https://twitter.com/tmla_tanzania Login • Instagram
Mhe waziri mwenye dhamana ya afya ummymwalimu
pengine hata wewe unajiuliza kwa nini wataalamu wa maabara wanalalamika.
Kifupi, hakuna aliyeonekana kuyasemea haya, hata tuliowaita viongozi wa taaluma walikaa pembeni wakishuhudia chombo hiki kinazama.
Mheshimiwa Waziri, haya ni malalamiko kwa uchache.
1. HAKUNA USAWA KATIKA MGAWANYO WA AJIRA ZA AFYA NCHINI
Tangu mwaka 2021 mpaka mwka 2023, ajira kwa upande wa Kitengo cha
maabara zimekuwa zikitolewa kwa kiwango kidogo mno, shughuli za vipimo vya maabara zinafanywa na
kada nyingine ambazo hazina utaalamu wa kutosha hivyo kupelekea
wateja wengi kupewa majibu yasiyo sahihi.
AJIRA ZA OR- TAMISEMI MWAKA 2021
Astashahada walipewa nafasi 142 sawa na
Wenye Stashahada walipewa nafasi 10 (0.3%
Shahada hawakupewa nafasi hata moja Sawa na 0%
Jumla ajira zilikua 2726.
MWAKA 2022
Astashahada nafasi 152 sawa na 2.2%
Stashahada nafasi 197 sawa na 2.8%
Shahada walichaguliwa 35 tu Sawa na 0.5%
Jumla ajira zilikua 6873
MWAKA 2023
Astashahada nafasi 56 sawa na 1.05%
Stashahada nafasi 18 sawa na 0.33%
Shahada nafasi 13 sawa na 0.24%
Jumla ajira zilikua 5319
Mheshimiwa, asiseme mtu hitaji halipo, tumefanya tafiti na tumegundua vituo hivi havina wataalamu wa maabara hata mmoja, je nani anafanya vipimo?
Vituo hivi havina wataalamu wa maabara.
Bulela dispensary - GEITA
Didia Dispensary - SHINYANGA
Mavota dispensary - KAGERA
Mselekea dispensary - MOSHI
Ibologero dispensary - TABORA
Bukondo dispensary - MWANZA
Kemgesi dispensary - MARA
Kisa dispensary - RUKWA
Mawe dispensary - ARUSHA
Tewe dispensary - TANGA
Ligumbiro dispensary - NJOMBE
Chajo dispensary - KILIMANJARO
Kilimani dispensary - MANYARA
Chumo Dispensary - LINDI
Na hivi ni vichache tu, Sasa je, Hawa wananchi huduma wanapewa na nani?
2. MAFUNZO YA UPIMAJI KWA WATU WASIO WATAALAMU WA
MAABARA NCHINI (NON LABORATORY
TESTERS) YAFUTWE.
Sheria hii iliwekwa mwaka 2007 kwa sababu kulikua na upungufu, huu upungufu haupo tena, wataalamu wa kufanya kazi zao wapo, huu utaratibu UFUTWE.
3. USAWA WA UONGOZI KATIKA KADA YA AFYA.
Mheshimiwa, kuna nafasi mpaka zimekaririwa anatakiwa kukaa daktari au muuguzi, kwa nini?
Nafasi ambayo sio ya kutumia taaluma bali uwezo wa uongozi, kwa nini tunakua kama tunaamini waliosoma maabara hawawezi kuwa viongozi?
Nafasi ya facility incharge, nafasi ya DMO kwani hizi nafasi zinawataka madaktari watibu?
Tunaomba ziwe nafasi za wazi, ziruhusu mtaaluma yeyote wa kada ya afya aongoze.
Kada hii pia mheshimiwa watu wamesoma management na leadership na hizi nafasi zinahitaji uongozi ila sio nafasi za kutumia ujuzi wa taaluma zao.
4. IDARA ZILIZOPO NDANI YA MAABARA ZISIMAMIWE NA WATAALAMU WA MAABARA.
Mheshimiwa, nenda Muhimbili pale kitengo cha maabara madaktari ndio wasimamizi wa vitengo vya maabara, kwa nini?
Tunatambua utaratibu huu unatokana na hoja kwamba kipindi cha nyuma tulikua hatuna wasomi wengi wa kada hii, leo tunao mheshimiwa, tuna wasomi wa PHD maabara, acha wakae vitengo vyao.
Ni sawa na kusema leo mtaalamu wa maabara asimamie kitengo cha mama na mtoto kisa alijifunza kuhusu hedhi.
Haiwezekani. Tunaomba vitengo vyetu tuvihudumie wenyewe.
Hata uwepo wa ulazima wa mkurugenzi wa diagnosis wizarani kuwa daktari haitakiwi mheshimiwa, tupo, mtutumie.
5. SIFA ZA KUJIENDELEZA NA KOZI MBALIMBALI ZIRUDIWE UPYA.
Mpaka leo kuna kozi huwezi soma kama sio daktari licha ya kuwa ni kozi zinazomuhusu mtaalamu wa maabara moja kwa moja.
Mfano Histopathology na Cytopathology.
6. VIONGOZI WA TAALUMA HAWAENDANI NA KASI.
Mheshimiwa, kwanza haya yote yangefaa kusemwa na wao.
Leseni zinachelewa, utaratibu wa mitihani unachelewa, sasa kuna maswala ya CPD utaona nako hakutiliwi mkazo, kuna swala la gharama za matumizi ya vyeti vya wanataaluma katika kufungua vituo vya huduma za afya bado hazijakaa sawa
Mheshimiwa binafsi namjua mtu alifanya mitihani ya shule akafaulu, ikabidi alipie kufanya mtihani wa provisional licence ambayo anakaa nayo kwa mwaka mmoja kisha analipia kufanya mtihani mwingine wa full registration.
Sasa Mheshimiwa, hii ni sawa? Mfululizo wa mitihani yote hii ni kupima nini? Kama hatuviamini vyuo tuvifunge, chuo kimempika mtaalamu akaiva, kafanya mtihani wa chuo kafaulu, kafanya mtihani kwa leseni wa kwanza kafaulu, kwa nini baada ya provisional asipewe full registration bila mtihani?
Utaona kuna mengi sana ya kuyasemea ila viongozi wanajua na hawaoni kama wana nafasi ya kufanya hivyo.
Mhe ummymwalimu
tuna imani kubwa na wewe, tunaomba utusikilize, tunaomba uyapokee haya, hakuna huduma bora bila mihimili iliyosimama.
Tunahitaji muhimili wa maabara usimame, ukusaidie kuboresha huduma za afya nchi wananchi wapate huduma inayostahili.