WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Natabiri case ya wale "wachunga kondoo" wa RC waliopokea zile hela za ESCROW kufufuliwa upya
 
Ila kiukweli hata RC no zinasomeka sasa hivi,sadaka ziko hoi,vyuo vyao wanavyomiliki siku hizi inapita hata miezi 4 wahadhiri hawajalipwa hela zao ni Changamoto pia wanazipitia.
 
Pengo atasema sio kauli ya wakatoliki, maana anaagenda yake anayoijua yy mwenyewe
 
Safi sana Hii ndio inatakiwa kuwa Nguzo ya Dini Zote kuhoji inapobidi sio wale ma shekhe uchwara wanaotumiwa dola
 
Ila kiukweli hata RC no zinasomeka sasa hivi,sadaka ziko hoi,vyuo vyao wanavyomiliki siku hizi inapita hata miezi 4 wahadhiri hawajalipwa hela zao ni Changamoto pia wanazipitia.
Chuo gani kwa mfano ?
 
Sidhani kama Serikali itakuwa na haraka sana kuanza ligi na Kanisa Katoliki. ni kitu kimoja kumhoji uraia Askofu NiweMugizi, au kukagua mpaka nguo za ndani za mke wa Askofu Kakobe, lakini ni kitu kingine kabisa kuanzisha ligi na Kanisa Katoliki lenyewe.

Unaanzishaje Ligi na kanisa katoliki ukiangalia mkoa kama Rukwa una hospitali moja tu ya serikali na zilizobaki za wakatoliki. Ukianzisha ligi wakafunga hospitali zao unategemea watu wa mkoa mzima wa Rukwa wakatibiwe katika hospitali moja tu ya serikali. Tegemea vifo kama kuku kwa watu wa Rukwa
 
Waambieni hao maaskofu, huyu wa sasa hajaribiwi! Wasije wakasema sikuwaonya mimi
 
Hili kanisa ni chochezi na chonganishi kati ya Rais na wananchi wake. Ni lazima vyombo vya uasalama kulichunguza kuundani zaidi kuna maaskofu wapo nje ya maadili yao ya kichungaji na wanachanganya siasi na dini ndani ya Tanzania.

Ninaomba Serikali kupitia kwa msemaji wake hata yeye Bwana mkubwa aliangalie hili kwa karibu na kulikemea kanisa na maaskofu wote waliohusika kuandaa waraka huu wakamatwe wahojiwe kama viongozi wengine wa dini waliotamka mambo ya siasa tena ya kidini kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanapaswa kutubu dhambi zao.

Sasa hao hawajasema kutubu tu bali wamesema ni dhuluma kwa haki na demokrasia hapa nchini.

Kama hili halitafanyika Kuanzia sasa nitajia kabisa hapa nchini kuna ubaguzi mkubwa wa Kidini, kwamba kwa kuwa wenye mamlaka wanatoka dini hii kuu ya Katoliki sasa wana haki ya kusema chochote hata kama kinawagombanisha Rais na watu wake na kuharibu amani ya nchi kwa kumfanya Rais mkiukwaji wa Katiba iliyomuweka madarakani NA kwamba Rais yupo juu ya katiba.

Pole Tanzania.

Lakini ni mwanzo mzuri sana kwa nchi yetu kama hata viongozi wa dini sasa wanatambua kwamba nchi hii inaendeshwa Kidicteta bila ya kufuata katiba na sheria za nchi.

Pia ninafikiri wamesoma na kufuatilia kwa karibu hatua za Wenzao wa Kongo kwa Kumuadabisha Rais Kabira.
 
Hatimaye maaskofu katoliki wameamua kufunguka hakika historia itawakumbuka. Kama walivyosema "Tukiiachia hali hii izoeleke tushishangae huko mbeleni kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa" Huu utabiri wao ukitimia taahadhari hii itawasafisha na kuwaweka huru.
 
Baada ya miaka mitatu ya uonevu, unyanyasaji na uvunjaji wazi wa katiba ya JMT ndio KATOLIKI WANAFUNGUKA. Ni bora kuchelewa kuliko kutosema kabisa.

Pamoja binafsi naona hamkutenda haki kwa kuchelewa sana, lakini sina wajibu kuwapa HONGERA. Hapa huenda Magufuli Dr haambiliki akafungua masikio na kusikia kilio cha Silaha ya mwisho anayeitegemea. Hana ujanja bila hili baraza.

Sasa akina Kakobe na wenzake waliotangulia kuikosoa serikali mapema inawashirika wengi. Sijui kama TRA watawafuata maaskofu hao na kuwapekua pekua. Haya ni yao mimi siwasemei.

Amebaki mmoja tu, SHEIKH MKUU WA MKOA (sheikh ubwabwa) WA Dar es salaaam na BAKWATA yake.
 
Sasa huu ni wa aina yake, maana haijawahi kutokea Baraza lenyewe likatoa tamko kali hivi. Huko nyuma matamko ya Kanisa yametolewa na kamati za Baraza, na siyo Baraza lenyewe. Na baadhi ya Maaskofu waliweza kutamka kutokubaliana. Hili ni tofauti. Hii ni rasmi kabisa ya Baraza zima na kama unavyoona kule mwisho Maaskofu wote wamejiorodhesha. siyo mchezo.
Wamechoka kuona waTZ tunanyanyaswa kwa kuvunja katiba waziwazi!!
Bunge liko wapi??
 
Hapa naona pia kuna habari ya Kingunge kukataliwa na Kanisa kwa sababu ya upinzani wake. Tofauti gani na Kanisa kujitoa katika kumhudumia Kingunge? Si ni mtu kujitenga mwenyewe kwanza? Sidhani kama Baba Askofu walikuwa wanasema haya bila kujua hali halisi iliyopo katika upinzani, kwamba tofauti zao si la kifalsafa bali za ubinafsi na ukabila. Hata uwae nini hawakubali, nia yao wachukue madaraka kwa faida ya wachache, watu wa kwao. Nchi hii ni changa, watu wengi walalahoi, hawataki sophistry ya upinzani, wanataka matokeo. Hawataki fujo, wanataka amani. Wanataka kulima na kusoma, siyo mikutano na maandamano yasiyoisha.

Mababa Askofu wamethibitisha ukweli wa umoja na mshikamano kwa jinsi walivyomfanyia Marehemu Kingunge - alijitakia mwenyewe, kwa nini ayumbishe Kanisa zima? CHADEMA wamejitenga wenyewe kwa misingi ya ukabila na ukanda, kwa nini waiyumbishe nchi? Sasa angalia hii ya Kenya: tunataka uhuru kama huu, wasomi wa Chadema si watatumaliza?



Na sisi, je, tunataka hii?
 
This is hom of great thinkers kama hata hilo unaomba ufafanuzi its better ukaenda kufanya mazoezi huko facebook tunahitaj watu wakomavu kifikra.
ungeeleza wa nje yupi wa ndani nani usingemaliza mistari yote hyo..great thinker ana subira
 
Huyo askofu hua ni mbabe,straightforward afu mkimya mkimya hivi kama hayupo hivi kumbe ana observe tu
Sindano imewaingi ee...????
Sasa mtulie mupewe ukweli japo hilo sio dhamira yenu na huwa hamupendi.

Waraka wa Kanisa Katoliki haujawahi liacha Taifa lolote salama pale ulipopuuziwa na viongozi waliojawa Viburi na Dharau kwa maisha ya hapa Duniani na mifano ipo.
 
Back
Top Bottom