WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Haya ni majibu tosha ya kanisa la Tanzania linasema nini kuhusu madai ya wananchi 26/4
 
Huu waraka ulitakiwa uwekwe katika jukwaa la siasa sio kufichwa huku general forums. Wanaojibu huu waraka kama kina mwakibinga mmewaweka kwenye Jukwaa la siasa huku waraka wenyewe mmeuficha huku? Acheni woga nyie JF
 
Tutawajibu majukwaani tena ikiwezekana mapema sana ukiwa bado unatrend ikitupasa kufanya hivo maana tulishasema hatupangiwi wala kujaribiwa.[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Aliuawa Mwangosi, mkakaa kimya ?

Kapotea Saanane, mko kimya ?

Azory ?

Watu wanaokotwa kwenye viroba Daily COCO BEACH mko kimya ?

Daudi wa Hanananif,

Aquiline kauawa kikatili

Hivi Tanzania tuna viongozi wa dini kweli aina ya YOHANA MBATIZAJI aliyemkemea HEROD waziwazi baada ya HEROD ( MFALME ) kuchukua mke wa nduguye ?

Tatizo ni nini kwa viongozi wa dini, HATUNA VIONGOZI WA DINI, NJAA, KUJIPENDEKEZA KULIKOPITILIZA, UOGA au nini ?

Wakikaa kimya taabu, wakisema tabuu!! Hebu jitahidi kujitambua wewe binafsi!!!! Ficha ujinga wako!!!!
 
WAANZE NA WEWE MNAFIKI MKUBWA!
MNAUANA WENYEWE KWA MAKAFARA KWA AJILI YA RUZUKU ALAFU UNATUSUMBUA KWA VISENTI UNAVYOLIPA ILI UONEKANE UMEANZISHA UZI. BLADIFUL, MPUMBAVU WEWE NENDA KATAFUTE KAZI UZEE UNAKUJA PAMBAF
Hili povu vipi inaonekana dawa imeingia vizuri.
 
The idea that religion and politics don't mix was invented by the Devil to keep Christians from running their own country. Jerry falware

Those who believe religion and politics aren't connected don't understand either. Alstein and mahatima Ghandi.

Kwa tafsri isiyo rasmi ni kuwa mawazo yanayo amini huwezi Kuchanganya dini na siasa ni mawazo yaliyo anzishwa na shetani kwa ajili ya kuwafanya waumini waikimbie nchi yao.

Nukuu ya pili,wale wote wanao dhani dini na siasa havifungamani huenda hawajitambui.

Msako wa maneno machafu na kejeli zinazo tolewa na wana harakati wenye mrengo wa kukimbia ukweli kwa kuipuzwa taarifa ya baraza LA maaskofu wa KKKT hakuifanyia dunia na nchi yetu kuto kujua kinacho endelea.

Siasa ya visasi,mfumuko wa matabaka ya kikanda,mikoa na uwiano wa kura za urais haziwezi kuiacha nchi yetu salama hata kidogo. Laiti waraka huu ungekuwa uzushi,tungeamini kanisa lina ajenda nyuma ya pazia.

Hali ya nchi ya usalama ni tete,Rais anajua,waziri wa mambo ya ndani anajua,makamanda wa vyombo vyetu vya dola wanajua ,mkurugenzi wa usalama wa taifa anajua hata wananchi na viongozi wa dini wanajua.

Taasisi ya dini ndicho chombo chenye kubeba na kusimamia maadili ya umma mzima,linapoona nchi ina kwenda kinyume bila kukemea ni sawa na kumruhusu shetani aliangamize taifa.

Unapotengeneza maneno ya ukali kuwakemea viongozi wa maadili eti wanaingilia siasa lazima tuhoji uelewa wako. Ikiwa mnaikataa dini kwa kupitisha maovu yenu kwa nini mnapo apishwa mnatumia vitabu vitakatifu vya Mungu,kwa nini mna waalika viongozi wa dini kuliombea taifa. Kwa mini yanapo tokea majanga makubwa ya kitaifa kama uhaba wa mvua,tetemeko la ardhi na. Mengineyo mna wakimbilia,lakini linapokuja suala la kukemea maovu mna taka kutenganisha dini na siasa?

Mahatima Ghandhi anasema"Those who say religion has nothing to do with politics do not know what religion is". Wale wote wanao sema dini si lolote kwenye siasa hawajui nini maana ya dini.

Ikiwa walinda maadili wana shambuliwa uadilifu wao na Mwakibinga kwa kuwa serikali imeanikwa peupe kuna haja sasa kama taifa kujitathimini kisawa sawa kama tuna kubaliana na mauaji holela ya raia wasio na hatia. Kuwashambulia maskofu ni kulishambulia kanisa na kulifundisha nini cha kusema kwa lengo la kuifurahisha serikali hata kama sifa hizo ni za kijinga.

Kuikosoa serikali na watawala wake hakuondoi sifa ya kuipenda nchi yetu,niliwahi kusema, hatumchuki Magufuli ati kwa kuwa ni Rais wa Tanzania,tuna kerwa na aina ya uongozi wake usio heshimu matakwa ya kikatiba inayoongozwa kwa sheria na kanuni,kuthibitisha hilo kuwa tuna mpenda,tunaitumia haki yetu kikatiba kuhoji na kukemea yale yanayo pingana na katiba,sheria na kanuni.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano si Mali ya chama kimoja,ni mali ya Watanzania wote bila kujali tofauti za kiitikadi,ikiwa mtapenda kusifiwa na kuombewa na viongozi hao hao wa dini,mkubali kupenda kukosolewa pia.

Ni jukumu la serikali kujitathimini na kuitafakari kwa umakini tamko la Pasaka lililo tolewa na Kanisa la KKKT,kwa kujitazama na kujisahihisha kuliko kutaka malumbano na makanisa. Kuwatisha maaskofu ni kulitisha kanisa,ni kupinga kazi ya kitumishi na ujumbe wa kitume ambao Sodoma na Gomora waliangamia kwa kukataa ujumbe wa kitume.

Kanisa limetekeleza wajibu wake,haijalishi utawafurahisha watawala au utawakera. Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni mwiko kuchanganya siasa na dini.
Naunga mkono hoja.
Kwa vile kazi ya dini zote ni kuwatayarisha tuu waumini wao kufika mbinguni, kwao hapa duniani ni safari tuu, hivyo dini zote, zifanye kazi moja tuu ya kumhubiri Mungu tuu na wasichanganye mambo ya siasa.

Hata zile shule na vyuo vya dini, vifundishe tuu injili na torati.
Na yale mashirika ya misaada ya kidini, yatoe misaada ya kueneza tuu Biblia.
Hata zile hospitali za dini, wagonjwa wakifika, wasiwatibu, bali wawaharakishe kwenda mbinguni.

Na akitokea mwanasiasa kuwaomba viongozi wa dini wamuombee, then viongozi wa dini wamuombee kweli ili mapenzi ya Bwana yatimizwe juu yake, akaikamilishe safari, maana kidini, hapa duniani tuko tuu safarini.
P.
 
Nadhani wana haki pia kuhakikisha waumini wao wanatii mamlaka za ' kikaisali'.
 
Halafu hukawii kuruka kimanga kwamba watu hawakuelewi humu. Kuteka, kutesa, kuua, kupoteza Watanzania kudharau katiba, bunge, mahakama, sharia za nchi na Watanzania ni zaidi ya siasa haya ni mambo ambayo kama yanaheshimiwa yanaongeza mshikamano katika nchi yoyote ile. Hivyo acha kutaka viongozi wa dini wakae kimya huku vitendo vya kutisha nchini dhidi ya raia na Viongozi wa upinazani vikiendelea kukithiri nchini kila kukicha.

Naunga mkono hoja.
P.
 
Maaskofu na mashehe kazi yao ni kukemea uovu, uovu unaofanywa na watu binafsi au serikali kikiwa ni kikundi cha watu kilichojikusanya kwa nadharia ya kisiasa. Ni wajibu wao kukemea, na wanaokemewa ni watu na si vitu. TUSIJITOE AKILI
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni mwiko kuchanganya siasa na dini.
Lakini sio mwiko wana dini kuombea wana siasa kusifia wana siasa kuchangiwa na wana siasa "a state with out religion it's like a vessel with out compass" Napoleon Bonaparte
 
......lakini kuchanganya siasa na udhalimu, dhuluma, utekaji, utesaji na uuaji wa raia wasio na hatia ni sawa sawa siyo? Akili za wapi hizi?????

Ni mwiko kuchanganya siasa na dini.
 
Back
Top Bottom