Hili zoezi linashughulikiwa na ofisi ya Utumishi kwenye ofisi yako (HR office kama wanalivyozoea kujiita). Kuna ofisi ambazo zina matawi sehemu mbalimbali na kule walipo hakuna mtu wa kuwahakiki hivyo wanakwenda ofisi za Halmashauri za miji, manispaa au jiji walipo au wanakwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Unatakiwa kwenda kwenye uhakiki na vitu vitatu: salary slip, kitambulisho cha kazini na kitambulisho cha taifa alimaarufu NIDA. kama uko likizo jitahidi uwasiliane na ofisi yako idara ya utumishi wakupe utaratibu. usidharau hii serikali ya awamu hii kukutoa kwenye system ni dakika!