Waraka wa Kanisa Katoliki na Nafasi ya Kanisa Tanzania, Tutarajie...!

Waraka wa Kanisa Katoliki na Nafasi ya Kanisa Tanzania, Tutarajie...!

Yericko Nyerere : Lowasa ni fisadi


Yericko Nyerere : Lowasa achaguliwe kuwa rais wa Tanzania
?? proof by contradiction haitoshelezi kila pahala. Logic itadai corollary kama base. Iko hivi, lwa vile UFISADI unalekea kuwa ni jadi kwenye tawala zetu hizi za jamhuri ya madizi, kuna fisadi ahueni kuliko wenzao katika nyakati flani. Mkuu, tuweke list ya mafisadi walokua wanachuana kipindi kile LOL, alafu tuambie kati ya yule alohamishia HAZINA kijijini kwao na EL yupi bora. Corollary hiyo
 
kanisa liliwapingaje wakolon wakati kanisa ni moja ya vitangulizi vya ukoloni?
Katoliki na Anglican na Lutheran hawaivi

Wakoloni waliotutawala ni wajerumani ambao walikuwa warutheli wao wao walikuwa wakiandaa waafrika warutheli kushika nchi baadaye wakakabidhiwa waingereza baada ya mjerumani kutolewa vita kuu ya dunia.Tukakabidhiwa kwa Waingereza wa Anglikana. Nao walikuwa na watu wao waliwaandaa kama Oscar Kambona mu Anglicana ambaye baada ya kuona mbinu zao zimeshindwa waingereza wakataka kumtumia apindue nchi kupitia jeshi lao la King African Rifles Jaribio lilliloshindwa.Kambona akatimukia Uingereza kwa waangkikana wenzie waliomtuma kupindua

Lakini katoliki wako vizuri .makundi yote hayakufua dafu wakakuta Nyerere huyo kaibuka

Catholics sio watu wa kubeza beza kienyeji tu Huandaa viongozi hata wawe waislamu uzuri hawabagui mtu wakiona anafaa wanaanza processs ya kumuandaa kwa njia wanaxojua wenyewe
 
Amejipambanua kuwa yeye ni wa timu fulani ! Kwahiyo wale wa timu ile fulani nyingine sidhani kama wataukubali uchambuzi wake !! Nchi hii kwa sasa kila kitu ni kama Simba na Yanga !!
Mpaka baadhi ya wachambuzi wamo 😅😅🙏🙏
🤣🤣🤣🤣
M/Mungu atatusaidia tutavuka salama, bado tuwamoja mno!
 
Huwezi kupata mwanga wowote kk utoka kwake kwa sababu story zake zote zipo twisted kuonyesha kuwa uhuru wa nchi hii walipiagania watu wa dini yake tuu hivyo yupo biased
Hapana, siyo kweli.

Mohamed Said kaandika historia Uhuru kama ilivyo.

Sema huamini tu kuwa makanisa hayakuunga mkono wapigania Uhuru.

Wewe si uandike uoneshe ya wazee wako? Mohamed Said kaandika ya wazee wake.

Mjadala wa historia ya Mohamed Said ndiyo ulifanya mpaka mleta mada abambwe uongo wake wa kujifanya yeye "mtoto wa nyerere".

Aliumbuka sana.
 
Naomba nijuze kwanza je kuna uhusiano wowote wa wamisionari na wafanyabiashara Kama mawakala wakuu wa mwanzo kabisa wa ukoloni?

Ndugu mchambuzi Yericko?
 
Hapana, siyo kweli.

Mohamed Said kaandika historia Uhuru kama ilivyo.

Sema huamini tu kuwa makanisa hayakuunga mkono wapigania Uhuru.

Wewe si uandike uoneshe ya wazee wako? Mohamed Said kaandika ya wazee wake.

Mjadala wa historia ya Mohamed Said ndiyo ulifanya mpaka mleta mada abambwe uongo wake wa kujifanya yeye "mtoto wa nyerere".

Aliumbuka sana.
Mohamed Saidi ukweli hujitahidi sana kuandika historia ila yuko biased kuna kitu anachosahau .Kwenye uhuru wa Tanganyika na mivutano ya kidini ya nani ashike dola baaada ya mkoloni kuondoka kati ya waislamu, warutheli wa Anglikana na wakatoliki

Kila kundi lilipanga safu mwisho wa siku wakatoliki na Nyerere wakaibuka washindi

Ndio maana baada ya uhuru makundi mengine hayakuridhika sana akiwemo Bibi Titi Mohamed muislamu aliungana na muanglikana Oscar Kambona kutaka kupindua serikali ya Nyerere i na warutheli wa kilimanjaro chini ya Chief Mareale walienda umoja wa mataifa kupinga Tanganyika isipate uhuru. Kwa hasira

Dini wakati ule kila moja ilitumia mgongo wa dini yao kushika nchi.Wakavutana ndani huko wee Katoliki akaibuka mshindi

Mohamed Said yeye huandika kwa kuegemea tu upande wa uislamu tu !! Hayuko balanced Ile struggle ya nani ashike ilikuwa struggle ya kila dini kutaka mtu wao.ashike wa dini yao mkoloni Akiondoka
 
Mohamed Saidi ukweli hujitahidi sana kuandika historia ila yuko biased kuna kitu anachosahau .Kwenye uhuru wa Tanganyika na mivutano ya kidini ya nani ashike dola baaada ya mkoloni kuondoka kati ya waislamu, warutheli wa Anglikana na wakatoliki

Kila kundi lilipanga safu mwisho wa siku wakatoliki na Nyerere wakaibuka washindi

Ndio maana baada ya uhuru makundi mengine hayakuridhika sana akiwemo Bibi Titi Mohamed muislamu aliungana na muanglikana Oscar Kambona kutaka kupindua serikali ya Nyerere i na warutheli wa kilimanjaro chini ya Chief Mareale walienda umoja wa mataifa kupinga Tanganyika isipate uhuru. Kwa hasira

Dini wakati ule kila moja ilitumia mgongo wa dini yao kushika nchi.Wakavutana ndani huko wee Katoliki akaibuka mshindi

Mohamed Said yeye huandika kwa kuegemea tu upande wa uislamu tu !! Hayuko balanced Ile struggle ya nani ashike ilikuwa struggle ya kila dini kutaka mtu wao.ashike wa dini yao mkoloni Akiondoka
Tusubiri Mzee Mohamed Said atuwekee mambo sawa katika hili !!
 
Taasisi linapokuwa kubwa na mambo yanakuwa mengi. Watu billion 2 chini ya kiongozi mmoja na matawi dunia nzima. Waraka umepiga penyewe
Hio sio excuse kama tunaishi maisha aliyoishi Kristo na Mitume wake tutaongozwa na kweli,lakini kweli kama haipo kwa wanaosema ni viongozi wetu hapo tunapata mashaka.

Usishangae mtu atakiwi kuoa lakini huko mtaani anazini na wanawake hata 6 na ana watoto pia akifikiri anamficha Mungu. Kubwa kuzidi ni molestation ya vitoto vidogo.

Kanisa litoe boriti ndio lione kibanzi kwa wengine.
 
Nilikaa kimya kwa muda baada ya Waraka wa Kanisa Katoliki, nilifanya hivyo ili kuruhusu mitazamo ya wengine katika tafakuri za waraka huu. Kabla sijachambua Waraka huo, Kwanza nithibitishe kuwa NINAUNGA MKONO kwa 100% waraka huo. Na pia kabla sijachambua nimebini kupitia maoni ya watu mbali wengi hawafahamu Nafasi ya Kanisa Katoliki katika Uhuru wa Tanganyika na nafasi ya Kanisa katika Mwelekeo wa Nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo ninaomba LEO NISICHAMBUE WARAKA HUSIKA, Isipokuwa nichambue kwakueleza nafasi ya kanisa katika Tanzania ambapo kwa sehemu kubwa nilishaeleza katika kitabu cha Ujasusi.

Baada ya kulijua kanisa, makala ijayo nitachambua Waraka na tafsiri yake pana ikiwa Serikali itakomaza fuvu lake. Ifahamike wazi ni kanisa katoliki ndio wametoa tamko, Bado Waislamu (BAKWATA) hawajatoa tamko, Bado CCT (KKKT, Anglikana, nk) hawajatoa Tamko, Bado CPCT (Makanisa ya Kilokole) hawajatoa tamko. Matamko mengi mnayosikia yanayotolewa kupinga waraka wa Kanisa Katoliki ni vikundi vya wahuni tu wanaotumiwa na magenge ya kihalifu huko mitaani yenye lengo la kuiingiza serikali chakani kwania za kiasiasa au kiuchumi. Waraka wakufanana na Waraka wa Katoliki zinakuja zitasomwa kila kaya na kila familia msikitini na kanisani. Hakuna raslimali ya nchi itapotea.

Pengine ni kwa mara ya kwanza Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ndio kinaeleza uhusika kikamilifu wa Kanisa katoliki duniani katika uhuru wa Bara la Afrika na hasa Tanganyika chini ya shirika nguli la Ujasusi la Kanisa Katoliki. Utafiti wa kinyaraka na machipuzi ya nera kwa mambo anuawai, ndio yaliyonihakikishia kuhitimisha katika kitabu juu ya nafasi ya kanisa, Tunapoongelea Uhuru wa Tanganyika tunayo sababu na ni haki yetu kutambua na kuheshimu mchango wa kila mtu alivyoshiriki katika uhuru huo, haijalishi mapokeo ya makundi mengine katika nchi, Tusipoandika historia yetu, tusilaumu tukiandikiwa.

Hebu turejee kwenye Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo la kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.

Kanisa halikuwa nyuma na mwito wa dunia, Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na mashirika yake tanzu yakiongozwa na shirika la kijasusi la kanisa hilo liitwalo (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana).

Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Society, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao na kwa Tanganyika Fabian Society wao walikuwa wamemuandaa Chifu David Kidaha Makwaia huku Jeisuti ya Katoliki wakiwa wamemuandaa Julius Nyerere. Rejea kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps akieleza nguvu ya Vatican katika kudhibiti ulimwengu, anakazia katika harakati za ukombozi duniani hasa Afrika na nafasi ya kanisa chini ya Jeisuti.

Barani Afrika, Jesuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake Tanganyika, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima.

Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jengo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji kinagaubaga waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi).

Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingorwila Mkoani Morogoro.

Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati. Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo).

Mnamo tarehe 7, mwezi wa 7, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajesuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.

Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.

Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tarehe. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata, MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA......

Kwaundani zaidi, Soma KITABU cha Ujasusi kwa Ofa Maalumu.

Watu 5 @ mtu atapata Kitabu cha "UJASUSI" kwa 30,000/= Badala ya 80,000

Lpia kwa:

Tigo Pesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

Kwa Dar ni free delivery

Nje ya Dar nauli ni 8,000/=

View attachment 2726157
View attachment 2726158
View attachment 2726159
Chambua kilichoandikwa ndani ya waraka.
 
Back
Top Bottom