Wasaidizi kufungua biashara ndani ya biashara kunaua biashara nyingi sana, kijana anadai mshahara kila mwezi kumbe anakuibia mamilioni

Wasaidizi kufungua biashara ndani ya biashara kunaua biashara nyingi sana, kijana anadai mshahara kila mwezi kumbe anakuibia mamilioni

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Siku hizi baadhi ya wasaidizi hawaji kazini kutafuta mshahara, wanakuja kujifunza mfumo then wanafungua biashara yao ndani ya biashara yako.

Unafungua baa kubwa, unaajiri manager unamlipa vizuri kabisa. Kumbe na yeye ana stock zake pembeni. Wateja wakija wanauziwa vinywaji vyake, stock yako inabaki inakula vumbi store huku ukiambiwa biashara imeshuka.

Unafungua duka la vyombo, wateja wanafika wanahitaji sahani 100, msaidizi anaziuza, hapo hapo anapiga simu kwa wasambazaji wamlete sahani 100 zinazofanana na zilizotoka, wewe unahisi hakuna kilichouzwa.

Unaweka CCTV dukani ukiamini umeimarisha usalama. msaidizi naye anafungua stoo yake ya siri. Wateja wanaambiwa mzigo upo stoo, wanaenda kumalizana nje ya mfumo wako kabisa huku wakidhani bado ni biashara yako.

Unafungua pharmacy, unaweka stock ya kutosha. Ukiondoka kidogo tu, mhudumu anamuita mtu wake anachukua dawa wholesale kwa bei ya chini anauza kupitia counter yako. Mwisho wa mwezi anakwambia biashara ni ngumu huku yeye ndio ana-grow fastest.

Unafungua salon ya kisasa, unaweka CCTV na mazingira safi. Wasusi wanaanza kujenga ukaribu na wateja, kubadilishana namba, hapo sasa wanaanza bookings za pembeni. Wateja wanaambiwa leo kuna foleni au njoo home service. Polepole salon inabaki na viti, wao wanaondoka na customers.

Restaurant nayo same story. Wapishi wanaanza kuuza sahani zao kimya kimya kupitia jiko lile lile, ukiweka cctv wanakula vichwa kwenye delivery, wanawapelekewa wateja vyakula vyao. Ukiangalia stock ya unga, mchele na viungo vinaonekana sawa, ila cashflow haisomeki.

Siku hizi biashara nyingi hazifi kwa kukosa wateja, zinakufa kwa kuibiwa ndani kwa ndani
 
Unampa kazi kijana kwenye hardware yako na yeye anaunda hardware yake vichochoroni huko, huku duka lako analigeuza stoo yake ya kujichotea bidhaa za bure kwenda kwake.

Ngumu sana vijana kuaminika ktk biashara, tamaa+haraka ya maisha inaendelea kuangamiza ndoto za vijana wapumbavu.

2026 hakikisha hurudii makosa
 
Baada ya kufanya mikazi migumu kwa muda mrefu. Unaona hii mikazi inaniumiza, nachoka sana.

Unaamua kudunduliza mtaji kutoka kwenye kipato cha mikazi migumu ili uanze kufanya biashara uachane na mikazi migumu.

Unaona kwamba kwasababu umepigika sana kwenye mikazi migumu, basi umwajiri kijana anayesifika kwa uaminifu ili wewe uwe unapumzika kufidia ulivyokuwa unapigika.

Siku zinakatika na biashara yako inakufa. Kijana amekuibia na mtaji umekata. Hapo itabidi uanze upya tena kufanya mikazi migumu.

Vijana wa kazi wanarudisha nyuma sana jitihada za watu.
 
Mimi ni mwalimu pia nina playstation kubwa, nikiwa shule naifunga nafungua saa 9 nikirud shule kufundisha, bora nikose hela za asubuh lakn upumbavu wa kumnufaisha mtu sinaga, na nakunja hadi 25K kwa siku, siku za weekend hadi 40+k nakunja
 
Mimi ni mwalimu pia nina playstation kubwa, nikiwa shule naifunga nafungua saa 9 nikirud shule kufundisha, bora nikose hela za asubuh lakn upumbavu wa kumnufaisha mtu sinaga, na nakunja hadi 25K kwa siku, siku za weekend hadi 40+k nakunja
Play station kama muuza bangi mda wowote polisi wanatimba hasa siku za shule.
 
Kabisa.wakianza kuajiriwa wakongo,wazimbabwe,wakenya na wengineo watu wanaanza kusema watanzania hatupendani kumbe matendo hayaridhishi.
Kuna biashara moja hivi nataka nifungue. Nasubiri kwanza huu ukata wa january upite. Mpaka sasa hivi changamoto ni hapo kwenye kupata msaidizi. So far nafikiria kuwacheki washkaji zangu wa mbeya wanitafutie kijana wa kimalawi. Vijana wa bongo najua nitakula hasara tu
 
Umefungua Baa yako kubwa tu, umemweka meneja au msaidizi na unamlipa mshahaa alioridhia lakini na yeye anaanza kuja na makreti yake, wateja wakija wanauziwa vinywaji vyake, vyako vinakuanya vumbi tu.

Unafungua duka la hardware wayeja wanafika wanahitaji mifuko 100, msaidizi anaiuza na anapiga simu kwa wasambazaji walete mifuko 100 iliyotoka, wewe unahisi hakuna kilichouzwa.

Una duka umefunga kamera CCTV, msaidizi wako nae anafungua kistoo chake cha kutunzia mzigo wake, wateja wakitaka bidhaa anawaambia mzigo upo stoo, wanaenda kumalizana sehemu tofauti kabisa, wateja wanadhani ni stoo yako.

Duka la dawa umemuajiri kijana auze dawa, unaleta mzigo dukani ila ukiondoka tu na yeye anamtuma mtu wake aende kumnunulia mzigo duka la jumla, kijana anakwambia biashara inasua ila usikate tamaa kumbe yeye biashara ipo safi kwake, baada ya muda kapiga pesa yake ya kutosha anaondoka atafungua duka lake atakwambia aliuza nyumba ya urithi

Umefungua saluni yako umeweka wasusi na umefunga, Wateja wakipiga simu wanaombwa waende maeneo mengine au kufatwa majumbani

Umejikamua umefungua restaurant yako, wapishi wanaanza kuuza sahani zao 5 na zako 4, wanakwambia biashara ngumu na ukikagua unga, mchele, viungo kila kitu kipo sawa
Hilo la kufunga cctv afu mdaidizi kuwaambia wateja mzigo upo stoo nahisi limenikuta, nimejifunza kitu hapa....nimekuwa nikicheki kwenye cctv camera yangu kuna baadhi ya wateja wanakuja wanakaa muda mrefu wanazungza na msaidizi then baada ya muda kuna kijana (nisiyemfahamu anakuja then wanaondoka naye) but msaidizi anaendelea kuwepo. Hapa nimeconnect dots.

Na je hilo la kufunga cctv camera kwenye salon na kuweka msusi but wateja wakipiga simu wanaambiwa wafatwe nyumbani au kuelekezwa kwingine linawezekana kwa salon za kiume? Maana kuna huduma zingine lazima zitolewe pale pale mazingira ya ofisini kama scrub na massage? Na kwa upande wa vinyozi si itakuwa rahisi kubaini kipindi anachokuwa hayupi kazini ilihali mmekubaliana muda wa kufungua na kufunga
 
Hilo la kufunga cctv afu mdaidizi kuwaambia wateja mzigo upo stoo nahisi limenikuta, nimejifunza kitu hapa....nimekuwa nikicheki kwenye cctv camera yangu kuna baadhi ya wateja wanakuja wanakaa muda mrefu wanazungza na msaidizi then baada ya muda kuna kijana (nisiyemfahamu anakuja then wanaondoka naye) but msaidizi anaendelea kuwepo. Hapa nimeconnect dots.

Na je hilo la kufunga cctv camera kwenye salon na kuweka msusi but wateja wakipiga simu wanaambiwa wafatwe nyumbani au kuelekezwa kwingine linawezekana kwa salon za kiume? Maana kuna huduma zingine lazima zitolewe pale pale mazingira ya ofisini kama scrub na massage? Na kwa upande wa vinyozi si itakuwa rahisi kubaini kipindi anachokuwa hayupi kazini ilihali mmekubaliana muda wa kufungua na kufunga
Sikuhizi cctv kwa muuza duka mzoefu ni pambo tu, atafanyia biashara zake kwenye simu kuanzia kupokea miamala mpaka kuwaelekeza wateja ni wapi pa kuchukulia bidhaa tena unakuta na yeye kaweka mtu wake huko kwake

hata kwenye salon za kiume ila kwa vinyozi ni rahisi kidogo kugundua. Tatizo sio tu sehemu ya kazi, mara nyingi ni connection anayojenga mhudumu na mteja. Kama unavyotujua wengi wetu tuko tayari hata kusafiri mbali si kwa sababu hakuna salon nyingine, bali tunamfuata kinyozi tulieamini ubora wa kazi yake na tuliezoea huduma zake.

Kuna vinyozi au wasusi wanajenga ukaribu mkubwa na wateja taratibu, mpaka mteja anakuwa loyal kwake binafsi badala ya biashara yenyewe. Ikitokea siku ameondoka, anaondoka na wateja pia. Ndiyo maana unaweza kuona salon ina vifaa vizuri, location nzuri, lakini mteja anasema “mimi nataka niletewe fulani tu.”

Na kuhusu hizo huduma za scrub au massage zinazohitaji mazingira ya salon, bado wanaweza kupanga muda tofauti au kuwapeleka wateja sehemu nyingine kwa makubaliano yao binafsi. Pia vinyozi sio watu wa kukaa sehemu moja sana, huko anakoenda kunaweza kuwa na mbinu wanafanya kuhamia pamoja na wateja wao.
 
Back
Top Bottom