Huo ujinga wa mume au mke kuwa na mamlaka kuwazidi wazazi au ndugu wa muhusika sitaki kusikia.
Kila mmoja akifariki akazikwe kwao isipokuwa tu alitoa taarifa azikwe wapi akiwa hai. Huwezi kuwa na mamlaka ya maiti ya mtoto wangu kwa ujinga unaitwa ndoa
Ukishamzika huyo mme/mke huko unakotaka tayari umekatisha mahusiano kati Yako na familia ya marehemu. Mfano marehemu kwao Tanga wewe unaamua azikwe Dar, hao watoto wako unazani huko Tanga wataenda kufata nini wakati Aliyekuwa anawaunganisha hayupo duniani na mwili wake mnao hapo dar?
Marehemu azikwe kwao Tanga ili wewe na watoto wake mkienda kutembelea kaburi mnatapa wasaa wa kujuana na ndugu wengine wa marehemu au kujuliana hali na undugu unakuwa active.