Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,926
- 6,430
Usingeusoma
Huu ni waraka wa Lisu kwa Chadema siyo kwa Watu wote!
Huu ni waraka wa Lisu kwa Chadema siyo kwa Watu wote!
Safari ya kushika dola ni ngumu sana.
Mi nimeamua kukaa pembeni na harakati za siasa.
Akishinda chadema ni sawa, akishinda ccm ni sawa na hata chama chochote.
Mkombozi wa maisha yangu ni mimi mwenyewe!!
Hiyo barua ilitakiwa ipitie kwa Shibuda kwanza ndio iende kwa Rais....... Vinginevyo aliyeandikiwa ni mwenyekiti wa CCM na Mbowe analielewa hilo vizuri!Ndio shida yenu, huyo ni Rais wa JMT hivyo eitha awe mwenyekiti wa ccm taifa au mumvue uenyekiti na kumpa ujumbe wa nyumba kumi lakini kama bado ni mwanachama wa ccm atabaki kuwa Rais.
Katiba ya Jamhuri haimtambui kama mwenyekiti wa lichama lenu bali Rais na Amiri jeshi mkuu, hivyo barua huyo haina mahusiano na uenyekiti wake wa ccm.
Huko shuleni mlienda kusomea ujinga?
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni waraka wa Lisu kwa Chadema siyo kwa Watu wote!
Unadhani hata huyo mawe alienda basi?.......aliionea huruma ruzuku ya akina halima!
Hahahaaaa......... ruzuku ijenge chama bhana!Sawa Mawe, tumekusikia
Hahahaaaa......... ruzuku ijenge chama bhana!
We mwenyewe ni mpumbavu pia, maana umeshindwa kuwabwekea CIA.Mpumbavu anabwekea ughaibuni,aje huku tubanane ,sio ang'ang'nie kujihifadhi sebuleni huko EU
Kwani kinachokuwasha nini ? Kama unaona haukuhusu wewe kausha tu.Huu ni waraka wa Lisu kwa Chadema siyo kwa Watu wote!
Nimekausha bwashee!Kwani kinachokuwasha nini ? Kama unaona haukuhusu wewe kausha tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mropokaji ni yule alisema watanzania wote waishio marekani warudi na wamarekani waishio Tanzania warudi kwao haraka...sasa unajiuliza hivi kichwani ana ubongo au matope!!Haki ya kuropoka ni tatizo la CHADEMA wala sio Watanzania, hakuna Mtz atakayeingia barabarani ili kutetea CDM ipate haki ya kuropoka, pambaneni na hali yenu.
Mkuu huamini kuwa Mola alitenda Miujiza Juu yake na Sasa Yu Hai? Bado anaendeleza mapambano kwenye ardhi ile ile ya Muumba wetu. Udongo ni ule ule mipaka ya Wanadamu tu ndiyo imetutenganisha.Uko wapi?.Rudi nyumbani!
mkuu tuminyimwa 500m na mabibiru🤒😭😭😭😭😭Uko wapi?.Rudi nyumbani!
baada ya kusoma waraka huu nimepata nguvu sana ! nitaendelea kuipigania Chadema katika maisha yote niliyosaliwa nayo hapa duniani .
Eee Mwenyezi Mungu nisaidie
Namba (ii) na herufi (f) inamhusu Joseph Selasini Mbunge wa Rombo. Huyu ni mbaya kuliko kirusi cha Corona virus.(1) Ni muhimu kutambua kwamba kipindi tunachopitia hakijawahi kuwepo katika historia ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini na hata wakati wa chama kimoja.
(2) Hatujawahi kuwa utawala wa kikatili wazi wazi kama huu. Hatujawahi kuwa na utawala usioheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu wazi wazi kama huu. Hatujawahi kuwa na utawala unaokandamiza haki za binadamu na haki za kisiasa kama huu.
(3) Hatujawahi kuwa na utawala uliojiapiza wazi wazi kuwa utaangamiza vyama vya upinzani kama huu. Kutekeleza kiapo chake hicho, baadhi ya mbinu anazotumia Magufuli na watu wake ni hizi:
(a) Kukandamiza wapinzani thru mauaji, kuwapiga na kuwaumiza, kuwafunga kwa kesi za kubambikiza;
(b) Kuwarubuni kwa rushwa ya fedha au ya madaraka wale wote wanaoweza kurubuniwa;
(c) Kuwashindisha kwa nguvu wagombea wa CCM katika chaguzi za marudio.
(4) Magufuli na watu wake wanafanya yote haya kwa sababu wanajua kwamba upinzani dhidi ya CCM ni mkubwa na una nguvu kuliko pengine tunavyojifahamu sisi wenyewe. Ya 2015 yamewatisha sana na hawako tayari kuyaona tena 2020. Ndio maana ya yote haya yanayoendelea.
(5) Tufanyeje???
(a) Tuyaelewe mazingira haya mapya ya kisiasa na sababu zake kama nilivyoelezea hapo juu;
(b) Tujielewe sisi wenyewe. Chama chetu kimekuwa kikubwa sana na hivyo kimeingiza watu wa kila aina:
(i) Wapo ambao wameingia kwenye chama kwa sababu wanaamini katika haja ya kulikomboa taifa letu na kujenga mfumo bora zaidi wa kikatiba na kiutawala. Hawa tutakuwa nao katika milima na mabonde tutakayopitia kwenye safari ya ukombozi;
(ii) Wapo walioingia ili kupata madaraka ya udiwani au ubunge au Urais au mengineyo. Wamegundua kwamba maisha ya upinzani ni magumu na ya hatari sana. Hawa sio wetu na hatutaweza kuwazuia kununuliwa au kuondoka kwa hiari yao wenyewe.
(iii) Wapo walioingia kwa sababu halali kabisa lakini kwa imani kwamba safari ya ukombozi itakuwa fupi na rahisi. Wamegundua katikati ya safari kwamba njia ya ukombozi ni ndefu na imejaa miba na mawe na kila aina ya ugumu.
Wapo watakaokimbia sio kwa sababu wamehongwa, bali kwa sababu ya ugumu wa safari. Na wapo watakaobaki na kuendelea na mapambano.
(iv) Wapo walioingia kwa sababu hawaoni njia nyingine yoyote ya kujikwamua na mfumo tawala uliopo. Hawa ni wetu vile vile through thick and thin, lakini tuhakikishe hawakatishwi tamaa na haya yanayoendelea.
(v) Wapo waliopandikizwa ili watuhujumu kwa ndani. Hawa nao sio wetu na hatuwezi kuwazuia kujiondoa au kununuliwa.
Tunachohitaji kufanya ni kuweka utaratibu bora zaidi wa kuchuja kila anayeingia kwenye chama chetu; na hasa kila anayetaka au anayepewa dhamana ya uongozi wa chama wa nafasi za kiserikali kama madiwani na wabunge.
(c) Tuhakikishe chama chetu kinaendelea kuwa salama. Tusije tukafanya jambo lolote litakalompa Magufuli na watu wake sababu ya kukipiga marufuku chama chetu.
Hii haina maana tusiendelee kupigania haki na demokrasia katika nchi yetu. Ina maana tu kwamba tusifanye yale ambayo Sheria na Katiba ya nchi kwa sasa imeyakataza.
Tufanye yale ambayo Sheria na Katiba zimeyaruhusu na ni mengi. Matope ya kukiuka Katiba na Sheria za nchi yetu yabakie kwa Magufuli na watu wake, yasihamishiwe kwetu.
(d) Tuwalinde viongozi na wanachama wetu dhidi ya maonevu wanayofanyiwa. Tuweke utaratibu wa kuwatetea wanapokamatwa na wanapofunguliwa mashtaka ya uongo. Utaratibu huu uwe wa nchi nzima na tuache kutegemea kila kitu kifanywe na Makao Makuu ya chama.
(e) Tuendelee kujitolea kufanya kazi za chama. Hatuna mjomba au shangazi wa kututatulia matatizo yetu bali sisi wenyewe. Tuache kunyoosha vidole vya lawama kwa viongozi wakati sisi wenyewe hatutimizi wajibu wetu.
(f) Tujifunze kuwa na nidhamu ndani na nje ya Chama. Tuna migogoro mingi ya bure kabisa; tuna vichuki na vijiwivu visivyokuwa na msingi. Tuna vitabia vibaya vya kufikiria kwamba kila kitu lazima kitolewe nje hadharani na kujadiliwa as if hakuna taratibu za kichama za kuyajadili na kuyatatua. Lazima tuwe na nidhamu.
(g) Tuache visingizio na tufanye kazi za chama kwa bidii na maarifa. Kuna mengi ambayo yanatufanya tushindwe chaguzi kwa sababu zetu wenyewe. Haya tuyatambue na kuyarekebisha, kabla hatujakabiliana na ya Magufuli na watu wake na ya kimfumo.
Mwisho, Magufuli na watu wake wanajua hawana jawabu la matatizo ya kimsingi ya nchi yetu na ya watu wetu.
Wanataka kutuharibu ili kusiwe na sauti mbadala itakayowaambia wananchi kwamba Magufuli ameshindwa.
Tutambue kwamba vita dhidi ya CHADEMA na vyama vya upinzani ni sehemu tu ya vita kubwa dhidi ya Watanzania.
CHADEMA iko mstari wa mbele wa vita hii. Tukishindwa sisi hakuna mwingine atakayeweza kusimama na kupigana na utawala huu.
Tuna wajibu mkubwa sana.
Mwataka mmalizie kwa sumu maana risasi imeshindikanaMwoga huyo kazi kuongelea Mitandaoni arudi Kama yeye kidume.Mwenzie Bob wine uganda anapambana ndani ya nchi