Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Nimekusikia ahsante saaana
 
Hilo neno
 
Tumeshawasoma ....ni mwendo wa kufunua tu na kufunika kwa hawa wenye akili za kushikizwaa...yaan mtu anakuuliza unafanya kazi.gani wkt yy nI housegirl mtaa wa pili...na ukimwambia kazi yako anaanza idharau as if yey anafanyia UN
Sio sawa kabisa
 
Sikusema hivyo soma vigezo vyangu vyote.
Upendo ni nyongeza, ahsante saaana
Sio sahihi kazi ni kazi tu
 
Nimekuelewa vizuri
 
Kwa upande wa dini yangu ya Kiislamu hakuna ndoa ya watu wa dini tofauti.
So,Dini ni muhimu bila hivyo itakua ndoa ya Wazinifu.

Mkuu umekosea.

Dini ya kiislamu inaruhusu mwanaume wa kiislam kuoa mwanamke wa dini zingine zilizoletewa Kitabu... yaani (wakristo na wayahudi..)

Waislamu wengi madrasa mnafundishwa kukariri kiarabu.. huku hampewi maana sahihi ya hicho kiarab mnachokikariri

Mfano Kassim majaliwa ambaye ni muislamu kamuoa mkristo marry majaliwa. Hapo kwa dini ya kiislam ni ndoa halali kabisaa



inaruhusiwa kwa mwanaume wa Kiislamu kuoa mwanamke asiye Muislamu maadam awe Mkristo au Myahudi. Lakini hairuhusiwi kwake kumuoa mwanamke asiyekuwa Muislamu ambaye si mfuasi wa dini ya Ukristo au Uyahudi. Dalili ya jambo hili ni aya ya Qur’an ambapo Mwenyezi Mungu anasema:

“Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na mmehalalishiwa (kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu. (NI halali kwenu kuwao) mtakapowapa mahari yao, mkafunga ndoa, biloa kufanya uzinzi wala kuwaweka kinyumba.” (5:5)

Katika kusherehesha aya hii, Imam Tabari anasema:

“Wanawake wema miongoni mwa waumini na wanawake wema miongoni mwa wale waliopewa”, maana yake ni wanawake walio huru miongoni mwa wale waliopewa Kitabu nao ni Wayahudi na Wakristo wanaoamini yaliyomo katika Taurati na Injili. Mnaruhusiwa kuwaoa mnapokuwa mmewapa mahari yao (Tafseer al-Qurtubi, 6/104)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…