Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona Juma Nature aliimba wimbo wa mtoto Idd?
Mimi ni mkatoliki, i dont know what ur talking aboutSalaam aleikum likud
Umesema wewe ni mshabike jd napia ni muisilaam
Ss nataka kukuswalika swali hili. Je ni halali au haraam kusikiliza muzik wwte
Nijibu nitaendelea kukuswalika kwa mujibu wa quraan na hadith
Wakatabahu
Great thinkers hawajadili ujinga kama huu wa kwako ulioandika chooni wakati ukijisaidia haja kubwa.
Ungeuchambia na kuuacha huu ujinga huko huko chooni ulipokuwa.
Of course, hakuna atakayedai ana hisa kwenye thread ya kijinga kama kama hii.
Ichukue kabisa rudi nayo kule kule chooni ulipokuwa.
Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watanzania ambao wana ji identify themselves kama mashabiki wako wakubwa. But kina kitu kimoja ambacho kwa maoni yangu ninaona hakipo sawa . Nacho ni kuhusu wmbo wako uitwao YAHAYA. Wimbo wako ni mzuri na unaelimisha jamii but kwa nini usingetumia jina tofauti na YAHAYA. Kwanini ninasema hivyo?
1. YAHAYA ni jina la kiislamu, na miongoni mwa majina ya kiislamu yenye maana kubwa kwa waislam.
2. Wewe ni mkristo wa madhehebu ya wasabato.
3. Hapa kwetu nchini Tanzania kuna vugu vugu la waislamu na wakristo. Waislamu wamekuwa makini sana kwa kila kitu kinacho fanywa na mtu yoyote yule mwenye jina la kikristo hususani pale maslahi ya dini ya kiislamu ama jina la kiislamu linapotajwa. Sihitaji kulizungumzia hili kwa kina kwa sababu naamini huwa unafuatilia taarifa mbalimbali za habari so am sure as hell unafahamu ni kitu gani kinaendelea kati ya wakristo na waislamu Tanzania wakati huu.
( KITU CHA MSINGI KUELEWA HAPA NI KWAMBA, KITU CHOCHOTE KILE KITAKACHO TAJWA NA MKRISTO DHIDI YA UISLAMU AMA MUISLAMU KWA NAMNA YOYOTE ILE KINAWEZA KUCHUKULIWA KAMA KASHFA DHIDI YA UISLAMU )
Hivyo basi wimbo wako wa YAHAYA ingawa una ujumbe mzuri, but unaweza kukuletea matatizo na waislamu wa Tanzania ambao wanaweza kuuchukulia kama kashfa dhidi yao. Maadui zako wanaweza kuitumia hiyo kama loop hole na ku dress beef lenu kulifanya lionekane kama beef kati yako waislamu.
MAPENDEKEZO: Nikiwa kama shabiki wako, ninakushauri ubadilishe haraka iwezekanavyo jina la wimbo YAHAYA na kutafuta jina lingine lolote lile. Katika kutafuta jina nakushauri utafute jina ambalo halihusiani na jina la dini yoyote kati ya ukristo na uislamu. Unaweza kutumia majina yanayo tumiwa na watu wa dini zote kama vile MAWAZO.
Ukibadilisha jina la wimbo wako, utajijengea heshima kubwa sana kwa mashabiki wako ambao ni waislamu na watachukulia hiyo kama heshima kwao.
Sina mengi ya kuongea zaidi ya hayo. Natumaini umenielewa.
NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 13 YA LADYJAYDEE.
Kaka hizo ni dalili za kutokujiamini,mimi sioni tatizo labda ungesema wenye majina ya yahaya ndo itakuwa tabu kwao,kwa sababu humo jide kamchora yahaya kama kijana mtanashati ambaye anaishi maisha ya kubangaiza na anajifanya mambo safi kumbe hana hela,anajifanya anaishi masaki kumbe kinondoni na nyumba anayoishi haijuilikani,naijua hiyo nyimbo haiko kama unavyoifikiria kaka,napingana na hisia zako kabisa ni potofu,unataka waislam waogopwe wamekuwa nani??,kumbuka jide hajazungumzia udini kamzungumzia YAHAYA..
- Siungi mkono ushauri wa mleta mada
- Siungi mkono "uhuru wa mawazo" unaouruhusu kuwaza alivyowaza mleta mada. Hakuna namna ubongo unaruhusiwa kuwaza hivyo. Hakuna. Nimesema hakuna.
Hivi dini ni kitu gani hiki kinachofanya watu wanachanganyikiwa hivi? Kwa namna dini inavyokuzwa hata Mungu inabidi awe muumini!! Dini inaogopwa kuliko Mungu mwenyewe!! Waafrika hao!!!
Dini dini, dini dini... mpwampwa..mpwampwa... kero bana!!
NB. Mleta mada usijipe moyo kwa kusema haya ni maoni yangu... maoni yako hayatakiwi kuwepo popote pale...iwe katika kichwa changu au chako.
Haya ni majina tu mkuu, huku kwetu tunatambua dini kwa majina yetu wakati wenzetu mpaka akutajie dini yake, TARIQ AZIZ aliekuwa waziri wa mambo ya nje wa Iraq ni Mkristo lakini check hilo jina lake ingekuwa huku tunapopima dini za watu kwa majina ingekuaje
Kwa iyo siku jambazi akiuwawa na wananchi, katika kumuuliza jina kabla ya mauti, akasema yeye ni Mwamed, je waislam wataenda kuwauwa pia wazazi wake kwa kuudhalilisha uislam?
Mleta uzi ni maandazi ya nyama temana nae. Bure kabisa,akawaambie basi misikitini waandamane,si vuguvugu hilo,usifanye waislam wote wehe na wenye uwezo mdogo wa kufikiri.
Kwenye dunia ya muziki shabiki anajua personal details zote za msanii nyimbo zake,umri,makazi,gari anazoendesha,mavazi n.k but msanii wala hakujui we shabiki. So consider urself ignored.au huu walaka wako uuimbe yani uutolee single may be anaweza akakusikia.
Akili ni nywele unapoteza nguvu na muda kuleta udini hapa looh.
Ukiwa una mawazo kwamba mke wako anatoka nje ya ndoa bila ushahidi,siku moja usiku akikuambia hajisikii kufanya mapenzi tu,labda sababu kachoka na kazi za mchana kutwa,utasema ametoka kufanya mapenzi na yule bwana umzaniaye! Naona ndio mawazo ya huyu mtoa mada. Hivi ni majina mangapi ya ki kristo na ki islam yametumika kwa mazuri au mabaya hapa Tanzania na hakuna mtu wa dini yeyote aliyeuliza!. Ha!