Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Yaani katika vitu sijawahi waza maishani ni ndoa yenye sherehe yaani kiujumla mimi sipendi sherehe. Nikienda kwenye sherehe najikaza tu kwasababu ni familia au jirani sio vizuri muda mwingine kujitenga. Mimi napenda ndoa isiyo na mbwembwe as long as nimemridhia niliye naye.

Pia huwa naona sherehe ni kutafuta stress plus usumbufu kwa familia especially wazazi na kwangu pia so sitaki hizo hekaheka mie. Kuna watu watakuja kusema labda huwa sio mtoaji ktk shughuli za watu wengine hivyo labda naogopa na yangu itadoda, familia yangu ni wachangiaji wazuri tu sema ndio hivyo, naona ni kausumbufu fulani kasiko na maana.

Kingine ile shughuli ya kukumbusha mtu achange siku zimeisha siiwezi kabisaa naona kama inakuwa kulazimishana sasa kwanini niteseke na kitu kisicho na ulazima kwangu.
 
Ndoa yangu nimeona nianze na mambo ya msingi kama ukumbi, usafiri, kuandaa kamati na vinywaji na chakula. Ila mwenza sijapata ndio nawaza kuanza kutafuta.

Sauti ya mpenda sherehe akiwa anawaza (mabinti walio wengi)
 
Ndoa ... Kadiiri inavopungua gharama zake ndo jinsi uimara wake unavyoongezeka.
Huu ni ushuhuda wangu tu naweza pingwa pia.
 
Niko Tayari bila kupepesa macho, achague yeye sasa.. tukitoka kufunga ndoa twende kazini au twenzetu home tukapige game
@Chakorii Ni vile tu ulishawahiwa ningenyoosha huko dm
Ila kama vp tufanye mapinduzi..
 
Kama hali ya uchumi hairuhusu Kwanini niendelee kushupaza shingo yangu ngumu kwa kung’ang’ania sherehe.kwanza ni gharama sana.hiyo pesa si bora tuifanyie uwekezaji ambapo itaongeza kipato.

Wanandoa wengi sana huishi maisha ya stress baada ya kufanya harusi.

Ingewezekana kufunga ndoa na kuendelea kupiga kazi ingekuwa mzuka sana.
Na kutegemea mifuko ya watu Kama ndio pesa ya kuendeshea sherehe.
Kuna watu unakuta wamezalishana mpaka watoto 3 na bado wanataka sherehe.
Hivi hamkujiandaa?
Mpaka watoto wanafika 3?
 
Wengi wao uwezo hawana tunabaki kusumbuana na Michango!
Nope nilikuelewa dear. Nimeshangaa tu hiyo conclusion yao kwamba mtu sipopenda sherehe basi automatically anakuwa wife material. Lulu hajafanya sherehe ila kafanya kufuru kwenye mavazi yake, so na yeye ni wife material kisa hakufanya sherehe? Kwa kweli kama mtu anapenda sherehe na uwezo anao, afanye tu sherehe kwa raha zake.
 
Mimi bila sherehe kabisa 🤫 nawish iwe japo ndogo tu ya wazazi wetu pande zote, sisters and brothers etc, tutakiane heri na tuombeane hapo. Misosi simple tu hakuna vilevi basi imeisha.

Ila hata isipokuwepo si mbaya sana.muhimu ni furaha yangu na huyo babe hubby.
 
Mimi bila sherehe kabisa [emoji2958] nawish iwe japo ndogo tu ya wazazi wetu pande zote, sisters and brothers etc, tutakiane heri na tuombeane hapo. Misosi simple tu hakuna vilevi basi imeisha.

Ila hata isipokuwepo si mbaya sana.muhimu ni furaha yangu na huyo babe hubby.
Sijui tunakwama wapi kulikamilisha hili jambo la kheri. Mbona tunaendana kabisa Mom!!

Habari za asubuhi?
 
Chukua bodaboda, mshikaki wa aina bibi mbele bwana nyuma mpaka kanisani au bomani. Banda ya kufunga ndoa mwendo wa bodaboda mpaka nyumbani na kuwajulisha majirani. Ndoa tayari!
 
Hii kitu ni kweli
Nko na mwanamke wangu sealed kabisa msiulize nimejuaje.
Me na yeye wote ni ma introvert na tumekubaliana kuwa ndoa itafungwa ofisini kwa padri then home.
Ile masherehe mbele za watu wote twaona ni extra.

eh Mwnyezi Mungu nisaidie me na huyu binti [emoji1276][emoji1276][emoji1276][emoji179][emoji1276]
wote introverts?? ana miaka mingapi?
 
Mbona hapo sijaandika kitu kabisa, mimi mama magazeti teh . I had a simple function (ingawa wanyaki hata tukiwa watatu hakunaga shughuli ndogo), lakini nawaheshimu pia walioamua kuvunja akaunti zao kwa sababu ya sherehe, ni pesa zao so far na chaguo lao pia na furaha yao pia. Kwa nini niteseke?

Siku nikijisikia kufanya function yoyote kubwa, nafanya tu as long as sababu ninayo, nia ninayo na uwezo ninao pia.
Imeisha hiyooooooooh
 
Back
Top Bottom