Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Bei ya mafuta imeshuka? Mnatutoa kujadili issues zinazogusa maisha ya watanzania, mnataka tupoteze muda kujadili sinema zenu humu. We are smart.
 
Leo hii MM 1 2 na 3 wako CCM!!! Alafu kuna watu walikuwa wanawatetea enzi zile kuwa sio mapandikizi ya CCM!!! Imagine waraka wao ungefanikiwa then kitila angekuwa katibu mkuu na mwigamba ateuliwe msaidizi wake alafu leo hii wangekuwa wameenda CCM kumuunga mkono magu hivi CHADEMA si ingefia hapo!!!

Licha ya madhaifu lukuki ya mbowe ila kwa hili bado namheshimu sana mpaka leo
 
Ina maana CHADEMA hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza hicho chama isipokuwa Mbowe tu? Ifikie wakati hiyo demokrasia wanayoihubiri, waiishi!
Hahaha Chadema wana katiba yao,katiba ndio inayoongoza vipi wamchague mwenyekiti wao,Unataka kunambia Tanzania hakuna Chama chengine kinachoweza kuongoza,mbona zaidi ya miaka 50 sasa Tanzania inaongozwa na chama cha CCM,Kwasababu Katiba ya Tanzania inaruhusu
Ifikie wakati hiyo demokrasia tunayoihubiri, tuihisi 😉
 
Wewe endelea kulalama lakini mizizi ya CCM ndani ya Chadema imekatwa ingawaje bado mmoja lakini huyo naye atajulikana muda si mrefu. Na kazi yote hii ilikuwa inafanyika kwa kutumia bajeti ya pesa za walipa kodi zilizokuwa zinatumwa ujerumani na ikulu na baadae kumrudia Zitto. No wonder Wassira alikuwa anatamba kwamba CDM itakufa kabla ya 2015. Wakajipange upya.

Tiba
halafu usajili uliofanyika baadae sasa ukawa ni pure members from ccm
 
Hahaha Chadema wana katiba yao,katiba ndio inayoongoza vipi wamchague mwenyekiti wao,Unataka kunambia Tanzania hakuna Chama chengine kinachoweza kuongoza,mbona zaidi ya miaka 50 sasa Tanzania inaongozwa na chama cha CCM,Kwasababu Katiba ya Tanzania inaruhusu
Ifikie wakati hiyo demokrasia tunayoihubiri, tuihisi 😉
Vyama vyote vinaweka wagombea.
Hivi kwenye uwenyekiti Mbowe anaruhusu agombee na mwingine?
 
Hao WENGI ndio watumie njia ya kidemokrasia (KURA) kuiondoa CCM madarakani, kinyume cha hapo ni BLA BLAH za DADA wa UGHAIBUNI!
 
Hivi CCM itaruhusu chama chengine kitawale Tanzania
Kwa nini unauliza hivo Mkuu?
Ni kwa sababu CCM ilisimamisha wagombea wawili wa urais 2015?
Au kwa kuwa CCM walimnunua Mbowe na CHADEMA yote na kutuletea mgombea wao wa pili kwetu?
 
Hahaha Chadema wana katiba yao,katiba ndio inayoongoza vipi wamchague mwenyekiti wao,Unataka kunambia Tanzania hakuna Chama chengine kinachoweza kuongoza,mbona zaidi ya miaka 50 sasa Tanzania inaongozwa na chama cha CCM,Kwasababu Katiba ya Tanzania inaruhusu
Ifikie wakati hiyo demokrasia tunayoihubiri, tuihisi 😉
Kwahiyo katiba ya chadema hairuhusu wanachama wengine kugombea nafasi ya uenyekiti isipokuwa mwenyekiti aliyeko madarakani tu?

Ccm inashinda baada ya kushindana na vyama pinzani. Kitu ambacho hatukioni kwenye chaguzi za nafasi ya mwenyekiti katika vyama pinzani
 
Demokrasia ni wengi wape kwanini husemi ifike wakati CCM nayo ipishe chama kingine.
Kwenye chaguzi vyama vyote hupewa nafasi ya kugombea na kwa bahati nzuri au mbaya CCM ndio hupata ridhaa ya wananchi. Ni vyema hata kwenye chaguzi za vyama wanachama wapewe nafasi ya kuamua nani awaongoze na sio mtu mmoja kukaa madarakani miaka nenda rudi. Ndio maana upinzani Tanzania ni jina tu
 
Kwahiyo katiba ya chadema hairuhusu wanachama wengine kugombea nafasi ya uenyekiti isipokuwa mwenyekiti aliyeko madarakani tu?

Ccm inashinda baada ya kushindana na vyama pinzani. Kitu ambacho hatukioni kwenye chaguzi za nafasi ya mwenyekiti katika vyama pinzani
Kama katiba yao inasema hivyo poa tu,wewe inakuuma nini?
 
Kwa nini unauliza hivo Mkuu?
Ni kwa sababu CCM ilisimamisha wagombea wawili wa urais 2015?
Au kwa kuwa CCM walimnunua Mbowe na CHADEMA yote na kutuletea mgombea wao wa pili kwetu?
Dunia waliyaona yaliyotokea 2015,idadi za watu walihudhuri mikutano ya kampeni za CCM na za kampeni za Chadema zilioneka,..CCM haijashinda ule uchaguzi,na ndio maana mpaka hii leo utawala wa CCM haujiamini.,CCM inaweka misengwe kibao katika vyama vya upinzani hii yote ni ishara tosha kuwa utawala huu haujiamini

Sasa tusubiri 2020,naona ndio itakuwa mwisho wa CCM,..
 
Imenibidi niusome huu Waraka. Hapo kwenye pesa za chama haijulikani zinatumikaje. Ndo maana hata jengo la chama wameshindwa kujenga.
 
Hii ni hisani kubwa Zitto kawafanyia Chadema.
 
Back
Top Bottom