Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Tumerizika??? Shida imeanzia hapo. Nenda shule dogo
 
Manara sio malaika afurahishe watu wote
Wewe kama hilo jambo hujalipenda jua Kuna mwingine kalifurahia, jifunze kustahiliana
Mimi binafsi sipendi mziki wa mapiano ila siwezi kuchukua dj akipiga mapiano watu wakaruka
Issue siyo mapungufu ya kibinadamu.

Manara aliboa kila mwenye akili timamu.

Mnalalamika mashabiki wa Yanga hawaendi uwanjani, lakini kwa yaliyo tokea jana ni ushahidi wa wazi kwanini mtu kwenda uwanjani lazima ajiuoize mara 100.

Imagine, mtu katoka nyumbani kaacha wazazi, ameenda na watoto, au ameenda na pesa ya chakula cha mchana pekee??

Au mtu katoka Morogoro, Bunju, Boko, Tegeta, Madale, Kimara, Kibaha, anarudi vipi kwa usafiri tulio nao??
 
Usitegemee makubwa toka kwa Yanga, ile ni timu ya Kiswahili na ndiyo maana mambo yao ni ya Kiswahili swahili tu siku zote.
 
Wewe ni Yanga? Inakuhusu? Acha wivu.
 
Hata mimi kiukweli sijafurahishwa na mambo kadhaa kwenye tamasha la jana;

1. Kupangwa siku ya Jumapili, badala ya Jumamosi! Na hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mashabiki wanatokea Mikoani, na usikute ni wafanyakazi! Sasa unarudi vipi Mkoani na kuwahi kazini?

2. Mchezo wa kuhitimisha tamasha kuanza saa tatu usiku! Wakati mwingine nashauri mchezo uanze kati ya saa 11 - 1 jioni, ili watu waondoke mapema kurudi majumbani kwao. Sidhani kama kulikuwa na sababu ya msingi ya kuanza saa tatu usiku.

3. Hajji Manara adhibitiwe. Huyu kiumbe akiendelee kuachwa afanye anavyotaka; bila shaka kuna siku watu watasusa kuhudhuria hilo tamasha. Haiwezekani mtu mmoja ajione ana haki ya kufanya chochote anachojisikia hata kama ni kitu cha kipuuzi! kwenye kundi la watu elfu 60+.
 
Gsm wanamuogopa manara wanajua wakimchinjia baharini ataitisha press na kuanza kuwaanika km alivyomfanyia mo dewji.

Inakuwa kama ile hadithi ' nani wa kumfunga paka kengele? Wanakosa ujasiri wa kumwambia hahitajiki yanga
Na tokea arudi hana alichoongeza zaidi ya drama tu!
Show ikiendeshwa na Manara kunakuwa na maujinga kama haya.
GSM Kama anampenda Sana Manara ampatie kazi nyingine ndani ya kampuni zake tofauti na Yanga.
 
upande wa protocol alikuwa hovyo

hivi Mangungu alitambulishwa ?
 
Manara hajawahi kufanya kazi GSM, sidhani kama anawajua.

GSM wamewahi kuanikwa humu na mtu waliyemtimua na mpaka leo wapo wanadunda, na alikuwa mtu muhimu aliyekuwa Manager wa GSM Mall wakati inaanza
 
Mkuu familia yako inafahamu unapigania haya yasiyo na tija...
😂😂
 
Ndugu mshabiki,ulienda uwanjani kwa raha zako,umefurahi kwa raha zako,ilipofikia hatua ukakereka ungeondoka kwa raha zako na ungebakia na raha zako.
 
Manara hajawahi kufanya kazi GSM, sidhani kama anawajua.

GSM wamewahi kuanikwa humu na mtu waliyemtimua na mpaka leo wapo wanadunda, na alikuwa mtu muhimu aliyekuwa Manager wa GSM Mall wakati inaanza
Manara yupo yanga sababu ya gsm na ni balozi wa bidhaa zao halafu huwezi kumfananisha huyo meneja na mtu maarufu kama haji manara
Haji manara akisema jambo linakuwa na uzito mkubwa kuliko angesema mtu mwingine wa kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…