Wasikilizaji wa Radio Imani: Ole wake atakayewalisha watoto wetu mchele wa msaada wenye virutubisho

Wewe mleta mada ni MWONGO. Mimi ni mkristo lakini katika hili NAUNGANA na hao waislam. Tutapewaje chakula ambacho tunacho? Kule Mbeya kuna mcheke mwingi. Nyuma y msaada huu kuna AJENDA YA SIRI. Hizi NGO lazima ziwe controlled.
Huo mchele wa mbeya ni ghali na watu hawana pesa ndio maana wanautaka huo wa bure !
Mimi pia ni muislamu lakini sikubaliani na huo msimamo wa kuukataa mchele wa msaada !
Kama wengine mnashiba mjue wengine wanalala na njaa !
 
 
Mkuu tunaongelea ishu ya wanawake kuzuiwa kwenda shule. Mbona unaingiza hoja ya usomi tena? Jibu swali kama lilivyoulizwa usijibu nje ya key.
 
Mbona wao walitetea mkataba hovyo wa bandari? Nasemaje, nasemaje, walete mchelee huo tulee
 
Kwanini hatuletewi msaada wa ndege za abiria tunaletewa wali tu? Tena uliorutubishwa?
Msaada ni kitu ambacho hakitolewi masharti na mpokeaji mkuu. Kama uwezo wangu ni wa kukupa wali huwezi kunilzamisha nikununulie ndege. Hakuna kitu kama hicho.
 
Bado maamuma mpo kumbe? Yani kuzaliwa mshamba kazi kweli. Msaliti yupo analiwa na funza huko. Bwawa la umeme gani wakati mgao bado upon? Alafu umeme wa maji sio WA muda mrefu!! Elewa.
 
Hawa jamaa si wanafiki...nawakubali kwa misimamo.
Ref. Zenjibar
 
Porojo za uswahilini hizi.
 
Hivi kwani marekani hakuna waislam? Naomba kueleweshwaa
 
Kuna vitu vingi ninawapingaga radio imani! Kwa hili niko pamoja nao 100% Hao mashetani ya mangaribi yana mbinu nyingi sana za kutumaliza! Pale tutakapoweza tupinge kwa nguvu zote! Hivyo viNGO vinavyojipendekeza kwa hao viangaliwe kwa jicho la tatu.
Ninaandika haya kwa uzoefu mkubwa! miaka mitatu iliyopita NGO ya huko marekani ilikuja na mpango wa kuleta tani nyingi za mahindi kutoka marekani.
1. Ushauri wa kwanza nilioutoa ni kuleta fedha hapa TZ ili chakula kinunuliwe kutoka mikoa yenye ziada (the big four) kuleta kwenye mikoa yenye changamoto WALIKATAA
2. Ushauri wangu wa pili ni kuwa wasaidie kujenge uwezo wa uzalishaji wa ndani utakaotosheleza nalo WAKAKATAA WAKISEMA SIO KIPAUMBELE CHAO
Hawa watu wana agenda mbaya for sure hata kama tuko vulnerable katika maeneo mengine mengi lakini pale tutakapoweza tuwakatalie!
Lengo lao kwa umoja wao!
1. Hawataki uchumi endelevu utakaleteleza kujitawala. Mifano ni mingi mno!
2.. Watahujumu hata uhai kwa muda mrefu ili kujihakikishia maisha kwenye hii sayari yetu dhidi yetu!

Big up Radio imani!
Yeyote alienda kupitisha huu upuuzi awajibishwe haraka! Hata huyo Bashe alikuwa wapi mpaka huu uchafu ukaingia nchini ATUPISHE
 

Wanafiki wakubwa hao. Kama wana uwezo wawaambie Marekani wasiwape chakula wapalestina. Halafu wawapelekee chakula huko Gaza.

Most of the Gaza GDP of $700 million comes as foreign humanitarian and direct economic support. Of those funds, the major part is supported by the U.S. and the European Union. Portions of the direct economic support have been provided by the Arab League, though it largely has not provided funds according to schedule.

Waarabu wamejaa unafiki mtupu, lakini ni watu wasio na upendo wa kweli.
 

Ujinga ni mzigo mzito.

Hivi ni lini US walipinga ujenzi wa bwawa la umeme?

Ujenzi wa bwawa la umeme ulipingwa kwa msingi wa kuharibu ekolojia ya mbuga ya wanyama ya Selou, na waliokuwa wamepinga walikuwa ni wataalam wa mazingira wa ndani ya nchi, na Jumuiya ya Ulaya, ambao ndio wanafadhili hifadhi mbuga zetu za wanyama!!

Ni mapema sana kusema kuwa ujenzi wa bwawa hilo la umeme ulikuwa ndiyo uamuzi bora zaidi kuliko ujenzi wa vyanzo vingine vyote vya umeme. Mlango mmoja tu umefunguliwa. Tusubiri litakapokuwa kwenye full operation, ndiyo tutajua kama maamuzi yetu yalikuwa sahihi au hao wataalam na nchi wafadhili wa hifadhi za Taifa walikuwa sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…