SoC04 Wasanii wasitumike ovyo na wanasiasa kipindi cha uchaguzi kwa kutanguliza pesa bali waangalie sera na maono ya wanasiasa hao katika kuleta maendeleo

SoC04 Wasanii wasitumike ovyo na wanasiasa kipindi cha uchaguzi kwa kutanguliza pesa bali waangalie sera na maono ya wanasiasa hao katika kuleta maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Tanzania ni miongoni kati ya nchi zilizobahatika kuwa na wasanii wengi sana wazuri, ambao ni wasanii wakubwa na mashuhuri ndani na nje ya nchi. Lakini pia kwa asilimia kubwa ya wasanii wetu hao, wengi wamekuwa ni wasanii wenye ushawishi mkubwa sana kwenye vitu mbali mbali vingi sana ikiwemo kwenye upande wa masuala ya siasa ndani ya nchi yetu. Kwa kweli hili ni jambo jema sana kwetu watanzania na tunajivunia kuwa na wasanii wenye mchango mkubwa kwetu sisi kama taifa kwenye vitu mbali mbali ikiwemo kwenye siasa zetu za nchi. Lakini pamoja na hayo yote hapa ninasuala moja kwa upande wa wasanii wetu hapa nchini, ambalo ningependa kuona likifanyiwa mabadiliko. Suala lenyewe ni hili la wasanii wetu hapa nchini kutumika hovyo na wanasiasa hasa ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi kwa kutanguliza tu pesa.

Ni wazi kwamba imekuwa ni kawaida kwenye nchi yetu kuona kila ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi, kuona wasanii wetu wengi wakitumiwa na wanasiasa kwenye masuala ya chaguzi hizo. Katika uhalisia mara nyingi tumekuwa tukiona wasanii wetu wengi wamekuwa wakitumika na wanasiasa hasa ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi ili wawashawishi watanzania waweze kuwachagua kwenye chaguzi zetu hizo. Japo jambo hili naweza kusema wala siyo jambo baya, kwa kweli wasanii wetu kutumika na wanasiasa hasa ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi siyo jambo baya, tatizo lipo pale kwa baadhi ya wasanii wetu hao wanapotumia fursa hiyo kama nafasi ya wao kujiingizia kipato pekee badala ya kuangalia pia kwenye upande wa sera na maono ya wanasiasa hao wanaowatumia katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Yani hapo inamaana mwanasiasa atamlipa pesa msanii kusudi likiwa ni kwamba msanii huyo aje kuwashawishi watanzania wamchague yeye kwa kuwa tu amemlipa pesa, yani inamaana pia msanii atakuja kukushawishi ukamchague mwanasiasa flani ambaye siyo kwamba labda anafaa na anasera nzuri au siyo kwamba labda ni mwenye maono bora ya kuleta maendeleo kwenye jamii ya watanzania, hapana bali ni kwasababu tu mwanasiasa huyo amemlipa yeye pesa, ndiyo maana anakuja kukushawishi ukamchague mwanasiasa huyo kwakweli jambo hili siyo sawa na halina afya kwenye taifa letu hata kidogo. Kwa kweli wasanii wetu watakapotumika hovyo kama hivi kunaweza hata kuathiri chaguzi zetu. mfano kunaweza kupelekea uwepo wa wanasiasa wengi watakao chaguliwa na watanzania kwenye chaguzi zetu kuliongoza taifa ambao hawatoleta maendeleo yoyote, ambao walichaguliwa na wananchi kwa kushawishiwa na wasanii kwasababu tu wanasiasa waliwalipa pesa na siyo kwamba wanamaono mazuri ya kuleta maendeleo na mabadiliko kwa watanzania.

Unajua hapa tunaweza kusema labda kwa asilimia flani ni sahihi kabisa kwa msanii yoyote yule kupokea pesa ili kupata malipo kutokana na kazi yake anayoifanya sawa, lakini linapokuja suala la msingi sana kwetu la kuchagua wanaoenda Kusimamia taifa letu la Tanzania, yani jambo la muhimu sana kiasi kwamba endapo labda tukifanya makosa tu kidogo linaweza kugharimu mali zetu au hata maisha yetu yani kwenye suala zima la uchaguzi, kwa kweli kwenye suala hili wasanii hatupaswi kutanguliza tu pesa. Naomba ifahamike kwamba masuala ya chaguzi kwenye taifa letu ni mambo ya msingi sana, alafu ni ya muhimu kupita kiasi ambayo yanamuhusu kila mmoja wetu ndani ya nchi na kama labda endapo sisi kama taifa tutakapofanya makosa yoyote yale kuna weza kuleta madhara kwa kila mtanzania kwenye nchi nzima, kwahiyo hata wasanii wetu hawapaswi kutumia ushawishi wao vibaya kwa kutanguliza tu pesa kwenye mambo ya msingi na ya muhimu sana kwenye taifa letu.

Mapendekezo
Nashauri wasanii wasitumike hovyo hovyo na wanasiasa hasa ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi kwa kutanguliza tu pesa, bali waangalie pia sera na maono ya wanasiasa husika wanaowatumia kuwashawishi watanzania wawachague kwenye chaguzi zetu, wasanii waangalie kwamba je wanasiasa hao wanaweza kweli kuleta maendeleo kwa watanzania, siyo tu wasanii wetu waangalie pesa pekee, bali wasanii wetu waangalie pia na maono yao kabla ya kutumiwa kama kishawishi kwa jamii ya watanzania. Ikimbukwe kama ikitokea tatizo lolote linaweza kuwagharimu hata wao pia, hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa wasanii kuangalia sera na maono ya wanasiasa hao wanaotaka kuwatumia kuwashawishi watanzania wawachague, kwa kufanya hivi tutakuwa tumefanya jambo la msingi sana kwenye nchi yetu.

Wasanii wetu kutumika na wanasiasa hasa ifikapo kwenye kipindi cha uchaguzi kwa kweli wala siyo jambo baya, lakini wanapotumika na wanasiasa hao wasitumike tu hovyo kwa kutanguliza tu pesa, bali watumike kwa namna chanya yenye kuleta faida kwao na taifa kwa ujumla, kwa kuangalia pia kwenye upande wa sera na maono ya wanasiasa hao wanaowatumia kuwashawishi watanzania wawachague kwenye chaguzi zetu kama kweli wanasiasa hao wanaweza kupelekea tuipate Tanzania bora tuitakayo. Kwani kwa kufanya hivi tunakuwa tunaijenga Tanzania bora tuitakayo kweli kweli, lakini siyo watumike tu hovyo na wanasiasa kwa kutanguliza tu pesa, kwasababu ikumbukwe kama labda wanasiasa hao watakuwa na sera mbovu na maono mabaya ya kimaendeleo kama kukitokea tatizo baadae linaweza kuwapata watanzania wote ikiwemo na wao pia, hivyo kuna umuhimu wa wasanii wetu kuangalia kwa undani pia sera na maono ya wanasiasa hao wanaowatumia kama kishawishi kwa watanzania.

Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo wasanii wetu hawatakuwa wakitumika hovyo na wanasiasa kwa kutanguliza tu pesa, bali ni kwa kuangalia sera na maono ya wanasiasa hao katika kuleta maendeleo kwa watanzania.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom