Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Kwa mazingira hayo, kilichooa hapo ni ajira na si mapenzi; chukulia mfano uko kwenye ndoa, mara ghafla ukapata ajali na ukawa kipofu; hapo si mtakimbiana?
 
Nimekuelewa mdogo wangu, unamtizama na mwanaume husika. Kuwa haya ni maisha, muhimu tu asiwe mvivu atatafuta kazi nyengine. Tatizo mdogo wangu akiwa mvivu.
Unaweza ukapaboresha kwa kusema, nataka mwanaume mwenye maono ya kuona mbali
 
Mkuu hizi mbwembwe na masharti ya kuwa na kazi and so on kwa wanawake ni umri kati ya 18 - 29. Huu muda ndio wanakuwaga na masharti kibao wako radhi hata kuwa vimada cha msingi ni pochi yako tu.

Shughuli yao inaishaga wakiwa na 30 na kuendelea, hapo huwaga hawachaguagi wanajua jua limeshazama (Umri umeenda) wanaweza wakakosa kabisa.
Umri huo huwa yeyote alie mbele yao huwa hawakatai.
 
Sidhani kama umemuelewa mtoa mada, hajamaanisha uolewe na marioo au kibenten hapana, alichomaanisha ni kuwa uolewe au kuoa kwa sababu ya upendo, mengine ni nyongeza.
 
Kizazi hiki Cha kudanga ni hatari Sana kwenye mustakabali wa ndoa..wanawake waelewa ktk hili wachache Sana..Sio Kila mwanaume anakuwa tayari amejikamilisha ndio aingie kuoa..Mwanaume akiwa na vision ya Nini anataka kufanya na anajibidisha inatosha.Mengine Mungu atafungua mbele ya safari .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…