Tetesi: Wasio na Vitambulisho vya Utaifa Kutopata Mshahara?

Tetesi: Wasio na Vitambulisho vya Utaifa Kutopata Mshahara?

Wakuu habari za kazi.
Kuna tetesi kua watumishi wa umma wasio peleka Vitambulisho vya Utaifa kwa Human Resources au ofisi husika kama ilivyoagizwa kwaajili ya uhakiki, hawatapata mshahara wa kuanzia mwezi huu July.

Hiyo nimeambiwa Leo na HR wa ofisi yangu. Mimi nikiwa mmoja wa watu wasiopeleka (kwasababu Sijapata bado), na deadline ya kupeleka IDs hizo ni Tarehe 16 July mwaka huu.

Nilikua nauliza kama kuna ukweli wowote katika tetesi/taarifa hizi.

Shukrani.
Wewe ndo ulikuwa unajite ngenezea kitambulisho au nida? Unakosaje mshahara kwa kitu ambacho hujapewa na anayestahili kukupa? Fikiria ndg kwa kina

Sent from my Vodafone 875 using JamiiForums mobile app
 
Hata mie hapa kibaruani kwangu tumesisitizwa kuhakikisha tunafanyiwa uhakiki huo wa kuonesha kitambulisho cha kazi, salary slip na kitambulisho cha taifa, wanasema ukizembea kuna hatari ya kukosa "mtonyo" wa mwezi wa saba.
Hizi ni propaganda ili musiongezwe salary, kaeni vizuri na ccm! Kama mtu hujapata kitambulisho na ulijiandikisha logic yao ni ipi kwa mfano kama si propaganda.

brain is the beautiful part of the body.
 
Watumishi wanaotishiwa ni waalimu tu,sijui kwa nini walimu wangu hawataki kabisa kujiongeza hata kwenye ishu ndogo kama hii yaani wakiambiwa kitu na hao maafisa utumishi wanaamini utadhani ni tamko la wizara najaribu kufikiria tu NIDA na mshahara wako wapi na wapi wanasahau uhakiki wa NIDA unaisha tarehe 15.july ambapo payrolls zimeenda zamani ingekua kuna uhasiano wangemaliza kabla ya tarehe 10 alafu kuna kundi kubwa la watumishi hawajapata hizo ID kuna kipindi nawaonea huruma sana walimu wangu wanavyoburuzwa kama watoto alafu watu wa HR wanavyowajulia walimu watawatishia vitu viwili tu kukasimamishiwa mshahara au kupelekwa kijiji heeee heeee hapo mwalimu atapigana vikumbo kwenye foleni [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Masharti ya kazi ya kuajiriwa hayakua lazima uwe na I'd ya taifa.wacehe ujanja ujanja.itakula kwao watapelekwa mahakaman

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Tafuta ofs za nida zilipo au ulipojiandikishia then wakupe number ya kitambulisho chako then nenda na hizo number za kitambulisho taarifa zako zitasoma vizuri. Sio lazima uwe na kitambulisho chenyew.
Zingatia ni muhimu.ahsante

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habari za kazi.
Kuna tetesi kua watumishi wa umma wasio peleka Vitambulisho vya Utaifa kwa Human Resources au ofisi husika kama ilivyoagizwa kwaajili ya uhakiki, hawatapata mshahara wa kuanzia mwezi huu July.

Hiyo nimeambiwa Leo na HR wa ofisi yangu. Mimi nikiwa mmoja wa watu wasiopeleka (kwasababu Sijapata bado), na deadline ya kupeleka IDs hizo ni Tarehe 16 July mwaka huu.

Nilikua nauliza kama kuna ukweli wowote katika tetesi/taarifa hizi.

Shukrani.
Nenda nida kapeleke karatasi zako watakupa namba ambayo utaipeleke kwa hr wako wengi wefanya hivyo...huku ulisubiria id...

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Kama upo wilayani au manispaa kuna ofisi kabisa ya nida kwa hiyo ni suala la kwenda tu hapo kwenye ofisi
 
Wakuu habari za kazi.
Kuna tetesi kua watumishi wa umma wasio peleka Vitambulisho vya Utaifa kwa Human Resources au ofisi husika kama ilivyoagizwa kwaajili ya uhakiki, hawatapata mshahara wa kuanzia mwezi huu July.

Hiyo nimeambiwa Leo na HR wa ofisi yangu. Mimi nikiwa mmoja wa watu wasiopeleka (kwasababu Sijapata bado), na deadline ya kupeleka IDs hizo ni Tarehe 16 July mwaka huu.

Nilikua nauliza kama kuna ukweli wowote katika tetesi/taarifa hizi.

Shukrani.
Mkuu mshahara wa mwezi huu naamini utatoka, zoezi lenyewe limekuwa na matatizo lukuki na sasa wamesema ambao hawakupiga picha wakati wa zoezi husika basi wakapigie mitaani kwao kama zoezi hilo lipo. Kwa tuliokuwa nje wakati wa zoezi hilo tumepata shida na usumbufu mkubwa. Nimeongea na jamaa yangu na kusema salary ya mwezi huu ipo, na bahadhi ya maofisi wameongeza uhakiki hadi August. Ni zoezi lililohitaji muda au liwe endelevu kwa ambao hawakuwepo waendelee kupat huduma.
 
Hizo taarifa si za kweli.
Huu sio uhakiki huu ni mpango wa kuunganisha taarifa za watumishi ambazo zimetawanyika sehemu mbalimbali(nida, utumishi na hazina) ili zifanane kuepuka mrundikano wa taarifa nyingi zinazojirudiarudia.

Na ni zoezi endelevu hivyo halihusiani na usitishwaji wa mishahara.

Mshahara utasitishwa kama itabainika taarifa zako zilizoko utumishi ni tofauti na za nida na hazifanani na za hazina na pia umeshindwa kuthibitisha taarifa sahihi ni zipi.
Hapo tayari unakuwa ni mtumishi hewa.
Wewe ndo umenena kitu chenye mantiki kabisa, MaHR wanapiga mkwara ili zoezi likamilike kwa wakati. kuna watumishi kibao wako nje kimasomo na hawana vitambulisho na hawawezi kuwakatia mishahara. Otherwise itakuwa ni akili ndogo kufanya hivyo ndani ya muda mfupi hivyo huku hata waliopiga picha wengine hata taarifa zao hazionekani. Baada ya zoezi hili hata mtumishi akitaka kuhama au kuhamishwa inakuwa rahisi sana kwani taarifa zote zitakuwa pamoja, pia ukifika muda wa kustaafu system yenyewe inasoma, unatemewa mzigo wako unasepa.
 
NIDA hawaku-update data za baadhi ya waliojiandikisha,. Na baadhi ya vitambulisho havijatoka hadi muda huu... kosa la nani?. Uzuie mshahara wa mtu kwa sababu zisizo zake!?
 
Usichee kibarua wakati unaona hali ilivyobana kupata kibarua kingine. Nenda wilayani kwako kuna ofisi za NIDA ukafanye taratibu zakupata kitambulisho. Watakupa namba ambayo utaenda nayo kwenye zoezi la uhakiki linaloendelea. Ingawa halimashauri zinatofautiana lkn wana utaratibu unaoweza kukusaidia kuhakikiwa.

Chezea mshahara, usichezee kibarua usawa mgumu.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Ofisi za NIDA wanasema wamepokea waraka kuwa watumishi wote ambao hawakuoma vitambulisho ndani ya muda uliotolewa waende kwenye mitaa yao husika wafanye hivyo kama zoezi hilo limeshaanza. Binafsi nimeenda leo na wamekataa kabisa na wana majibu ya dharau sana, customer service ni zero.
 
Haiwezikuwa ni July kwani mshahara wa mwezi wa serikali huprintiwa 5th date of the month husika...
 
"Workers of the world you must unite there's nothing to lose but your own chain" Karl Marx..
 
Back
Top Bottom