Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Kuanzia Leo nimemdharau Tundu Lisu,na yeye anashindwa kutumia akili yake kuona mazuri ya waraka,nimekumbuka maneno ya mwanasheria mkuu wa serikali alimwambia Tundu Lisu"atumie kichwa kufikilia na sio kufuga nywele
 
I like it
 
Kitila Mkumbo, nadhani Usalama wa Taifa ni kulinda maslahi mapana ya nchi. Au inaruhusu upuuzwe?
 
Last edited by a moderator:

Poleni magamba mmepigwa daflani
 
kama kweli barua hii ilitoka kwao basi, adhabu walioipata walistahili kwa maana wangechelewa ingekuwa dhahama kubwa zaidi
 
Kwangu mimi katika misingi huru, ni mara chache kwa mamlaka kutoa uamuzi kama huu bila kuridhika na ushahidi. Na kimsingi kujitetea ni utaratibu wa kawaida ili kuweka kumbukumbu vizuri. Kinachoniuma hapa ni kuwa watu walioaminiwa na kuwa mfano wa kuigwa wako tayari kupotosha ukweli kwa mahitaji binafsi. Ni hapa mshangao wangu unaanzia!
 
Huyo mmoja ameshaandika barua ya kujiuzulu. Huu ni wakati wa kurudisha umoja wetu ktk chama.
Mungu mkubwa aisee, vinginevyo tulikuwa tunaizika Chadema hivi hivi.

Muizike Mara ngapi....hamna uwezo wa kufikiri...mmebakia Na ushabiki uso tija.....Nadhani atakayefuata baada ya zitto ni lissu....hatoki kwa wenye chama....
 
Jamani labda huu waraka sio wenyewe.

Kama ni wenyewe kuna nini cha ajabu hapa kwenye siasa za vyama na demokrasia? Bila mikakati huwezi kupata hata ubalozi.
Tatizo la waraka ni kuwa walioandika walikuwa na uwezo wa kutoa
maoni kwenye vikao badala yake,wakakaa na kuandika waraka
kiongozi mzuri ni yule anayezungumza na kukosoa kwa uwazi,siyo
kutumia njia za uaini.
Kama kiongozi ataongoza kwa majungu yanayoitwa nyaraka
mwanachama wa kawaida asiyeingia kwenye vikao atafanya nini?
Waraka umetaja viongozi wa kwanza walioongoza vizuri kwa maono ya mwandikaji,
je kama hawa waliokuja baadaye wamekosea,mwandishi aliwaona hao viongozi wa kwanza na kuwaomba wawakutanishe ili kunusuru taasisi? kama hakufanya hivyo badala yake akaamini nguvu zake hicho ndicho kinaitwa
usaliti,na usipodhibitiwa mapema madhara yake ni makubwa sana.
 
Zitto alibugi,nashindwa kumsoma..kama mtendaji mkuu (Dr Slaa) alikuwa dhaifu katika kubuni mbinu za kiutendaji na yeye kama msaidizi wake kwanini asingemsaidia mpaka aanze kuandaa huu waraka.
Kweli jamaa mroho wa madaraka.
 
Chadema imeshakufa, thats all. Kwenye uchaguzi kunakuwa na kambi, kwann chadema ni dhambi kuwa na kambi na ni dhambi kutofautiana kimawazo na mtizamo?

Wewe unaongea nini mjinga mkubwa? Unaropoka tu mpaka mapovu yanakutoka bila kujua unaongea nini gamba mkubwa! Akili zako ni kama za huyu hapa:
View attachment 122878
 
Wapendwa nimeusoma waraka huu na umenisikitisha sana. Ninajiuliza hivi SIASA ZA TANZANIA zinaelekea wapi....???
Hivi tutaweza kujenga INSTITUTIONS IMARA za KISIASA; KIJAMII; na KIUTAMADUNI kwa misingi ya SIASA CHAFU za chuki,fitina,udini,ukabila,ukanda......na zaidi sana UNAFIKI;UZINDAKI namna hii....???

That is very unfair,ukiona hata WASOMI TUNAOWATEGEMEA katika kukuza Demokrasia na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla wanaweza kuingia katika MCHEZO MCHAFU namna hii,ujue Taifa hilo sasa linaelekea KABURINI.
Maana zilivyo Siasa za Nchi(chafu)-ndivyo ilivyo Serikali yake(chafu);na kama Serikali yake(chafu)-ndivyo walivyo wanainchi wake(wamechafuka hata bila wao kupenda)
Watanzania kama kweli tunataka maendeleo angalau ya uchumi wa kati (Singaporean Tigers Economy) ni lazima TUBADILIKE KIMTAZAMO na KIFIKRA kwa maana ya KUJITAMBUA maana kwa hali hii ni dhahiri kuwa tumeshindwa KUJITAMBUA.

Hatuwezi ku-misuse funds kiasi kikubwa namna hii (kodi za walala hoi)kwa SIASA CHAFU namna hii halafu tukategemea Maendeleo tuliyoyakusudia.....never,never,ever.

Kama wasomi wanaweza kudiriki kufanya madudu kama haya,je,hao wasio wasomi watafanya nini....??? Yaani Tanzania UZALENDO kwisha kabisa,SHAME ON US....!!!
Nachelea kusema....TUBADILIKE ili hatimaye TUJITAMBUE.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika Dola, na lengo la mwanasiasa yeyote mahiri ni kushika hatamu za uongozi ndani ya chama chake tena kwa maslahi ya wananchi. Waraka huu sioni tatizo lolote kwani wanachama wamegundua wanakopelekwa na viongozi wa taasisi yao na wao ni wazalendo na mahiri katika siasa na hivyo wanatafuta mikakati ya kuongoza chama kwa maslahi ya chama na wananchi kwa ujumla. Lakini kwa kuwa ilibainika si busara kwa hatua iliochukuliwa na viongozi wa taasisi, wangetumia mbinu nyingine nao kuzima mikakati yao kuliko hii ya kuwavua uongozi na kuumbuana mbele ya sisi tullioamini kuwa sasa taasisi hii ndio mpinzani mkuu wa taasisi tawala. Kwa kufanya hivi wamenifanya niamini kuwa kwlei taasisi hii ni ya UKANDA, UDINI, UKABILA,UNDUGU, USHEMEJI, na UKWE. mtaishia kuwa mafisadi ktk taasisi yenu na wala hamtashika Dola katu kwani si wazalendo hata kidogo na watanzania wa leo si wale wa jana. ndio maana huwa najiuliza, ruzuku yote hiyo lakini bado mnapanga ofisi ya makao makuu tena nyumba ambayo ni sawa na servant quarters.
 

Mkuu nimekukubali, hata mimi sioni tatizo la waraka huo. Tundu Lissu rafiki umenidisapoint kabisa tukikutana nitakueleza. Kwa siasa hizi sioni mbadala wa CCM ni heli shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua. Nimesikitishwa sana na chadema nilikipenda sana.
 
Dah.. that long plan...... its whow Wise Man think....keep it up MM. M1.M2, M3 very intrested watch uuuu 2015
 
cdm inatufia mikononi cmon! sioni tatizo kwenye waraka huu
 
Hawa wapuuzi walitaka jifanya waandishi wa spy movie?Wakati wana fikra za hadith za sungura na ndizi vichwani.

Zitto alishajisahau akajiona kuwa master planner..na Mkumbo km kibaraka wake badala ya mwalimu wake...sasa atakwenda vipi fundisha wanafunzi wake jinsi ya kushindwa?
 
Men!!!
I read waraka wote apo juu, nadhani tha analysis ni sahihi, and we have ever advice you pple on those matters. Ila nadhani this shows the maturity thou na ujinga nadani ya chama. Kuongoza taasisi kama hii kuanahitaji wasomi na wenye vipaji vya uongozi either walozaliwa navyo au walosomea.

Most of the issues discussed zianfahamika na wanachama na wananchi walowapigia kura, ila to highlight some point, Kiongozi wa upinzani kwenye mjengo...n hakuna kitu, hana hoja, bado ata wapinzani mmegawanyikaaaa...nadhani hiyo inaonyesha udhaifu ndan ya CDM,,,

Mnahitaji muijenge taasisi yenu ionekane iko na nguvu na uwezo wa kuchukua dola, ila kwa mwenendo wenu,....next election mtarudi kama CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

You should note: Ange ya mtu doesnt matter in leading...what matters ni uwezo, either kielimu au ule wakuzaliwa na wa kuchambua mabo...yahusuyo nchi....achen upotofu wa kulalamika,,,tuu

Mimi ntawaunga mkono vijana wakishika hatamu ya hiyo taasisi.
Asanteni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…