Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Hapa namuona Membe kama mtu fulani ambaye anakaribia kupata uchizi.Kama huogopi mbona unalialia kupitia kwa Askofu ?

Mtu ambaye haogopi huwa hasemi mimi siogopi,matendo yake yanaongea.Wewe ni mwoga sana na ndiyo maana unaanza kutaja makosa yakoU liyoyafanya mwenyewe bila kuulizwa.

JAMANI MAGUFULI ANATISHA.

Kumbuka huyo jpm naye husema haogopi na kujiita jiwe kwelikweli. Je unasemaje kuhusu hilo?
 
Kwanza nimsifu Askofu kwa kusimama kwenye ukweli kwa ujasiri. Watu wa Mungu hawastahili kuwa waoga maana aliyetuumba hakutuumba hivyo. Alitupatia roho ya ujasiri ipendayo kweli. Ibilisi ametutia uoga na unafiki sisi na viongozi wetu wa dini, serikali na makundi mbalimbali.

Namshukuru Mungu pia kwa kumjalia Bernard roho ya ujasiri. Ujasiri wa kuunena ukweli. Kwa hali ya sasa ambapo wengi wamepigwa ganzi na sindano ya uoga, inahitaji msaada wa Mungu kuunena ukweli. Wengi tumebakia kuwa majasiri wa mtandaoni. Hata huku pia tumeyaficha majina yetu kwa uoga. Naomba siku moja Roho wa Mungu atujilie, sote tuamue kuyaweka majina yetu dhahiri, ikiwezekana na namba zetu na mahali tuishipo. Ili kama kuna shetani aliyewahi kuushinda ukweli atukamate wote tunaounena ukweli (ukiacha wanaotusi).

Kwa upande mwingine hekima iwaingie watawala ili watambue hawabebi chochote katika miili yao zaidi ya kile Mungu aliwaumba nacho:

1) hawatuzidi wengine katika ubinadamu

2) hawakupewa akili kutuzidi sisi sote

3) hawakupewa roho nyingi zaidi ya wengine

4) wamepewa madaraka yanayoweza kuwafanya wabarikiwe au walaanike kutokana na kiburi cha mamlaka au unyenyekevu utokanao na hekima ya Mungu

Wakipata hekima, watayafanya haya:

1) watakuwa watumishi wa vitendo badala ya kuwa watawala wanafiki wanaonena tofauti na wanayotenda

2) watakubali hekima za wazee wetu kuwa ukubwa ni jalala, watayapokea mema na mabaya dhidi yao lakini wao watatenda mema hata dhidi ya wale wawaneneao mabaya kwa husda

3) watatmbua kuwa hawakuletwa duniani wala hawakupewa mamlaka kwaajili ya kutesa, kuteka, kupoteza watu au kuua bali walistahili kusimama katika hekima ya utawala yaani kuwa kama jabali lenye kutoa kivuli kwenye jangwa (kukiwa na joto kali la jua, watu wajikinge nalo), na pia wawe kama kijito kitiririshacho maji katika ardhi kame (watu wakifuate hicho kijito ili kupata tulizo la kiu)

4) hawatahangaika na kisasi wala kuwakomoa watu kwa kuwatengenezea kesi za utakatishaji fedha au uhujumu uchumi pasipo haki wala hawatapora mali za watu kwa sababu tu wana mamlaka

5) hawatawakomoa wapinzani wao kwa kuwafilisi bali watakuwa wanyenyekevu na wenye hamu kuwasikiliza wapinzani wao ili wayasikie mapungufu yao

6) hawatafanya teuzi za upendeleo wala utumbuaji wa kisasi bali kila jambo kwa kweli ya Mungu

7) Hawatajificha katika jina la Mungu katika kuuficha uovu wao bali wataenda mbele za Mungu kumwomba awajalie roho ya kutenda haki, kuondoa chuki na upendeleo, kuyaishi wanayoyatamka na kuongoza kwa kweli yake na wala siyo kwa hadaa.

8) hawatatenda kwaajili ya kutafuta sifa, wala hawatataka kuwatweza watawala na watendaji waliotangulia bali kwa unyenyekevu watasawazisha ambapo hapakuwa sawasawa maana na wao ya kwao yatasawazishwa na wengine

9) watatamani kusikia mapungufu yao kuliko kusifiwa kwa unafiki

10) watatambua kuwa ukiwa mtawala, wengi wanafiki watakuimbia sifa usiku na mchana, lakini ukiwa na hekima utawasikiliza zaidi wenye mawazo tofauti kuliko wanaokusifia tu.

Mugabe kaondoka duniani kama anavyoondoka msukuma mkokoteni,mbeba zege,mfagiaji kaacha vyote ndumba,walinzi,mahekalu,Mali,Pesa,ukuu nk kwwenda kusimama kwwenye hukumu
 
Mambo ya chikwete Raisi fisadi .Mke wa raisi kahaba na Mtoto anauza ngada hatuyataki sasa hivi ni dhama za Magufuli Raisi mzarendo Mke wa raisi mchamungu mtoto msomi
Kama Membe ni fisadi Mbona mungufuli wenu hamgusi Membe? Mguseni anuke.
 
Jamaa akipewa mic itakuwa balaa!! Maneno yake machache yatajadiliwa na kudadavuliwa kila nukta na neno linasimama kama lilivyoandikwa. Aiseee!!
ingekuwepo spika ya bashite bado ina nguvu leo leo ungesikia porojo zake
 
SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE. Huu msimamo sio mchezo, mwanaume kaonesha uanaume wake
Hiyo ni nyongeza ya bora ufe umesimama kuliko kuishi huku umepiga magoti.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kama ni mtanange basi praise team wanakula za uso...mi sio mshabiki wa team yoyote.
 
Afadhali leo shetani kaambiwa ukweli, maana amesababisha ubaya, mauaji, utekaji, unanyasaji, uvunjaji sheria na katiba, maonezi, dhuluma, uporaji wa mali na wake za watu, nchi imejaa uharibifu wa kila namna.
 
Kwa mtindo wa utendaji wa utawala huu wa awamu ya tano, tusije shangaa "wakamzushia" huyo Askofu na Membe wake, kuwa wote siyo raia wa nchi hii!
Mmoja anaweza fanywa raia wa Malawi na mwingine wa Msumbiji.
 
Yeye anasema "Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."
Waraka huu utaiwezesha chadema kwenda ikulu moja kwa moja hapo 2020
 
"Tusipotokea wachache wa kuyasema na kuyakemea mabaya Baba Askofu, nchi hii itaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona!"

"Lakini leo sisi tunaonekana ni maadui wa Serikali na hakuna jema lililofanywa na awamu zilizopita"

"Pamoja na makosa yote yaliyofanywa na Awamu zilizopita, Serikali na Viongozi hao walijitahidi kuheshimu Katiba, Uhuru, Sheria na Haki za binadamu. Huo ndiyo msingi wa Uongozi Bora Duniani".

Kama haya kweli ni maneno ya Membe, basi amemaliza! Need we say more?
Ishu ni kayasemea wapi?

Hata kama ni yake mbona anayasema kwa kificho? Kwanini asitokee moja kwa moja kwenye vipasa sauti?

Sasa huko alikoandika kamwambia nani?
 
“Niguse ninuke”

"Baba Askofu Emmaus Mwamakula!

Tumsifu Yesu Kristo!

Napenda nikushukuru sana kwa ujumbe mzito na wenye tija katika Taifa. Nikiri kwamba nami nimekuwa nakufuatilia sana kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao umekuwa ukiutoa kwenye mitandao. Endelea kufanya hivyo! Nikiri pia kuwa nimekuwa nafuatiliwa, nazushiwa shutuma za hatari kama vile za uhaini, usaliti, ufisadi, uhujumu, kufanya kampeni ya Urais nk.

Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE.

Ninakushukuru sana kwa ushauri na maneno ya busara uliyonipatia. Tusipotokea wachache wa kuyasema na kuyakemea mabaya Baba Askofu, nchi hii itaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona! Serikali ya Awamu ya tano imepewa ridhaa ya Uongozi na sisi wenyewe. Lakini leo sisi tunaonekana ni maadui wa Serikali na hakuna jema lililofanywa na awamu zilizopita. Ninawasikitikia washauri wanafiki na waoga wanaokaa kimya au kumshauri vibaya Rais wetu. Wanafiki wanaomlinganisha Rais wetu na Yesu na wanaomwomba Mungu amshukuru Rais wetu kwa yote anayoyafanya. Pamoja na makosa yote yaliyofanywa na Awamu zilizopita, Serikali na Viongozi hao walijitahidi kuheshimu Katiba, Uhuru, Sheria na Haki za binadamu. Huo ndiyo msingi wa Uongozi Bora Duniani.

Baba Askofu, usichoke kutushauri na kutupa moyo wa kuyatenda yale ambayo yatampendeza Mungu. Unifikishie salaam zangu kwa Maaskofu wote! Ubarikiwe sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandikile Mwamakula na tuzidi kuombeana.

Bernard K. Membe. Mstaafu!"

NB: Waraka huo hapo juu kutoka kwa Mheshimiwa Membe (pichani), umenifikia leo kupitia nami nimeona niuweke hapa hasa ikizingatiwa kuwa ujumbe wangu wa awali kwake niliuweka hapa pia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)
Ujumbe huu umeutoa wapi? Una mawasiliano ya karibu na Membe? Kama nindiyo basi, jaribu kumshauri kwamba kwa historis ya utumishi wake, siyo rahisi yeye, Membe kuwa ni mtu anayejitwisha mzigo wa kusema na kukosoa utawala ulioko madrakani. Hana sifa! Njia anayojaribu kupitia ni kama hiyo ya wengine waliojiita wanaharakati. Njia anayoshauri na kuitaja katiba, hakuna ilipotuletea mafanikio. Yeye mwenyewe alikuwa madrakani na hatukuona matokeo chanya ya nafasi yake.
 
Back
Top Bottom