WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini



Kwani JPM siye chaguo la mungu ???
 
Hao maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania ni wasemaji maneno matupu bila matendo kama wenzao wa nchi ya DR Congo.

Waraka wa wajumbe TEC ni kelele za debe tupu hayana athari kwa serikali yao kama mnavyoona sasa kinachoendelea nchini.
"Waraka" ambao kiukweli ni "UJUMBE WA KWARESIMA" una sura nne, mbona mnadandia mada? Kwanini msisome na sura nyingine?
 
Wakati wa JK maaskofu wakiongea utaskia , mfumo kristo huo, wakati huu, walivokuwa kimya utaskia hawaongei kwasababu mwenzao, sasa wameongea utaskia walikuwa wapi muda wote, waislam Mungu anawaona mjue.
 
Somehow jamii sasa inatambua kuwa hawa jamaa wako against na yanayofanyika hapa kwetu kwenye kisiwa cha.......
 
Mara nyingi nyaraka za wakatoliki huwa zinatetemesha sana serikali

Hasa zile serikali ambazo Marais wake huwa ni Waislam daima huandamwa na kanisa kwa nyaraka lukuki. Lakini akitawala mkatoliki mwenzao daima kanisa hujifanya halioni kinachoendelea na hata likitoa waraka huwa unakuwa na lugha ya kubembeleza hivi. Hili ndilo kanisa katoliki mara zote liko kimaslahi zaidi.
 
Ni kama unafiki;
Watu pekee wanaoweza kusikilizwa kirahisi na rais ni viongozi Wa dini;
Maaskofu kila siku wapo na rais huko makanisani wanashindwaje kumkanya? Mtu ambaye kila jumapili mpo naye kanisani sioni haja ya kupoteza sadaka za waumini kukaa kikao ili kuandaa waraka Kwa ajili ya kufikisha ujumbe.
Pamoja na nia ya kuwasemea wananchi, maaskofu wanao uwezo Mkubwa Wa kuomba appointment ya kumuona rais na kumwambia!.

Nashauri rais asipoteze mda kuwajibu maana wameonyesha unafiki;
Haiwezekani mtu unakaa naye meza moja ukamwandikia barua kupitia njia ya Posta!

VIONGOZI WA DINI NDIO ZAO LA KUPATA VIONGOZI HAWA TULIONAO
 
Kwani wewe ndiwe Rais? Au wewe ndiye mwandaaji wa ratiba zote za Rais? Una uhakika gani maaskofu hawakutani naye? Una uhakika gani hawamwelezi hayo? Lakini ule waraka ulijaa mambo mengi ya msingi sio kwa Rais tu; na wala haukumlenga Rais bali ulilenga wote "wenye mapenzi mema".

Kama una mapenzi mema ule waraka hauwezi kukureka kamwe! Na sidhani hata Mh. Rais mwenyewe kama unamkera zaidi ya kukera vibaraka kama ninyi ambao mnadhani mna uzalendo kuliko watanzania wote wakiwamo Wahashamu Maaskofu. Swali muhimu katika waraka ule "Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"; tafakari!
 
Katika ujumbe wako huu kuna sehemu umepatia na kuna sehemu umeboronga, ujue nafatilia sana topic zako na huwa nazipenda ila kwa hapa km nilivyokuambia. Ila tusiulizane
 
Kwani kwenye waraka wao umeona kuna sehemu maaskofu wameomba wajibiwe na Rais au ndo kuwashwa kwenyewe!!!!?
 
Kwanza hakuna waraka uliyoandikwa kwa rais isipokuwa kuna waraka unaozungumzia hali ya siasa inayoashiria ukosefu wa haki na hatimaye amani

Wanaoona ujumbe ulioko kwenye waraka unafaa kwa mustakabali wa amani ya watanzania na wanajukumu la kusimamia haki basi ni muda muafaka kujitafakari

Waraka unawakumbusha hasa waumini wakatoliki hasa wajibu wao kama wakristo

Waraka una kurasa ishirini na wamezungumzia siasa kurasa mbili tu lakini unaochoma sana kwa wale wanasiasa wasiopenda haki japo haki hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu

Kwa hiyo nia ya waraka kwa ujumla siyo siasa bali imekuwepo kama agenda mojawapo kwa hali inavyoenda ndani ya nchi

Kumbuka wanasiasa ni wengi ndani ya nchi kwa hiyo ujumbe si kwa rais pekee kama unavyotaka kutuaminisha

Pia hakuna dhehebu au dini liko karibu na rais kuliko nyingine kama unavyofikiria kuwa maaskofu wako karibu na rais kuliko mashekhe. Rais ni wa watanzania, Maaskofu ni kwa ajili ya wakristo na Mashekhe ni kwa ajili ya waislamu
 
Umesoma sura zote nne za "UJUMBE WA KWARESIMA"? Usiandike ili kupata likes za JF bali kuelimisha. soma Sura ya kwanza "BASI ENENDENI", Sura ya pili "SASA NI ZAMU YETU" Sura ya tatu "MIMI NI MLINZI WA NDUGU YANGU?" Sura ya nne "NIMRUDISHIE BWANA NINI?" hapo utapata ujumbe kamili waliotaka jamii iupate na kuufanyia kazi.
 
Maamuzi halali ya taasisi yoyote yamewekewa utaratibu, bila kufuata utaratibu maamuzi huwa batili, nafikiri ni vizuri kuheshimu utaratibu wa kanisa, kama una hoha za msingi sema
 
Ukweli unauma waliyoyasema ndo kilio cha walio wengi wanaopinga ni wanufaika tu
 
Toa povu liishe kabisa. I can guess wewe ni mmoja wa waliotumbuliwa. MUACHE RAIS APIGE KAZI. Period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…