kwanza na-declare interest yangu. mimi ni mmoja wa wengi wetu ambao ni "chama-less" tuliojichokea na ukiritimba wa CCM, na hivyo tumejikuta tukiitegemea sana Chadema kama ndiye mbadala.
pia nikiri kabisa kuwa mimi binafsi siuoni kabisa mkono wa CCM kwenye waraka (or rather mpango) huu. it looks to me like a document that has been worked out by a genetically pure Chadema germ.
hata hivyo ninaelewa na kukubaliana na ukweli kwamba jambo lolote, hata likiwa ni zuri kwa kiasi gani, likifanywa kwa kificho lazima litapelekea mtikisiko kwa community husika.
hiki ndicho kilichotokea kwa Chadema.....i.e watuhumiwa wenye nia njema kabisa na taasisi yao wamefanya mambo clandestinely lakini kwa bahati nzuri/mbaya wamekuja kugundulika.
kwa mtizamo wangu, huu waraka una maudhui mazuri sana lakini una mapungufu makubwa ya kimkakati (tactical deficiency) kwa waandaji wake. waandaji hao wanaonekana kuelewa sana walichotaka kukifanya lakini hawakuwa smart...they goofed it big time (and this am particularly addressing to my good friend Dr Mkumbo, going forward).
nikirudi kwa uongozi wa Chadema, mtizamo wangu ni kuwa maamuzi yao dhidi ya watuhumiwa yamekuwa equally poor or worse. huwezi kuchukua maamuzi waliyochukua Chadema with general elections beckoning only 2 years away halafu utegemee eti kushinda uchaguzi huo. itakuwa ni vigumu sana au pengine impossible kabisa. hii inatukatisha tamaa sana - tena sana tu - sisi tunaowategemea.
kuna positives nyingi kwenye waraka huu ambazo uongozi wa Chadema ungeweza kuzichota na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kukipeleka chama mbele. daima tukumbuke kuwa, kwa mfano, kwenye football match spectators huwa wanayaona vizuri zaidi makosa ya wachezaji walioko ndani ya pitch kuliko wachezaji wenyewe wanaocheza. hawa watuhumiwa ni kama spectators na ninyi viongozi ndiyo wachezaji - you should (or rather you could) have used approach mbadala anuai za kuwawajibisha watuhumiwa bila ya ku-create drama hii tunaishuhudia leo.