Wasaidizi wa Rais Samia: Mkutano wa BRICS nyie Mnamwandalia Rais Hotuba ya North-South Geopolitics

Wasaidizi wa Rais Samia: Mkutano wa BRICS nyie Mnamwandalia Rais Hotuba ya North-South Geopolitics

Mambo ya North-South yalishapitwa na wakati zamani sana tokea enzi za ujamaa na kujitegemea. Hizo ni siasa za enzi ya Nyerere. Bora angekaa kimya kama alivyoamua kufanya nyumbani maana ni aibu. Nyumbani anauza rasilimali za nchi kwa kampuni za kiarabu bila ya ridhaa ya wananci au hata bunge, halafu kwenye mkutano wa kimataifa anapata ujasiri wa kuleta hadithi za North-South/nchi za kibepari dhidi ya nchi maskini?
 
Angestic kwenye hiyo theme adadavue namna gani italeta faida angeua sana. Ni namna gani Brics inaweza kabili changamoto za Sasa na zijazo kama katika biashara na uwekezaji.
 
Angestic kwenye hiyo theme adadavue namna gani italeta faida angeua sana. Ni namna gani Brics inaweza kabili changamoto za Sasa na zijazo kama katika biashara na uwekezaji.
Na ajikite kwa Tz. Ndio Foreign policy yetu. Economic Diplomacy, mfano Tanzania ina nini ambacho Brics wanaweza kupata pa kuwekeza, mfano Kilimo, gesi, chuma etc
 
Asalam.
Nimefuatilia hotuba ya Rais wetu Mpendwa. Nikaona maudhui Mengi ni ya Mkutano Mwingine, sio huu. Hotuba imejaa masuala ya North-South badala ya BRICS. Iko hivi,
Kwenye Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa kuna miungano mingi ya namna nyingi (Intergrations). North_South ni mojawapo ya mahusiano ya muda mrefu sana toka nyakati za uhuru miaka ya 1960 ambapo dunia ilikuwa na pande mbili, North (kaskazini ) ikizikusanya Nchi zilizoendelea na zikiwa na mitaji, viwanda, technology etc. Kusini zikiwa nchi masikini. Pili tukawa na nchi za mashariki ( za kijamaa ) na za Magharibi ( za kibepali) na tukawa na na NAM ( Nchi zisizofungamana na upande wowote). Miaka ya 80 na 90 mashariki ikaharibika na kwa sehemu kubwa tukabaki na magharibi ilhali nchi za kijamaa zikihangaika wapi zishike. Pakazaliwa Nchi zilizoendelea, zilizoendelea na Masikini.

Lkn miaka 10 iliyopita ikaziliwa huu Muungano wa BRICs (Brazil, Russia, India, China) zikilenga kutengeneza muungano wa kipekee, na ukawa na mambo yake. Kwenye BRICS hakuna Marekani na Uingereza, ufaransa, Italy ambazo ni vinara wa North.

Sasa Rais anapohutubia masuala ya NORTH SOUTH kwenye MKUTANO wa BRICs ni kukosea. Lkn dah. Muwe makini.
Hao waandishi wa hotuba ni wazee wa 'Copy and paste' .
 
Nafikiri tungeomba uanachama, huu ndio unaweza kuwa muungano wa Kidemokrasia na faida, win- win situation kwa
Demokrasia ipi unayomaanisha ?

Na huko mbeleni labda BRICS itakuwa na jeshi lake, benki zake, sheria zake, mbadala wa UN, G7, IMF, World bank, mahakama zake za usuluhishi migogoro, tofauti kwa haki.
Benki tayari ipo, ila hayo mengine zitabaki kuwa ndoto tu.
 
Sasa na yeye kwanini anakubali kulishwa tangopori? Hajui hadhira anayoenda kuihutubia?. Aipitie kabla hajaenda jukwaani.
Nimeiweka hapo. Iangalie. Tuendako tutaomba kama inawezekana wawe wanatoa taarifa mapema ya mikutano atakayohudhuria President halafu JF tunawapa dondoo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaona sawa kama.haujui tofauti zake na protocols za hizi miungano. Wenyewe wenye muungano wao wanakushangaa. Ni sawa na kutafuta spea za tractor kwenye duka la vipodozi.
Hii tunaita #BothTeams Not to Score🤣
 
Yeye mwenyewe je alikua anajua anachokizugumza.
Hahahaha umenichekesha sana iyo kuna siku nitawapa lecture wanafunzi wangu, Tanzania nchi ngumu sana nimekubaliana na wewe,shida nafasi seriously wanapeana kiukoo unaweza ukakuta Nape ñdyo aliandaa
 
Huyu mama mara nyingi nasemaga hua asomi kabisa vitu kabla ya siku y mwisho YY anasoma palepale siku ya tukio.
Rejelea makataba wa bandari watu wamempeleka chaka.ndio matokeo yake haya ss..
 
Back
Top Bottom