Washington: John Mnyika aanza ziara kwa kishindo, atembelea VOICE OF WASHINGTON DC. Ailipua sheria ya Uchaguzi

Washington: John Mnyika aanza ziara kwa kishindo, atembelea VOICE OF WASHINGTON DC. Ailipua sheria ya Uchaguzi

Voice of Washington DC = Voice of America? Wewe mfuasi wa Mbowe uliandika huu uzi ukiwa umelewa mataputapu?
Screenshot_2023-09-05-22-31-54-1.png
 
View attachment 2835142

Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika , aliye kwenye ziara ya kikazi Nchini Marekani, ameanza kutembelea vyombo vya habari vya Nchi hiyo na kuanika uozo unaoendelea nchini Tanzania.

Akihojiwa na Kituo cha TV cha Washington DC, amefichua kwamba Mchakato wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi umedorola kwa sababu ya njama za ccm kwa vile wana hofu ya kung'olewa madarakani.

Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba kwenye bunge la January Chadema itahakikisha miswada hiyo inarekebishwa.

Hapa kwenye kuhakikisha inarekebishwa Ndo napata mashaka, labda watawatumia wabunge wa COVID 19
 
Huyu katumia zaidi ya milioni 300 kwenye ziara hii, anaenda kupiga mdomo tu ili ale ruzuku ya Chadema,tangu akiwa kijana mdogo yeye ni kupiga mdomo tu, hana shamba, hana maradi wowote, ni mdomo tu
Formula
 
Ukitaka kujua CDM imeishiwa basi mfano hai ni uteuzi wa John Mnyika kuwa katibu mkuu.

Sio kwamba Mnyika ni mwanasiasa mmbovu. La hasha Mnyika alishaweka wazi malengo yake baada ya 2020 hata gombea ubunge na wala hataki uongozi wa siasa, isipokuwa atabaki mwanachama mtiifu wa CDM.

Katika wanasiasa walioshiba na kutumia mshahara wao vizuri kwenye investment ni Mnyika na mtu anae ridhika haraka.

Hiyo nafasi ya katibu mkuu kapewa kwa sababu ya usaliti wa aliekuwa kaishika kuamia CCM.

Hila kwenye kichwa cha Mnyika alishastaafu siasa 2020 baada ya hapo aendelee na maisha mengine.

Kwa sasa kwenye hiyo nafasi analipa fadhila tu kwa kuombwa na Mbowe (mind you Mbowe ana amini loyalty ya watu wawili tu Mnyika na Salum Mwalimu huyu ni mtoto wake wa kufikiia ndio yupo comfortable kudhurula nae).

Ila Mnyika hana shida na hiyo nafasi, wala mshahara wake na marupurupu yake; anaonekana ana mbinu zingine za kutengeneza hela zinazorodhisha kwa maisha anayoyataka yeye sio lazima utajiri mkubwa.

Ndio maana umuoni Mnyika kushiriki kwenye mikutano yao huko mikoani kutafuta posho kama wenzake.

Mnyika kwa sasa yupo kwenye siasa kwa sababu ya loyalty kwa heshima ya god father wake Mbowe and nothing else; deep down angependa kuwa raia wa kawaida. na kuangaika na mikakati yake mengine ya kuingiza kipato nje ya siasa. Hans njaa ya mshahara wa million saba kuna sehemu kubwa anaona anaweza tengeneza zaidi ya hiyo akiachwa huru.

Hutaki acha

Ujinga zaidi ni kuamini Mnyika ni tumaini la kesho la CDM.
Jiuwe na ukife
 
View attachment 2835142

Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika , aliye kwenye ziara ya kikazi Nchini Marekani, ameanza kutembelea vyombo vya habari vya Nchi hiyo na kuanika uozo unaoendelea nchini Tanzania.

Akihojiwa na Kituo cha TV cha Washington DC, amefichua kwamba Mchakato wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi umedorola kwa sababu ya njama za ccm kwa vile wana hofu ya kung'olewa madarakani.

Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba kwenye bunge la January Chadema itahakikisha miswada hiyo inarekebishwa.
Amesahau kuanika ukweli kuhusu ruzuku ya cdm inavyoliwa
 
Jiuwe na ukife
Nijiuwe nina shida gani kwenye maisha, wakati nina ndoto kibao bado nafukuzia.

Speak for yourself if you have suicidal thoughts.

CDM imeishiwa na inatafuta matatizo, hata hiyo michango ya kusaidia mafuriko sidhani kama chama cha siasa kinarihusiwa kuchangisha, wao sio NGO siku wakiitwa ofisi ya msajili kutoa maelezo utasikia wanalalamika wanaonewa.

Wangetoa hela bank kusaidia sawa, ila kuitisha harambee ya kusaidia kwenye maafa uhitaji kwanza kusoma sheria ya usajili wa vyama vya siasa kubaini hilo ni kosa la mipaka ya usajili.

By the way Mnyika msimamo wake ulikuwa wazi ni maneno yake kabla ya uchaguzi wa 2020 yeye siasa za mstari wa mbele kwake ilikuwa basi tena.
 
Huyu katumia zaidi ya milioni 300 kwenye ziara hii, anaenda kupiga mdomo tu ili ale ruzuku ya Chadema,tangu akiwa kijana mdogo yeye ni kupiga mdomo tu, hana shamba, hana maradi wowote, ni mdomo tu
Kwani kazi ya siasa si ni kupiga domo tu? Kingunge na wengine unaowajua hapo lumumba walishawahi kuwa na mashamba wapi tangu wakiwa wadogo?
 
Back
Top Bottom