Wasaidizi kufungua biashara ndani ya biashara kunaua biashara nyingi sana, kijana anadai mshahara kila mwezi kumbe anakuibia mamilioni

Njia rahisi tumia app ya SmartBusiness kusimamia biashara yako, utaweza kufanya stock audit na kama kuna mahali kuna shida utaweza kujua mfanyakazi aliyeleta hasara.
 
Sikuhizi cctv kwa muuza duka mzoefu ni pambo tu, atafanyia biashara zake kwenye simu kuanzia kupokea miamala mpaka kuwaelekeza wateja ni wapi pa kuchukulia bidhaa tena unakuta na yeye kaweka mtu wake huko kwake

hata kwenye salon za kiume ila kwa vinyozi ni rahisi kidogo kugundua. Tatizo sio tu sehemu ya kazi, mara nyingi ni connection anayojenga mhudumu na mteja. Kama unavyotujua wengi wetu tuko tayari hata kusafiri mbali si kwa sababu hakuna salon nyingine, bali tunamfuata kinyozi tulieamini ubora wa kazi yake na tuliezoea huduma zake.

Kuna vinyozi au wasusi wanajenga ukaribu mkubwa na wateja taratibu, mpaka mteja anakuwa loyal kwake binafsi badala ya biashara yenyewe. Ikitokea siku ameondoka, anaondoka na wateja pia. Ndiyo maana unaweza kuona salon ina vifaa vizuri, location nzuri, lakini mteja anasema “mimi nataka niletewe fulani tu.”

Na kuhusu hizo huduma za scrub au massage zinazohitaji mazingira ya salon, bado wanaweza kupanga muda tofauti au kuwapeleka wateja sehemu nyingine kwa makubaliano yao binafsi. Pia vinyozi sio watu wa kukaa sehemu moja sana, huko anakoenda kunaweza kuwa na mbinu wanafanya kuhamia pamoja na wateja wao.
Nimekuelewa kaka, na hizi ni changamoto za biashara mtu ukishajua tatizo basi unatafuta solution yake. Uzi mzuri sana huu kama mtu unabiashara zako unazosimamia ukiwa mbali.
 
Ndo mtafute vijana kama sisi waaminifu sio kulalamika tu kila siku wakati kuna watu tuna mioyo na tunajua bishara zinaendaje
 
Nafikiri mfanyabiashara anajua number zake kuanzia sales mpaka faida, ukiona umeajiri mtu, number zimeenda chini bila sababu ya kueleweka, fukuza haraka sana usifikirie mara mbili, numbers don’t lie
 
Siku hizi baadhi ya wasaidizi hawaji kazini kutafuta mshahara, wanakuja kujifunza mfumo then wanafungua biashara yao ndani ya biashara yako.

Unafungua baa kubwa, unaajiri manager unamlipa vizuri kabisa. Kumbe na yeye ana stock zake pembeni. Wateja wakija wanauziwa vinywaji vyake, stock yako inabaki inakula vumbi store huku ukiambiwa biashara imeshuka.

Unafungua duka la vyombo, wateja wanafika wanahitaji sahani 100, msaidizi anaziuza, hapo hapo anapiga simu kwa wasambazaji wamlete sahani 100 zinazofanana na zilizotoka, wewe unahisi hakuna kilichouzwa.

Unaweka CCTV dukani ukiamini umeimarisha usalama. msaidizi naye anafungua stoo yake ya siri. Wateja wanaambiwa mzigo upo stoo, wanaenda kumalizana nje ya mfumo wako kabisa huku wakidhani bado ni biashara yako.

Unafungua pharmacy, unaweka stock ya kutosha. Ukiondoka kidogo tu, mhudumu anamuita mtu wake anachukua dawa wholesale kwa bei ya chini anauza kupitia counter yako. Mwisho wa mwezi anakwambia biashara ni ngumu huku yeye ndio ana-grow fastest.

Unafungua salon ya kisasa, unaweka CCTV na mazingira safi. Wasusi wanaanza kujenga ukaribu na wateja, kubadilishana namba, hapo sasa wanaanza bookings za pembeni. Wateja wanaambiwa leo kuna foleni au njoo home service. Polepole salon inabaki na viti, wao wanaondoka na customers.

Restaurant nayo same story. Wapishi wanaanza kuuza sahani zao kimya kimya kupitia jiko lile lile, ukiweka cctv wanakula vichwa kwenye delivery, wanawapelekewa wateja vyakula vyao. Ukiangalia stock ya unga, mchele na viungo vinaonekana sawa, ila cashflow haisomeki.

Siku hizi biashara nyingi hazifi kwa kukosa wateja, zinakufa kwa kuibiwa ndani kwa ndani
Inasikitisha sana kwa kweli.
 
Hamna kitu kama hiko..
Wizi unatokea baada ya kukosekana kwa uaminifu
Wengi wanafikiri kama wewe kutoibiwa ni kwa sababu ya wafanyakazi waaminifu si kweli, kinachozuia wizi au hujuma kwa 99% ni mfumo imara, tatizo wengi hawajui hilo, next time before hujaanza any business do your homework na ujue hakuna kitu kinaitwa uaminifu kwenye kuendesha biashara
 
Ukweli ni kwamba ikiwa ivyo ni raisi sana kugundua na kumbadilisha mfanya kazi na kutafuta mwingine

Watoto wa mjini wanakwambia boss apate na sisi tupate so atahakikisha boss anakula faida nyingi na yeye anapata kiasi chake
 
Wengi wanafikiri kama wewe kutoibiwa ni kwa sababu ya wafanyakazi waaminifu si kweli, kinachozuia wizi au hujuma kwa 99% ni mfumo imara, tatizo wengi hawajui hilo, next time before hujaanza any business do your homework na ujue hakuna kitu kinaitwa uaminifu kwenye kuendesha biashara
Wengi tulikuwa tunafikiria kama yeye kabla hatujaanza kuweka wasaidizi, tulijifunza kwa maumivu.

Uaminifu una umuhimu lakini ni lazima kuweka mifumo imara,
 
Sikuhizi cctv kwa muuza duka mzoefu ni pambo tu, atafanyia biashara zake kwenye simu kuanzia kupokea miamala mpaka kuwaelekeza wateja ni wapi pa kuchukulia bidhaa tena unakuta na yeye kaweka mtu wake huko kwake

hata kwenye salon za kiume ila kwa vinyozi ni rahisi kidogo kugundua. Tatizo sio tu sehemu ya kazi, mara nyingi ni connection anayojenga mhudumu na mteja. Kama unavyotujua wengi wetu tuko tayari hata kusafiri mbali si kwa sababu hakuna salon nyingine, bali tunamfuata kinyozi tulieamini ubora wa kazi yake na tuliezoea huduma zake.

Kuna vinyozi au wasusi wanajenga ukaribu mkubwa na wateja taratibu, mpaka mteja anakuwa loyal kwake binafsi badala ya biashara yenyewe. Ikitokea siku ameondoka, anaondoka na wateja pia. Ndiyo maana unaweza kuona salon ina vifaa vizuri, location nzuri, lakini mteja anasema “mimi nataka niletewe fulani tu.”

Na kuhusu hizo huduma za scrub au massage zinazohitaji mazingira ya salon, bado wanaweza kupanga muda tofauti au kuwapeleka wateja sehemu nyingine kwa makubaliano yao binafsi. Pia vinyozi sio watu wa kukaa sehemu moja sana, huko anakoenda kunaweza kuwa na mbinu wanafanya kuhamia pamoja na wateja wao.
Nimekuelewa kaka, na hizi ni changamoto za biashara mtu ukishajua tatizo basi unatafuta solution yake. Uzi mzuri sana huu kama mtu unabiashara zako unazosima
 
Siku hizi baadhi ya wasaidizi hawaji kazini kutafuta mshahara, wanakuja kujifunza mfumo then wanafungua biashara yao ndani ya biashara yako.

Unafungua baa kubwa, unaajiri manager unamlipa vizuri kabisa. Kumbe na yeye ana stock zake pembeni. Wateja wakija wanauziwa vinywaji vyake, stock yako inabaki inakula vumbi store huku ukiambiwa biashara imeshuka.

Unafungua duka la vyombo, wateja wanafika wanahitaji sahani 100, msaidizi anaziuza, hapo hapo anapiga simu kwa wasambazaji wamlete sahani 100 zinazofanana na zilizotoka, wewe unahisi hakuna kilichouzwa.

Unaweka CCTV dukani ukiamini umeimarisha usalama. msaidizi naye anafungua stoo yake ya siri. Wateja wanaambiwa mzigo upo stoo, wanaenda kumalizana nje ya mfumo wako kabisa huku wakidhani bado ni biashara yako.

Unafungua pharmacy, unaweka stock ya kutosha. Ukiondoka kidogo tu, mhudumu anamuita mtu wake anachukua dawa wholesale kwa bei ya chini anauza kupitia counter yako. Mwisho wa mwezi anakwambia biashara ni ngumu huku yeye ndio ana-grow fastest.

Unafungua salon ya kisasa, unaweka CCTV na mazingira safi. Wasusi wanaanza kujenga ukaribu na wateja, kubadilishana namba, hapo sasa wanaanza bookings za pembeni. Wateja wanaambiwa leo kuna foleni au njoo home service. Polepole salon inabaki na viti, wao wanaondoka na customers.

Restaurant nayo same story. Wapishi wanaanza kuuza sahani zao kimya kimya kupitia jiko lile lile, ukiweka cctv wanakula vichwa kwenye delivery, wanawapelekewa wateja vyakula vyao. Ukiangalia stock ya unga, mchele na viungo vinaonekana sawa, ila cashflow haisomeki.

Siku hizi biashara nyingi hazifi kwa kukosa wateja, zinakufa kwa kuibiwa ndani kwa ndani
Nyie mnawaona wahindi wajinga muda wote wapo dukani?
Ukiamua kuwa mfanya biashara kuwa mfanyabiashara kweli. Mambo ya kujifanya uko busy ukisondelea mashahara wako wa mwezi utasanda tu.
 
Usimwamini mfanyakazi. Pia pambana ssna uwepo kwenye biashara yako kwa muda mwingi kadiri iwezekanavyo. Ninadhani watu maduka ya dawa ndo wanaongoza kwa kuibiwa.
Mdogo wangu ni daktari, alikua anapiga kazi kizahanati kimoja mtaani huko cha private. Asubuhi ananunua dawa zake duka la jumla, zile most common. Mteja akija pale keshapanga mchongo na mtu wa famasi anapewa dawa zake. Tajiri analialia. Nyie dunia hii.
 
Inasikitisha sana ndugu. Halafu mkuu umetokea Masqaroda? Nilishawahi kuja huko kwa mganga mmoja konki sana..
 
Bonge moja la changamoto.
Lakini lazima maisha ya bznes yaende tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kibongo bongo kwa sababu technology inaweza kuwa expensive, kuajiri masnichi na rewards kwa atakayeripoti wizi au hujuma inaweza kusaidia
 
Back
Top Bottom