Wasikilizaji wa Radio Imani: Ole wake atakayewalisha watoto wetu mchele wa msaada wenye virutubisho

Waislam wako sawa na wana uhuru wa kuukataa huo mchele.
Na Kwa wakristo kama wanaona unawafaa ni fursa nzuri kuchukua chakula cha kutosha wakale na familia zao.

Ila usiseme ni ubaguzi wa kidini maana hamna dini inaitwa marekani, zipo nchi nyingi ambazo hazikubaliani na marekani na siyo nchi za kiislam.
Huo mchele mimi nautaka sn
 
Sakata la mchele wenye virutubisho kutoka Marekani limeendelea kuchukua sura mpya baada ya waislamu kuukataa bila kumumunya maneno. Wakiongea kupitia redio ya kiislamu ya Imaan FM inayounguruma kutokea mkoa wa Morogoro, wamesema hawautaki mchele huo na wametoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayewalisha watoto wao. Wamesema chakula wanacho cha kutosha hapa nchini na kushauri waletewe vitu wasivyokuwa navyo kama vile ndege, magari na ambulance.

Ili kuonyesha kuwa hawatanii katika hili, hata watangazaji waliokuwa wakiendesha kipindi walionekana kushabikia kitendo hicho. Mtu yeyote aliyepiga simu kwenye kipindi akionyesha kwenda kinyume na msimamo wao, walimkatia simu mara moja. Hebu wasikilize wewe mwenyewe kupitia klipu hiyo hapo chini.

MAONI YANGU
Huu mchele sasa naona umeanza kutugawa kiitikadi. Wakristo nao wakitoka hadharani na kuweka msimamo wao, hapatatosha. Ifike mahali ubaguzi wa kijinga kama huu ukemewe kwani unaweza kuligawa taifa na kuhatarisha umoja na mshikamano tulio nao hapa nchini. Tusiruhusu kikundi kidogo cha watu kitugawe kwa sababu yoyote ile.

Nawasilisha.
CCM NI JANGA LA TAIFA WAPO KWA AJILI YA MASLAHI YAO
 
1. Wawe jasiri na kusema atakayewalisha watoto au mtu mzima atakayeula mchele huo, wao kama Waislam(kikundi) watamfanyaje? (Waitaje adhabu itakayompasa)
2. Ingefaa watambue na wakubali kwamba watoto kama watoto, kwa tabia za kitoto unavyozijua, wataula tuu bila wao au ww mzazi kujua. Isitoshe watoto ni watoto wa Taifa hili. Wazingatie kutokuanzisha aina ya Ubaguzi -Vinginevyo wakawatoe huko mashuleni watoto wanaosema eti ni watoto wao kutakakopelekwa huo mchele. Mbona tunataka kuanzisha fitina isiyo na maslahi ndani ya Taifa hili?
 
Kukataa sio shida sana, vp lakini wametoa suluhisho utatumika mchele, maharage, mafuta gani? Na nani atatia vitu hivo?
 
1. Wawe jasiri na kusema atakayewalisha watoto au mtu mzima atakayeula mchele huo, wao kama Waislam(kikundi) watamfanyaje? (Waitaje adhabu itakayompasa)
2. Ingefaa watambue na wakubali kwamba watoto kama watoto, kwa tabia za kitoto unavyozijua, wataula tuu bila wao au ww mzazi kujua. Isitoshe watoto ni watoto wa Taifa hili. Wazingatie kutokuanzisha aina ya Ubaguzi -Vinginevyo wakawatoe huko mashuleni watoto wanaosema eti ni watoto wao kutakakopelekwa huo mchele. Mbona tunataka kuanzisha fitina isiyo na maslahi ndani ya Taifa hili?
Maisilamu baadhi ni majinga, makirisitu mengi yana akili, hata msaada utoke Maka au Iran yanauchukua.
 
Sakata la mchele wenye virutubisho kutoka Marekani limeendelea kuchukua sura mpya baada ya waislamu kuukataa bila kumumunya maneno. Wakiongea kupitia redio ya kiislamu ya Imaan FM inayounguruma kutokea mkoa wa Morogoro, wamesema hawautaki mchele huo na wametoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayewalisha watoto wao. Wamesema chakula wanacho cha kutosha hapa nchini na kushauri waletewe vitu wasivyokuwa navyo kama vile ndege, magari na ambulance.

Ili kuonyesha kuwa hawatanii katika hili, hata watangazaji waliokuwa wakiendesha kipindi walionekana kushabikia kitendo hicho. Mtu yeyote aliyepiga simu kwenye kipindi akionyesha kwenda kinyume na msimamo wao, walimkatia simu mara moja. Hebu wasikilize wewe mwenyewe kupitia klipu hiyo hapo chini.

MAONI YANGU
Huu mchele sasa naona umeanza kutugawa kiitikadi. Wakristo nao wakitoka hadharani na kuweka msimamo wao, hapatatosha. Ifike mahali ubaguzi wa kijinga kama huu ukemewe kwani unaweza kuligawa taifa na kuhatarisha umoja na mshikamano tulio nao hapa nchini. Tusiruhusu kikundi kidogo cha watu kitugawe kwa sababu yoyote ile.

Nawasilisha.
Hakuna itikadi hapo acheni ufisadi ili mambo ya kijinga ya kuomba mchele Marekani yaishe.
 
Hatuna njaa wala uhaba wa nafaka kwanini wasipeleke Kenya, Sudan, na kwingineko kwenye uhaba wa chakula?
Kama kuna chakula cha kutosha hapa nchini kwanini wanafunzi wanashinda njaa mashuleni? Kwanini serikali haiwapelekei huo mchele wakapikiwe? Je, wewe hapo ulipo uliwahi kujitolea angalau kilo 5 za mchele ukawapelekea wanafunzi wapikiwe au unabwabwaja tu kama debe shinda wakati watoto wetu wanaendelea kudumaa kwa utapiamlo? Ficha ujinga wako mkuu.
 
Hicho chakula chako cha Marekani kinatosha kwa shule zote nchini Tanzania au kwa majiji tu?Je kipindi ambacho hicho chakula chako hakikuwepo watoto hawakusoma?Zaidi ya yote baada ya kuleta mchele kutoka Marekani division zero zitaisha?
 
Kama kuna chakula cha kutosha hapa nchini kwanini wanafunzi wanashinda njaa mashuleni? Kwanini serikali haiwapelekei huo mchele wakapikiwe? Je, wewe hapo ulipo uliwahi kujitolea angalau kilo 5 za mchele ukawapelekea wanafunzi wapikiwe au unabwabwaja tu kama debe shinda wakati watoto wetu wanaendelea kudumaa kwa utapiamlo? Ficha ujinga wako mkuu.
Hahaha; Halafu kila siku tunalalamika "Tunataka Elimu ya bure kama tulivyoahidiwa..." Lakini watoto wanashinda njaa shuleni. Hatukubali kuchangia hicho chakula cha watoto cha mchana. Sasa Akitokea mfadhili tunasema ana agenda ya siri. Hivi watu hatujiulizi sisi ni NANI na tuna UMUHIMU gani hivyo hata watu (Mataifa yaliyoendelea) watuonee gere hadi watumie nguvu kubwa na ujanja kivile wa kutudanganyishia mchele? Jamani tupunguze unoko - hauna tija kabisa.
 
Back
Top Bottom