baby s
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 487
- 323
Hilo linafiki tunalijuaga tu halitupi shida
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hilo linafiki tunalijuaga tu halitupi shida
Ni laana au nini ??WAANZE NA WEWE MNAFIKI MKUBWA!
MNAUANA WENYEWE KWA MAKAFARA KWA AJILI YA RUZUKU ALAFU UNATUSUMBUA KWA VISENTI UNAVYOLIPA ILI UONEKANE UMEANZISHA UZI. BLADIFUL, MPUMBAVU WEWE NENDA KATAFUTE KAZI UZEE UNAKUJA PAMBAF
Yanayotokea Tanzania yanaogofya kwa kweliswali lako la hadi wangapi wauawe lmenikumbusha civil war ya Liberia Foday Sankoh akaibatiza ile vita jina la Operation No Living Thing.
Wakati vita inaendelea kuna jamaa alikua anachukua video, anaitwa Sorious Samura documentary ikaitwa Cry Freetown. Kuna jamaa akiwa anahojiwa akasema..
"Ameanzisha vita ili atawale milele mara ghafla anaanzisha operation ya kuua kila mtu sasa atamuongoza nani?"
Mjaa laana ww!WAANZE NA WEWE MNAFIKI MKUBWA!
MNAUANA WENYEWE KWA MAKAFARA KWA AJILI YA RUZUKU ALAFU UNATUSUMBUA KWA VISENTI UNAVYOLIPA ILI UONEKANE UMEANZISHA UZI. BLADIFUL, MPUMBAVU WEWE NENDA KATAFUTE KAZI UZEE UNAKUJA PAMBAF
HAKIKA!Mjaa laana ww!
Wamebaki kukusanya sadaka tuu, kwa kifupi hamna viongozi wa dini, viongozi wa michango, michango, michangoAliuawa Mwangosi, mkakaa kimya ?
Kapotea Saanane, mko kimya ?
Azory ?
Watu wanaokotwa kwenye viroba Daily COCO BEACH mko kimya ?
Daudi wa Hanananif,
Aquiline kauawa kikatili
Hivi Tanzania tuna viongozi wa dini kweli aina ya YOHANA MBATIZAJI aliyemkemea HEROD waziwazi baada ya HEROD ( MFALME ) kuchukua mke wa nduguye ?
Tatizo ni nini kwa viongozi wa dini, HATUNA VIONGOZI WA DINI, NJAA, KUJIPENDEKEZA KULIKOPITILIZA, UOGA au nini ?
KWANZA NIKUPE LIKEHivi unajua maana ya NEWS? Maneno ya Kichungaji huwa tunayasoma mara kwa mara, lakini pale Maaskofu wanaamua kutoa ujumbe mkali wa kisiasa, tena kwenye charged atmosphere kama hii ya kwetu kwa sasa hivi, ni lazima moto uwake tu. kuna hali tete nchini hivi sasa, na Maaskofu wanaongelea "Kusoma Alama za nyakati" Ni Maaskofu wenyewe walioamua kuweka ujumbe mkali sana wa kisiasa katika Waraka wao wa Kwaresima. ni kauli ya kwanza kutolewa na Baraza la Maaskofu tangu limeanzishwa, kauli kali kwa kiwango hiki, tena umesainiwa na Maaskofu wote. Ni statement ya Kanisa Katoliki Tanzania. Ni Historia. sasa ni bahati mbaya kwamba hayo yamewekwa katika Waraka wa Kwaresima, ambao bila shaka una mambo mazito ya kiroho kama unavyosema. lakini bado hata katika Nukuu yao ya Biblia: "Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?" wamechagua nukuu ya kimapinduzi, inayowaamsha walengwa waamke na kuchukua hatua. tunaweza kujadili zaidi hili katika muktadha wa kidini, lakini bado overtones kubwa zaidi ni za kisiasa, tena zikilenga taifa zima la Tanzania, siyo waamini tu.
Unaweza pia kusema Maaskofu wametonesha kidonda. Wanaongelea kuzuiliwa mikutano ya vyama vya siasa, kufungiwa vyombo vya habari, na wanatamka bila kupepesa macho: HUU NI UKIUKWAJI WA SHERIA NA KATIBA. Halafu ipite hivi hivi tu? Katika mazingira ambayo mtu mwingine aliyekosoa vikali serikali, alipigwa zaidi ya risasi 38, na bado anauguza majeraha nje ya nchi, na serikali imegoma kumtibu ikidai eti taratibu hazikufuatwa. hivi unapookoa maisha ya mtu unafuata taratibu gani? maana hata AMBULANCE HAIFUATI TAA NYEKUNDU WALA NJANO, NI MOTO CHINI KUOKOA MAISHA YA MTU. sasa Serikali inataka kwa suala la Lissu AMBULANCE ifuate foleni????
Katika mazingira ambayo Ben Saanane alipokosoa Digrii ya Mkulu, amepotea. yule mwandishi wa gazeti la Mwananchi naye kapotea, alikuwa anaandika vitu ambavyo serikali haipendi. Katika mazingira ambayo Askofu wa Kanisa Katoliki, Askofu NiweMugizi, anasumbuliwa na vyombo vya dola kuhusu uraia wake, baada ya kujitokeza kudai Katiba mpya, jambo ambalo Mkulu amesema hataki kusikia. Katika mazingira ambayo Askofu Kakobe aliyehoji mambo kadhaa ya serikali, ameishia kuchunguzwa na TRA kama hana miradi ambayo haijalipiwa kodi, na akasachiwa hadi chupi za mkewe, midume inatafuta miradi sijui miradi gani kwenye chupi za mama Askofu???
Katika mazingira hayo yote, wanajitokeza Maaskofu ambao wanaikosoa serikali hii ya kibabe, lazima pia kuwe na TAHARUKI. hawatahojiwa uraia? hawatapekuliwa? hawatapelelezwa miradi isiyolipiwa kodi? Lazima kuwe na TAHARUKI.
Uwe makini sana na maneno yako. Usijisahau ukazani Upo salama unaweza kupatikana ulipo.WAANZE NA WEWE MNAFIKI MKUBWA!
MNAUANA WENYEWE KWA MAKAFARA KWA AJILI YA RUZUKU ALAFU UNATUSUMBUA KWA VISENTI UNAVYOLIPA ILI UONEKANE UMEANZISHA UZI. BLADIFUL, MPUMBAVU WEWE NENDA KATAFUTE KAZI UZEE UNAKUJA PAMBAF
Hakika uko sahihi. Tanzania tuna bahati mbaya kweliWamebaki kukusanya sadaka tuu, kwa kifupi hamna viongozi wa dini, viongozi wa michango, michango, michango
unaweza kueleza kazi zinazotakiwa kufanywa ni zipi? serikali haiendeshi hivyo kama biashara ya nyanya.Unaweza eleza kazi mnazozifanya tangu mumeingia madarakani 2015..???
Hata nyumba za serikali ni gharama kubwa tu, watu wanapeana kama karanga, na wanadunda na nyie mnashangilia kama mazuzu. hata kujenga kiwanja cha ndege kikubwa kule Chato ni gharama kubwa sana, tena isiyo na sababu. EPA ilikuwa fedha zilizochotwa kugharimia uchaguzi kwa ajili ya CCM. za ESCROW walizochota wakubwa wala hatujui kinachoendelea. hapo JPM wala hatii neno, atasema "hataki kufukua makaburi" hakuna nchi inayonyooshwa kwa matamko yasiyo na tija, ndiyo inazidi kupinda kwa ugumu wa maisha.Nchi inakwenda mbele. discipline inakuwepo kati ya walionacho na wasiokuwanacho. Heshima inakuwepo. Hizo gharama unazolilia ni sheria ndo inafuatwa. mbunge au diwani akijiuzuru kuwepo na uchaguzi mwingine. shida nini? hii mihemuko ni shida sana. Sasa na yale mabilioni ya EPA na ESCROW huoni kuwa ni gharama tena pesa za walipa kodi? Muache atunyooshe bana.
Naam, hilo swali na wao linawahusu haswa. ni msumeno unakata kuwili. Lakini wao wametimiza wajibu wao bila kupepesa macho. wametutengenezea mazingira ya kujadili hayo mambo kwa uwazi na kwa upana. tujimwage tutoe maoni yetu bila woga.KWANZA NIKUPE LIKE
nimeshukuru kwasababu umekuja katika mlengo kwamba umesoma Ujumbe na unaweza kuuelewa. Jambo jingine ni kwamba unaelewa mazingira ambayo taifa linapitia. Je, Katika yote hayo na yanayoendelea kutokea, mababa hawa wa imani waendelee kukaa kimya? Au nao wataulizwa swali "Yupo wapi ndugu yako?"
ahahahhaa toa povu likuishe kabisa mkuu. lisipoisha utapata shinikizo la moyo......Hata nyumba za serikali ni gharama kubwa tu, watu wanapeana kama karanga, na wanadunda na nyie mnashangilia kama mazuzu. hata kujenga kiwanja cha ndege kikubwa kule Chato ni gharama kubwa sana, tena isiyo na sababu. EPA ilikuwa fedha zilizochotwa kugharimia uchaguzi kwa ajili ya CCM. za ESCROW walizochota wakubwa wala hatujui kinachoendelea. hapo JPM wala hatii neno, atasema "hataki kufukua makaburi" hakuna nchi inayonyooshwa kwa matamko yasiyo na tija, ndiyo inazidi kupinda kwa ugumu wa maisha.
Hiyo gharama ya Demokrasia ni kama mtu amefariki labda. mnahonga watu na kuiba kura halafu mnamdanganya nani?