Wasikilizaji wa Radio Imani: Ole wake atakayewalisha watoto wetu mchele wa msaada wenye virutubisho

Wasikilizaji wa Radio Imani: Ole wake atakayewalisha watoto wetu mchele wa msaada wenye virutubisho

Sakata la mchele wenye virutubisho kutoka Marekani limeendelea kuchukua sura mpya baada ya waislamu kuukataa bila kumumunya maneno. Wakiongea kupitia redio ya kiislamu ya Imaan FM inayounguruma kutokea mkoa wa Morogoro, wamesema hawautaki mchele huo na wametoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayewalisha watoto wao. Wamesema chakula wanacho cha kutosha hapa nchini na kushauri waletewe vitu wasivyokuwa navyo kama vile ndege, magari na ambulance.

Ili kuonyesha kuwa hawatanii katika hili, hata watangazaji waliokuwa wakiendesha kipindi walionekana kushabikia kitendo hicho. Mtu yeyote aliyepiga simu kwenye kipindi akionyesha kwenda kinyume na msimamo wao, walimkatia simu mara moja. Hebu wasikilize wewe mwenyewe kupitia klipu hiyo hapo chini.

MAONI YANGU
Huu mchele sasa naona umeanza kutugawa kiitikadi. Wakristo nao wakitoka hadharani na kuweka msimamo wao, hapatatosha. Ifike mahali ubaguzi wa kijinga kama huu ukemewe kwani unaweza kuligawa taifa na kuhatarisha umoja na mshikamano tulio nao hapa nchini. Tusiruhusu kikundi kidogo cha watu kitugawe kwa sababu yoyote ile.

Nawasilisha.
Wazee wa bit, watalishwa na hamna kitu watafanya.
 
Huko Gaza watu wanakula hiyo misaada na ndio wanaijua dini vizuri kuliko hao Walalamishi !
Ukienda Pakistan na Afghanistan utakutana na wagonjwa wa polio wengi kiasi ambacho hutoamini macho yako !
Hiyo yote ni kwa sababu eti chanjo zinazotolewa na wazungu zinazuwia watu kuzaa !!
Cha ajabu ni kwamba Dawa karibu zote zilizopo Hospitalini na kwingineko zimetengenezwa na hao hao wazungu. !

Na hata hizo mashine zote utakazozikuta huko Hospitalini kuanzia kipimo cha joto la mwili au X-ray , MRI, Citiscan na kila kitu mpaka visu vya kupasulia wagonjwa vimetokea kwa hao hao Wazungu !
Wazungu wakitaka kutudhuru watatudhuru hata kwa kutumia mionzi ya simu tunazozitumia 😅😅 !

Wazungu wapo na vitu vyao vipo kila mahali ulipo na unavitumia kila siku !
 
Hiyo redio ni ya kipuuzi kuwahi kutokea nchini. Hata hao watangazaji wao ni wapuuzi na wakiukaji wa miiko ya utangazaji. Hao waislam ni kina nani duniani/nchini mpaka watoe ole? Ni wapuuzi, wana uhakika gani kama huo mchele ni mbaya? Basi kama ni hivyo watoto wao wasile, watakula wengine na wasilalamike kubaguliwa, shame on them
Vyakula vigawiwe wanaotaka kula watakula na wasiotaka kula na wasile !
Simple mathematics- unataka chukua kama hutaki kwenda zako 😅😅
Wasitubabaishe hao watu !
Sisi tuna njaa tunautaka huo Mchele !
Acha wao ule mchele unaotengenezwa na mashine wapike biriani zao !!
 
R.I.P Magufuli

Sasa tunaletewa vitu vya kijinga badala ya kuletewa vitu vya maendeleo kwa nchi yetu.

Ni wamarekani hawahawa kwa kumtumia mamluki Tundu Lisu wanayemsomeshea watoto wake walipinga ujenzi wa bwawa la umeme alafu wanajifanya wanatupenda sana kutuletea mchele!!
Huo mchele waulete huku mikoani tuuchukue, huku haturembi.
 
Back
Top Bottom