Waraka wa Kanisa Katoliki na Nafasi ya Kanisa Tanzania, Tutarajie...!

Unasemaje kuhusu MOU ya kikatoloki iliyasainiwa na serikali eti wawe wanapewa kila mwezi 60bln , je haya ni ya kweli au ni uzushi tu?
 
Very well, narration
 

Itabid ninunue kitabu kwa bei ya dp world
 
Wanatuchanganya. Mohamed anasema pesa ya nauli kwenda UN wanachama wa TANU walichanga, huyu anasema kanisa lilidhamini; sijui tushike lipi!
Sikiliza vizuri hayo maelezo ni kweli wanachama walichangia lakini kanisa lilitoa nusu ya nauli kwahiyo uko sawa pia
 
Unasemaje kuhusu MOU ya kikatoloki iliyasainiwa na serikali eti wawe wanapewa kila mwezi 60bln , je haya ni ya kweli au ni uzushi tu?
Kuna chumvi nyingi katika mambo haya! Serikali itakuwaje na upendeleo kwa Wakristo? Ila kuna wapiga debe wa mambo haya na kusababisha watu wema kupotoka.
 
Kwa ujumla umeeleza vozuri na ukweli mtupu. Kwa ujumla mpango wa Tanganyika kupata uhuru haukuwa iwe tarehe 9 mwezi wa December. Tarehe iliyopangwa awali iliahirishwa ili uhuru wa Tanganyika upatikane usiku wa tarehe 8 Desemba, iendane na sikuku ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili.

Ni kweli pia ni kanisa Katoliki ndiyo lililipia tiketi ya ndege kwenda UN.

Ni kweli pia Mwalimu Nyerere alipofukuzwa kazi, familia yake ilipelekwa Tosamaganga, na ilihudumiwa kila kitu na masista Wakonsolata.
 
1. Ufafanuzi wako na ule wa Mzee Mohamed Said
Mohamed unatofautiana sana. Yeye anasema wazee wetu wa Pwani ndio waliomsadia Mwalimu Nyerere kwenda UN kudai uhuru. Na alipikiwa chakula mchana ule na Bibi Titi. Wewe unasema alisaidiwa na Shirika la Masista la Marknoll.
2. Wewe unasema zilikuwa harakati za Jesuits (Catholics) vs Anglicans kutaka kuongoza nchi huru ya Tanganyika. Yeye anasema zilikuwa harakati za Wazee wetu wa Pwani na Nyerere alikaribishwa tu.
3. Wewe umeweka harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika katika Muktadha wa Kikristo, Yeye anaweka katika muktadha wa Upwani na Uislam.
4. Wewe unaona harakati mpya za mapambano ya Ukatoliki Tanzania vs Serikali zenye kuegemea uislam na Ulutheri. Yeye, kwa bandiko lake la kumnukuu Shehe wa Mkoa Mwanza anaonesha Ujio wa DPW kama sehemu ya harakati za kuwainua waislam Tanzania.

Lini mtakutana kwa mjadala wa wazi, maongezi ili kujaribu kutatua huu mfarakano wa kihitoria. KWANI AMA MMOJA WENU HAJUI VIZURI HISTORIA HII, AU WOTE, lkn haiwezekani wote mkawa mko sawa. Nasubiri hiyo siku
 
Mimi naamini kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote kwamba baada ya kupatikana uhuru, serikali ni lazima litii matakwa ya Kanisa Katoliki. Lakini ni jambo la kawaida, mtu akikufadhili, akikusaidia, utakuwa na heshima kwake, na hata akitoa ushauri, utaupa uzito.

Hata kule Zanzibar, ni Kanisa la Anglikana ndiyo liliwakomboa watumwa waliokuwa hatarini kusafiroshwa na Waarabu. Waliwanunua kama walivyofanya wanunuzi wengine wa watumwa, kisha wakanunua na ardhi toka kwa Sultani, kisha wakawakabidhi hiyo ardhi wale waliokuwa watumwa. Ma sehemu ile waliyokuwa wanafanyia mnada wa watumwa waliinunua na kujenga Kanisa ambalo lipo mpaka leo.

Hata hivyo, baada ya Waanglikana hao kuondoka, watumwa kutokana na sababu za kiuchumi, walislim ili wafaidike na nafua za kiuchumi walizokuwa wakizipata waislam, hasa walipokuwa wakienda kununua bidhaa kwenye maduka ya waarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…