Waraka wa Tundu Lissu kwa wanamabadiliko na watanzania wote

Safari ya kushika dola ni ngumu sana.
Mi nimeamua kukaa pembeni na harakati za siasa.

Akishinda chadema ni sawa, akishinda ccm ni sawa na hata chama chochote.

Mkombozi wa maisha yangu ni mimi mwenyewe!!

Mkuu wewe ni General au Jenerali kwa jina kama lile la Ulimwengu?
General hawezi kuonyesha kukata tamaa na kukaa pembeni huku anasema mkombozi wa maisha yangu ni mimi mwenyewe.
Kwani ukombozi wanaopigania watu ni kuletewa daily bread na CCM au Chadema? Hapana.
Kinacho gombaniwa ni General Mangi afanye yake kwa Uhuru, sio utafute maisha yako lakini amaweza kuwepo jirani yako ana madaraka akaamua kukuweka ndani na huna la kufanya kisa huungi mkono chama chake nk.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo barua ilitakiwa ipitie kwa Shibuda kwanza ndio iende kwa Rais....... Vinginevyo aliyeandikiwa ni mwenyekiti wa CCM na Mbowe analielewa hilo vizuri!
 
Tujifunze kuwa na nidhamu ndani na nje ya Chama. Tuna migogoro mingi ya bure kabisa; tuna vichuki na vijiwivu visivyokuwa na msingi. Tuna vitabia vibaya vya kufikiria kwamba kila kitu lazima kitolewe nje hadharani na kujadiliwa as if hakuna taratibu za kichama za kuyajadili na kuyatatua. Lazima tuwe na nidhamu.

Hapo Lissu amejiingiza mkenge, kama anajua sio sawa kuanika kila kitu uwanjani, na ni lazime kuwe na nidhamu, mbona yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kutaka serekali za awamu ya 4 na 5 wafanye hivyo kwa kila kitu.

Hesabu za matumizi ya ruzuku na michango lazima iwe wazi na kujulikana kwa kila chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haki ya kuropoka ni tatizo la CHADEMA wala sio Watanzania, hakuna Mtz atakayeingia barabarani ili kutetea CDM ipate haki ya kuropoka, pambaneni na hali yenu.
Mropokaji ni yule alisema watanzania wote waishio marekani warudi na wamarekani waishio Tanzania warudi kwao haraka...sasa unajiuliza hivi kichwani ana ubongo au matope!!
 
Namba (ii) na herufi (f) inamhusu Joseph Selasini Mbunge wa Rombo. Huyu ni mbaya kuliko kirusi cha Corona virus.

Kwenye fedha anaweza kusafiri yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…