Washkaji wenye Afro mnafanyaje nywele zinakuwa nyingi kiasi hicho

Usioshe Kila siku.
Ukiosha chana ikiwa mbichi,taratibu.
Isokote uzi,iache ikauke... usipendelee kutumia blow dryer

Tumia steaming,,
Tafuta mafuta mazuri ya nywele..yapo mengi.
Mafuta ya mnyonyo yanajaza nywele ila harufu yake ni mbaya kiasi.
 
Kuoga bila kuoshwa kichwa ni ngumu sana…
Kuna wakati niliweka style ambayo haitakiwi nywele ipate maji, sasa wakati wa kuoga nakuja kushtuka nishajimwagia maji.
Wenzio wanakaa miezi sita bila kuosha kichwa ndio utajua hujui!
 
Nikugawie nywele zangu?
Zina asili ya huko mashariki ya kati
 
Tumia mafuta ya belavista, wana akaunti Instagram wanauza online mafuta yao ni mazuri sana na yanajaza nywele na kuzuia kukatika mimi niliwahi tumia.
 
Kuna mafuta ya nywele yanaitwa vaseline ni ya maji... Ukishaoga kausha nywele then paka hayo mafuta.... Hayo mafuta ni unyama mtupu utakuja kunishukuru.... Kachupa kake kanafanana na ka gricelini......

Kadogo kanauzwa 5000/6000 na kubwa ni sh 10000.... NI UNYAMA MTUPU
 
Tumia mafuta ya belavista, wana akaunti Instagram wanauza online mafuta yao ni mazuri sana na yanajaza nywele na kuzuia kukatika mimi niliwahi tumia.
Mkuu unaweza share link
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…