Nimeshangaa sana wasanii bado wanapeleka burudani kwenye mji wa Mbeya uliojaa binadamu washamba kupindukia.
Acheni kupeleka burudani kwa watu wasiostaarabika kama wakati ule mlivyofanya kwa Arusha.
Watu wa Mbeya bado wapo kwenye ujanja 1980s ule usela nondo, fujo za kinyani.
Kwanza mji wenyewe wanaita jiji lakini kuna nyumba za tope mpaka leo mjini, mji vumbi tupu, mji hauna hotel ya 3 star, hauna malls wala burger points, hakuna hata international office moja. Wakipata jengo lenye lift wanaita mpaka spika akazindue.
Watu wa burudani achaneni na huo mkoa waendeleee kumsikiliza na kuburudishwa na Awilo wao.
Mtu anatoka kwake anaenda kwenye burudani kufanya vurugu, kutupa chupa, kutukana matusi kama kalazimishwa kwenda vijana wa Mbeya wanaona kuwa wahalifu ni ujanja.
Mwaka 2020 huko kwenye viwanja wa Hard Rock ,Miami Marekani, Rapper Kad Cudi alirushiwa makopo na washabiki,Je Watu wa Miami ni Washamba kama wa Mbeya?
Mwaka 2020 GDP ya Mbeya kwa ujumla ilikuwa ni Dola bilioni 8 chini ya Mkoa wa Mwanza na Dar es salaam tu, naomba unioneshe Kijiji kimoja Cha Mkoa uliotoka chenye GDP sawa na Mbeya.
Eden Highlands Hotel na G town Hotel ni Hotel zenye hadhi ya 4 🌟 ulikuwa unatafuta 3 🌟 hotel Mimi nimekupatia 4 ....
Kuhusu vumbi, unapafaham kwa Mrombo, Patel, nado, Dampo kipindi Cha kiangazi Pako vipi?
Je umewahi kufika Swaswa, Maili mbili Area A, Kikuyu ,Mkonze kuanzia mwezi wa Sita?
Unaposema International office unakuwa hueleweki ( maana ya haraka haraka ni ofisi inayotoa huduma kimataifa) kama maana ni hiyo basi Stanbic bank ni international office, NMB, CRDB, Hotel Desderia zote zina fall katika category hiyo...lakini kama ukimaanisha office ambazo ni zao la FDI's hapo zipo nyingi sana kuanzia benki, viwanda vya malumalu/marumaru na mengine mengi.
Pia kuwa na wingi wa skyscrapers si jambo moja tu linaloifanya jiji kuwa attractive...London, Manchester, Berlin, Cape town, Port Elizabeth, Washington DC ni miji ambayo Haina majengo marefu sana kama ilivyo Dubai, Joburg, New York, Hong Kong, Beijing, LA, Dallas...lakini hiyo miji haipo kwenye orodha ya ugliest cities in the World..
Mbeya Kuna nyumba za matofali mabichi na si nyumba za tope,naomba usipotoshe...halafu nikuambie nyumba nyingi kule Ghana, soko matola zimejengwa kwa matofali mabichi lakini ni Imara hata hizo block zako zikasome...
Sehemu za baggers si uende hoteleni Mzee, nenda tughimbe, Utengule utazipata hizo baga....
Uliza wenyeji wakuambie machimbo,jombaa hata kama una milioni 20 unataka kuipiga kiberiti kwa wiki moja,nenda Mbeya tukuoneshe machimbo ili wakati wa kurudi huko kwenu ubakiwe huna kitu na tukuchangie nauli.
All in all two wrongs don't make one right, Zuchu alikosea lakini hata washabiki walikosea ku react walivyo react...
Karibu sana Mbeya 😂😂😂😂💪💪💪💪