa kwa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari


Maaskofu wamesema kuwa shughuli za siasa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Wamesema kuwa shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila raia, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi.

“Vile vile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza uwigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari, maoni na wa kujieleza. Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambaba na kuminya uhuru wa mahakama na bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya Kikatiba” wameongeza.

Gazeti la Kiongozi.
Sijaona uhusiano wa mikutano ya kisiasa na Kwaresma, naomba mnijuze tafadhali!
 
Wameanza kujitambua sasa......good ila kuna mmoja atakuja kukana hili tamko. Time talks a lot
 
Je hili nalo ni tamko la kichungaji kama yale ya awamu ya nne?.
 
Sasa huu ni wa aina yake, maana haijawahi kutokea Baraza lenyewe likatoa tamko kali hivi. Huko nyuma matamko ya Kanisa yametolewa na kamati za Baraza, na siyo Baraza lenyewe. Na baadhi ya Maaskofu waliweza kutamka kutokubaliana. Hili ni tofauti. Hii ni rasmi kabisa ya Baraza zima na kama unavyoona kule mwisho Maaskofu wote wamejiorodhesha. siyo mchezo.
Hii ni kawaida na ni kila mwaka kanisa linapoelekea katika kipindi cha toba. Nimebahatika kuwa na nyaraka hizi kwa muda mrefu sasa
 
Back
Top Bottom