Mwengeso, we were to be paid 400 trillions, sasa wamelipa? Ndilo swali langu au wamekubali kulipa? si unasikia kuwa hata zile US$ 300 million hawatalipa mpaka hapo...... au hawatalipa kabisa.Kama alivyodadavua Yajub, wenye upeo mdogo wataishia kuona mwisho wa pua zao. SIYO WEWE RETIRED Mkuu, una heshima kubwa humu jamvini
Hiyo fedha inayolipwa $300m, hata kama haitalipwa, haina mabadiliko makubwa kuliko makubaliano ya kurejea mikataba kulingana na marekebisho ya sheria ya madini, 2017.
Mbali na hilo la mikataba, kwamba barrick imekubali shughuli zote za mauzo kufanyika nchini na Watanzania kuwa wajumbe wa bodi ya kuendesha kampuni mpya ya kusimamia uchimbaji wa dhahabu migodi inayomilikiwa na Barrick, ni ushindi mkubwa sana.
Isitoshe, kuna makubaliano ya kujenga kinu cha kuchakatua madini na Barrick watasalimisha, kwa Serikali, aina ya madini yote yasiyo kwenye mkataba. Ukirejea ripoti ya pili, hayo madini pia yana thamani kuliko.
Hitimisho, makubaliano hayo yamefungua mlango wa kudhibiti rasmali zetu wenyewe.
HATUSHITAKIWI kama upinzani ulivyotegemea. Kama siyo aibu kwao ni nini!!
Mkuu, MMENUNUA MBEREKO MTOTO HAJAZALIWA
Mwengeso hayo yote mpaka barrick wakubali, bodi ikae ikubali au ikatae! ( Ni mwanzo mzuri lakini la kushangilia hivyo as if tayari ni washindi, sio sawa. Let us keep our fingers crossed?!