Wasikilizaji wa Radio Imani: Ole wake atakayewalisha watoto wetu mchele wa msaada wenye virutubisho

Hiyo redio ni ya kipuuzi kuwahi kutokea nchini. Hata hao watangazaji wao ni wapuuzi na wakiukaji wa miiko ya utangazaji. Hao waislam ni kina nani duniani/nchini mpaka watoe ole? Ni wapuuzi, wana uhakika gani kama huo mchele ni mbaya? Basi kama ni hivyo watoto wao wasile, watakula wengine na wasilalamike kubaguliwa, shame on them
 
Huko Sudan, Yemen na Somalia kwenye waislam wa kutosha wanakula mchele wa Mamarekani. Gaza unashushwa kwa maparashuti watu wanaugombea ..... Tanzania maskini jeuri. Kuna watu hajui kuwa Tanzania almost 40 % ya watoto wamedumaa kwa ajili ya kukosa lishe bora. Yaani watoto wapate utapia mlo kwa vile tu wanasubiria mchele wa Kyela. Watoto dodom wanashindia mboga mboga za majani sometimes bila hata kuonja starch. Kama Tanzania ina chakula cha kutosha si iwapelekee huo mchele wa Kyela bure .... kwa mwka mzima.

Anyway, Watu wengi hawajui kuwa huo msaada haukuja kwa bahati mbaya. Actually, huu msaada ni wa tatu .... tayari serkali ilishapokea msaada wa kwanza, watoto wakaupiga, wakapokea wa pili wakapiga .... sasa hii awamu ya tatu tumejua kwa kuwa tu serikali ya USA wametangaza.

Kwangu mimi, Bashe namumuona ni Mnafiki mkubwa. Haiwezekani chakula kiingie nchini hata kama ni cha msaada bila Wizara ya Kilimo kutoa kibali. Pia huo mchele ukiingia lazima upewe msamaha wa kodi .... hivyo Mwigulu naye lazima afahamu. Kwa wao kuanza kupiga danadana na kuwapotosha wananchi ndiyo wameleta taflani isiyokuwa na sababu. Badala ya kuwaeleimisha wananchi wao wanakuja na siasa na propaganda zao. Pathetic...!!

Hata North Korea wenyewe wakizidiwaga huwa wanaupokea mchele wa marekani ..... ndiyo ije hii Tanzania yetu.
 
Nawaunga mkono kwa 100% , virubisho kwenye vyakula ati kupunguza utapia mlo kwa watoto, hivi kwa umri huu tumefika kwa kula vyakula vyenye virutubisho kutoka ulaya?

Wanunue vitabu na kugawa mashuleni, wawekeze katika vyuo vyetu hasa vya kati mfano veta, mambo ya vyakula tz tuna vyakula vya asili ambavyo vimejaa virutubisho kibao , na vimetukuza vizuri tu
 
Hoja yako ingekuwa na maana kama ungeondoa udini.
Hoja imeletwa na redio ya kidini na mjadala unaendeshwa kwa misingi ya kidini mimi nauondoaje mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…