Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Duh sina hakika kama nitapata mgao wa Noah imekula kwangu
 
Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida

Hakuna waliposema wamekubali mgao wa faida 50/50.

Jifunzeni maana ya maneno rahisi ya Kiingereza cha Chairman Thornton.

"In future we will form a 50/50 partnership..." maana yake kila mtu ana kampuni yake tunagawana faida, hasara na gharama za uendeshaji.

Haimaanishi yeye aendeshe kampuni wewe umekalia kitako unasubiri faida ya 50% plus 16%. Yani wewe upate 66%, umemzidi mwenye kampuni! Kuamini uongo kama huo you have to be psychotic.
 
Mlidanganya watanzani kuwa kwenye mchanga tumeibiwa sh trion 108,tra wakasema kwenye kodi tumeibiwa trion 484,rubbish
Kumbe ni uongo wa mchana kweupe
 
Kwani tumeshinda jamani
Noah Zipo tutapata Kama akuna tukaushe Kama mpira yani tumefungwa halafu tunajipongeza bila aibu
 
Kwanza ni vizuri tukampongeza Mkuu wa Nchi kwa kuthubutu kuwatingisha hao jamaa mpaka wakatoa hivyo vijisenti.
Ni pesa ambazo zitaweza kuweka nskshi kwenye bajeti yetu.
Fedha hizo zikiingizwa kwenye miradi ya maji zinaweza kuleta mabadiliko chanya kwa wakati huu.

Ni kweli ni fedha kidogo ukilinganisha na tulichoambiwa kwenye riport.

Ni sawa na kumsifia mwanafunzi kuwa anauwezo wa kufaulu mtihani kwa 98 halafu matokeo yake apate 0.2% .
Any way ni fedha zimeingia kwenye nchi yetu kutoka nje.

Nadhani cha kujivunia hasa sio hizo fedha bali makubaliano yaliyofanyika.
Mana hata kama wangeuza na kutupa mgao wetub kwa kipindi chote tulichozuia mzigo pale bandarini bado tungepata mgao wetu kama kawaida.
Ni jambo zuri kufikia makubaliano ya 50/50.

Jambo nililoona hapo ni uzalendo wa wale wanakamati na wajumbe wa tume zote kwani ile rushwa ya bil. 300 waliyotaka kuhongwa waliamua ipelekwe serikalini.

Yani fedha hizo hao wazungu walikua wanazitumia kuhonga watu na kuishia mifukoni mwa watu lakini sasa wameihonga nchi yetu kwa kile walichokiita kuaminiana na kusameheana kwa kutushikisha kitu kidogo ,dola mil 300.
Sio haba kwa kweli.
Nawapongeza wajumbe wa kamati kwa kuwaambia hao jamaa wa Barrick kuwa waongeze kidogo ile rushwa ya mil. 300b ili inufaishe umma badala ya wachache.

Ila itakua ni jambo la ajabu kuendelea kuwaita wezi hao jamaa kwani kama tuliona kuwa wanaiba tungewapeleka mahakamani kwani ndio maana hada yankuwekeana mikataba kisheria .
Kwa madai yale yenye ushahidi wa wazi kama tulivyoonyeshwa na tume zote basi tungelipwa fedha nyingi zaidi kupitia hukumu ya mahakama ukilinganisha na hii nyongeza ya mil. 400 toka ile mil. 300 ya rushwa tulioambiwa kuwa walitaka kuitoa.

Na pia hao jamaa wa Barick kama wangeona kuwa wao sio wezi wangeenda mahakamani ili wadai fidia ya kimahakama badala ya wao kutoa fedha na kutulipa au kukimbilia kutaka kutoa rushwa ya mil. 300; iliyokataliwa.
Hii ndio win win situation. 50/50.
Ni jambo zuri sana kwa kweli.

Jambo lingine linaweza pia kuwa hao jamaa wameingiwa na hofu baada ya kuona serikali imetumia ubabe kuzuia mzigo na pia baada ya kuona ofisi za mawakili zinalipuliwa kwa mabomu wakaona mpango wowote wa kisheria unaweza usifaulu.

All in all hiyo ndiyo 50/ 50, wao wameshinda na sisi tumeshinda.
Hakuna aliyeshindwa kwenye lile sakata la makinikia.
Nampongeza Mkuu wa nchi kwa kutoa droo kwenye mechi na timu hii ngumu iliyokuwa inatufunga kila mechi.

Angalizo tu ni kuwa tuangalie wasije wakajinoa na kuja kivingine.

Ni vyema tukatambua kuwa utajiri mkubwa duniani sio ulioko ardhini bali ulioko ndani ya mwili na nafsi ya binadamu yaani "MAARIFA"
Tukiwa na maarifa hata mchanga wa baharini na mawe ni utajiri. Na tukiwa hatuna maarifa dhahabu tutaichezea bao.
Maarifa ndiyo yanayoifanya Japani iwe kama ilivyo na sio rasilimali zilizoko kwenye ardhi yao.
Tuwekeze kwenye maarifa na teknolojia na sio kubweteka kwa kujidanganya kuwa kuna siku tutalingana na Denmark kwa sababu ya mawe yanayomeremeta ardhini.
Elimu
Elimu
Elimu.
 
 


Yaani tunalipwa asilimia 0.14462809917355371900826446280992 ya tulichopania kupata
((billion 700)/(trillion 484))x100=0.14462809917355371900826446280992%
 
Atazileta Lissu kipitia MIGA
 
Wale wa MIGA povu linawatoka naskia mgonjwa huko BP iko juu hahaaaaaa Mwambieni tumeshinda tumeshashinda
 
Mkuu kama unakunywa soda, chukua novida take away , buku 1000 iyo hapo lipia.

Nimeshangazw na hawa Lumumba kukurupukia hii mambo akati bado wakubwa wa Acacia hawaja approve..

Yaani ninaona wameamua kuachia hii ishu kwa sasa ili kuzima na kuwasahaulisha watu kuhusu furaha yao kwa lissu kupata nafuu.

Waliona hawapo midomoni kwa watu sasa wameileta hii makusudi kubaki ktk kiki
 
Huyo jamaa apone tu...ila ni pumba kabisa empty...hamna kitu
 
Nauliza kwa pesa hizo Noa zetu tulizoahidiwa kupewa kila mmoja wetu tutazipata au? Kama hatuzipati basi wakurupukaji wapo wengi. Noa Yangu nilichagua nyeusi.
 
Ila ilisemekana hawata lipa hata senti tano na watatupeleka mahakamani watushinde asubuh na mapema vip hilo mbona hamlizungumzii jamen hapo cjaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…