Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

kwani mlikuwa mnashindana na LISSU!Mungu wangu tunaitaji mapinduzi ya kifkra.Lissu ni mbunge tu wala si waziri sasa tumemshinda nini.Tusijiweke Low kiasi hicho jamani mwacheni Lissu apambane na hali yake.
 
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Pole sana msomi Lissu kwa kuumwa. Lakini sasa kwa taarifa za jana ni kuwa unapata nafuu na Mungu Mwenyezi awe nawe urejee.

Hata hivyo huku ulipotuacha ni umeshindwa vibaya. Wale uliosema watatushitaki na kuwalipa mabilioni sasa wao ndio wanatulipa sisi mabilioni.

Kile ulichosema kuwa ni makosa yetu ya mikataba na ulofa, wamekubali kuwa ni makosa yao na wako tayari kwa marekebisho ya "terms" vipengele vipya kwenye mikataba.

Hata zile kesi ndogondogo tulizokuwa nao katika mahakama "tribunal" mbalimbali sasa nazo wamekubali iundwe kamati ya kuzimaliza kwa mazungumzo.

Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida na Tz kuwa na wawakilishi kwenye bodi ya wakurugenzi na mengine mengi yenye kutia moyo. Sijui, lakin nadhan habari hizi sio njema sana kwako.

Msomi Lissu, siku nyingine ukiambiwa wako watu wana akili kuliko wewe uwe mwepesi tu kuelewa. Ukiambiwa wako watu wanaona maili 50 zaidi yako uelewe haraka.

Hatukatai, unaweza kuwa mzungumzaji mzuri lakin sio mwenye upeo. Upeo hupimwa kwa matokeo ya matendo. Na kwa matokeo haya twaweza tu kupima nani mwenye upeo kati ya wale uliowaita wa hovyo na wewe. Pia twaweza kujua wa hovyo ni nani sasa.

Nilikushangaa sana uliposema huoni kosa la Acacia. Watu wamedanganya uzito wa madini, wamedanganya sampuli walizobeba na ushahidi upo, msomi unasema huoni kosa !!!? , Looh.

Unajua vyema kuwa hawa jamaa wangekuwa upande salama kama ulivyopiga chapuo wasingefikia makubaliano kama haya. Wangeenda kwenye tribunal za kimataifa kama ulivyowasaidia kupendekeza na wangeshinda na tungelipa mabilioni kama ulivyokuwa umetabiri.

Ulikera sana hapa :

Makontena yakazuiwa, ukasema kimkataba ni yao na yamezuiwa kimakosa.

Ripoti ya kwanza ikasomwa,ukasema ripoti hiyo ni takataka"rubbish".

Ripoti ya pili ikasomwa, ukasema hamna jipya.

Akaja bosi wa Acacia Prof. John.L.Thompton akasema watalipa, ukasema hajasema kama watatulipa na hawawezi kutulipa.

Ulidhihirisha uadui na nia ovu na ndio maana ni halali leo kusema JAPO UNAUMWA LAKINI UMESHINDWA. Haikujulikana ulitaka nini hasa.

Msomi, hawa watu hawakuwa wasafi na hili kila Mtanzania aliliona isipokuwa wewe. Kwa matokeo haya sasa twaweza kujua nani ana maamuzi ya KUKURUPUKA na kuzungumza hovyo.

Tunakutakia afya njema lakini upunguze kidogo kuropoka msomi. Watu wako makini kuliko unavyofikiria.
Basi ungekuwa na akili timamu ungemshukuru Lissu sio kumlaumu

Yote yaliyofanyiwa kazi ni mambo ya Tundu Lissu ambayo ni maswala ya sheria na mikataba

Umeona kuna pendekezo lotote la tume mbili za uchunguzi iliyofanyiwa kazi?

Acacia wakawa wanadeclare madini aina tatu, tume zikasema ziko aina takribani kumi na tano.. leta feedback yake hapo(acacia watabaki na Gold, Copper Na silver hayo mengine ya kwetu), je unamtambo wa kuyachenjua hayo mengine na yanafaida gani?

Wakasema wanadeclare amount ndogo ya gold(2-4Kg) tume ikasema kuna zaidi ya gold(28-47Kg), je, umesikia jana wamezungumzia?

Wakasema wasisafirshe mchanga mpaka walipe kila kitu. jana kwa tamko la rais watasafirisha kwa kukubali kulipa 0.157% ya hela tunayowadai

hebu tupe kipengelee kwenye mapendekezo ya tume iliyofanyiwa kazi kwa mafanikio makubwa

Nasema si haba kuna gain tunapata tofauti na nyuma
 
Muache mwenzio apate nafuu. Mgetaka kubishana naye Risasi za nini......?
 
Kama walijua Angeshindwa kwanini walimtandika Risasi?
Walijua yeye ni kitisho cha kuwaumbua.




Nchi hii kuna watu wa ajabu sana... Kwa Mwananchi wa kawaida ambae anajua kushangilia tu yeye atapokea taarifa kama ilivyo na kushangilia.., ni ngumu sana kudanganya watu wote kwa wakati wote.. Wengi wameingia mkenge.. Naona propaganda kwamba "WANAUME wamekubali kutulipa"..,

.., kuweka kumbukumbu sawa,
USD300M sio deni..., ni kulinda uaminifu.. ni kama bonus.., hakuna deni lolote walilokubali kwa mujibu wa maelezo ya pande zote mbili..., bonus haiwezi kuwa deni., "Kama malipo ta kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo"


Kwa hiyo BARRICK watalipa bilioni 600 (USD300M) na sio ile trilioni 450 ambayo tulielezwa na kuaminishwa awali kwamba ndio tunawadai!? Tunashangilia tena.. Sisi watu wa maajabu na hatujawahi kuacha kujishangaza.., Zile kelele za trilioni 400 ambazo tulielezwa tunawadai BARRICK zimeyeyuka ghafla..

Bado BARRICK wanakwenda kuchenjua wenyewe. Wanakwenda kupeleka wenyewe sokoni, kwenye masoko ya kimataifa Belgium, RSA, Britain. Baadae Mauzo baada ya safari yote ndio analeta mezani faida ya Mauzo GOT na BARRICK wagawane 50/50 percent . Hii unaona iko sawa tu!?

Ukimsikiliza Profesa Kabudi na Dr. John Thornton, kuna eneo Kabudi anasema WAMEKUBALI lakini Thornton anazungumzia subject to APPROVAL ya wakubwa zake huko kuliko na head quarter zao ambazo huenda zikahamia Mwanza kwa mujibu wa makubaliano..

..., ukimsikiliza Dr John Thornton anasema "proposal zote lazima zipitishwe na London Board of Directors na Acacia ..." Tunafanya propaganda ambazo hazina faida hata.L kidogo....., changa la macho ....., kutoka madai ya trilioni 426 hadi bilioni 700 bado unashangilia tu.

My prudence would have been to hold this press conference until everything has been approved by their shareholders and the board in London.., to avoid any potential embarrassment in future.

Usishangae BARRICK/ACACIA wakagoma..., au wakaja na counter proposal.. maana hata kama BARRICK ni majority share holder wa ACACIA.., minority wakigoma itabidi kutumia kwenye usuluhishi au kuwalipa minority kama watakubali kununuliwa. its bit tricky.. lets remain sober for now.. Nasubiri press release ya BARRICK/ACACIA..
Tunapambana na rushwa wakati huohuo tunapokea rushwa, halafu tunashangilia watu eeeeeee
 
Basi ungekuwa na akili timamu ungemshukuru Lissu sio kumlaumu

Yote yaliyofanyiwa kazi ni mambo ya Tundu Lissu ambayo ni maswala ya sheria na mikataba

Umeona kuna pendekezo lotote la tume mbili za uchunguzi iliyofanyiwa kazi?

Acacia wakawa wanadeclare madini aina tatu, tume zikasema ziko aina takribani kumi na tano.. leta feedback yake hapo(acacia watabaki na Gold, Copper Na silver hayo mengine ya kwetu), je unamtambo wa kuyachenjua hayo mengine na yanafaida gani?

Wakasema wanadeclare amount ndogo ya gold(2-4Kg) tume ikasema kuna zaidi ya gold(28-47Kg), je, umesikia jana wamezungumzia?

Wakasema wasisafirshe mchanga mpaka walipe kila kitu. jana kwa tamko la rais watasafirisha kwa kukubali kulipa 0.157% ya hela tunayowadai

hebu tupe kipengelee kwenye mapendekezo ya tume iliyofanyiwa kazi kwa mafanikio makubwa

Nasema si haba kuna gain tunapata tofauti na nyuma
Mkuu pole sana, naona unafanana na bondia aliyepigwa ngumi nzito akaanguka chini sasa anajaribu kujikusanya aweze kuamka ili aendelee na pambano huku mwamuzi akiendelea kumhesabia.

Hayo yote uliyoyaandika yapo kwenye karatasi zile zilizosainiwa mbele ya JPM. Uliyoyasema ni sehemu ya michakato ya mikataba. Msipende kujidharau sana mnapowaona hawa watu weupe, wana udhaifu mwingi tu kama sisi watu weusi.
 
Mkuu hapo tumepewa rushwa in the name of Good faith
Hauwezi ukapewa ahadi ya 0.15% ya unachokidai ukajisifu mshindi . Hiyo ni bakshishi a.k.a rushwa ili unyamaze, uache makelele ya kuwaharibia kwenye soko la hisa duniani.
Another naïve doubting Thomas....They are so many in number...others will show up soon, but abadan, they will not steal this show!
 
Ahhhhhhh!!!!!,ni kweli alikosea,na hatujajua ya mbele lakini siasa mbaya sana;
SINA CHAMA,MIMI NI MTANZANIA;
Ndugu zangu watanzania hasa wenye mapenzi mema na nchi hii, naomba kwa dhati kabisa kutumia fursa hii adhimu kwa ajili ya kuiombea msamaha ile BINGWA MROPOKAJI kwa aibu kubwa ya kiwango cha lami aliyoipata baada ya Acacia kushindwa kuishtaki serikali MIGA kama ile BINGWA MROPOKAJI ilivyowaaminisha watanzania. Hii ni aibu kubwa kwake, kwa familia yake, ndugu zake, jamaa zake, marafiki zake na hata kwa chama chake.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuunga mkono upuuzi anbao Lissu alitaka kutuletea kama taifa, naamink hata ndugu zake wanajitutumia tu kwa sababu ndugu yao

Mkuu, umenongea jambo la maana sana na mwenye macho asome na kuelewa.
 
Mkuu pole sana, naona unafanana na bondia aliyepigwa ngumi nzito akaanguka chini sasa anajaribu kujikusanya aweze kuamka ili aendelee na pambano huku mwamuzi akiendelea kumhesabia.

Hayo yote uliyoyaandika yapo kwenye karatasi zile zilizosainiwa mbele ya JPM. Uliyoyasema ni sehemu ya michakato ya mikataba. Msipende kujidharau sana mnapowaona hawa watu weupe, wana udhaifu mwingi tu kama sisi watu weusi.

Mkuu, kula tano kwanza.
 
Back
Top Bottom