Wasanii wa kike wa Bongo Fleva ambao walitamba kisha wakatoweka

Wasanii wa kike wa Bongo Fleva ambao walitamba kisha wakatoweka

Kuna yule aliimba "nakuhitaji mpenzi wangu nakuhitaji" sijui cat b
 
Kuna yule aliimba "nakuhitaji mpenzi wangu nakuhitaji" sijui cat b
Anaitwa Sarah kama sijakosea, aliimba na Caz T mtoto wa Komba. Mara ya mwisho kumuona alikuwa ni mtangazaji wa ITV na Radio one katika vipindi vya nyimbo za injili
 
yule mwanadada alikua ni hatari. Alitisha sana kwenye mdundo wa nako2nako hawatuwezi, na ile aliyoshilikishwa na makamua (so baby please rudi nyumbani). sijui kwa nini aliamua kuacha mziki
Kuna sababu nyingi sana kwa wasanii wengi wazuri kujitoa kwenye muziki bongo,....
 
List haiwezi kukamilika bila kumuweka Fatma yule dada yake na Hardmad, dada alikuwa anaimba aisee, kipindi hiko bila kumuweka kwenye chorus wimbo wako haukubaliki kitaa.

Ule wimbo wa Eno mic wa Ziggy D wa Uganda mpaka leo nausikilizaga saana hasa kile kisauti cha huyu bidada.
Aiseee Hardman na Fatma waliimba lile goma lao linaitwa TAMALA lilibamba kinoma noma. Hilo la Eno Mic nakumbuka mwaka 2003 kuna jamaa zangu Waingereza walinikutaga nasikiliza kwenye Walk-Man wakalipenda kinoma, wakaomba niwaandikiage mistari yake. Daah hata kiganda chenyewe nikawa sijui, nikaandikaga pumba tu. These moments were one among the Best times of my life.......
 
Back
Top Bottom