feitty
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 2,594
- 4,189
Yaani katika vitu sijawahi waza maishani ni ndoa yenye sherehe yaani kiujumla mimi sipendi sherehe. Nikienda kwenye sherehe najikaza tu kwasababu ni familia au jirani sio vizuri muda mwingine kujitenga. Mimi napenda ndoa isiyo na mbwembwe as long as nimemridhia niliye naye.
Pia huwa naona sherehe ni kutafuta stress plus usumbufu kwa familia especially wazazi na kwangu pia so sitaki hizo hekaheka mie. Kuna watu watakuja kusema labda huwa sio mtoaji ktk shughuli za watu wengine hivyo labda naogopa na yangu itadoda, familia yangu ni wachangiaji wazuri tu sema ndio hivyo, naona ni kausumbufu fulani kasiko na maana.
Kingine ile shughuli ya kukumbusha mtu achange siku zimeisha siiwezi kabisaa naona kama inakuwa kulazimishana sasa kwanini niteseke na kitu kisicho na ulazima kwangu.