Wasioamini Mungu inawahusu

Wasioamini Mungu inawahusu

Kama kitu kipo huitaji imani ya kujua uwepo wake.

Mfano, Hauhitaji imani kujua kwamba mwanzilishi wa JF ni Maxence melo.

Kwa sababu tayari una uthibitisho na uhakika kwamba JF ilianzishwa na Maxence melo. Na hilo linathibitika pasi shaka.

Sasa tutahakikisha vipi na kuthibitisha vipi, imani yako ya uwepo wa huyo Mungu ni imani ya kweli, Na si Mauza uza tu?
Najua haihitaji imani kujua maxence melo lakini inahitaji imani kumjua Mungu au hatujaelewana? Kama wewe huitaki imani wengine wanaitumia na wanamuona Mungu.
 
Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba Hayupo.
Sasa ndugu tumeongea vyakutosha naomba kwa uelewa wako na kwa faida ya wengine hebu tueleze tujue kwamba tumetokea wapi? Au tumeumbwa na Nani?
 
Najua haihitaji imani kujua maxence melo lakini inahitaji imani kumjua Mungu au hatujaelewana? Kama wewe huitaki imani wengine wanaitumia na wanamuona Mungu.
Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea huyo Mungu kwa vile hajawahi kuwepo na hayupo kujidhihirisha mwenyewe, kwamba yupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe hadharani ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
 
Sasa ndugu tumeongea vyakutosha naomba kwa uelewa wako na kwa faida ya wengine hebu tueleze tujue kwamba tumetokea wapi? Au tumeumbwa na Nani?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimeumbwa, Hata huyo muumbaji wa kila kitu lazima awe ameumbwa.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimetoka sehemu fulani, Hata hiyo sehemu fulani lazima iwe imetokea sehemu nyingine fulani.

Hivyo hivyo to infinity...

Yani kutakuwa na waumbaji endless.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza tu chenyewe pasipo kuumbwa, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo pasipo kuumbwa.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina muumbaji, Hata Ulimwengu Hauna na Hauhitaji Muumbaji.
 
Imeandikwa wapi iyo mkuu
Kitabu cha Mwanzo kuanzia aya ya 8

Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
 
Ikiwa huamini Mungu alieumba ulimwengu mzima na vilivyomo, kwamba kila kitu kipo nature, mbona magari na vitu vyengine tunaona Made in China, made in Tanzania etc

Wenye akili tu wataelewa
Mungu alieiumba Tanzania akamwachia shetani jukumu la kuchagua viongozi wa kuwaongoza watu wake (watanzania)
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimeumbwa, Hata huyo muumbaji wa kila kitu lazima awe ameumbwa.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimetoka sehemu fulani, Hata hiyo sehemu fulani lazima iwe imetokea sehemu nyingine fulani.

Hivyo hivyo to infinity...

Yani kutakuwa na waumbaji endless.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza tu chenyewe pasipo kuumbwa, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo pasipo kuumbwa.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina muumbaji, Hata Ulimwengu Hauna na Hauhitaji Muumbaji.
Ok sawa japo hujanijibu nitakuuliza swali dogo kwanza then tuendelee.

Je hivi umbali unamwisho?
 
Mungu huyu huyu ambaye anaruhusu haya manyamwera watekaji,na watoa roho za watu waendelee kuvuta hewa safi ya dunia!
 
Ok sawa japo hujanijibu nitakuuliza swali dogo kwanza then tuendelee.

Je hivi umbali unamwisho?
Ulisoma Geography vizuri kwamba ukisafiri kuizunguka dunia, Utarudi palepale starting point yako.

Shuleni tena kidato cha kwanza kabisa, Hukusoma mambo ya Circumnavigation of the Earth?
 
Ulisoma Geography vizuri kwamba ukisafiri kuizunguka dunia, Utarudi palepale starting point yako.

Shuleni tena kidato cha kwanza kabisa, Hukusoma mambo ya Circumnavigation of the Earth?
Usiwe unakurupuka kujibu tafakari swali kwa umakini then ujibu. Umefikiri kwenye dunia hujafikiri nje ya dunia hii au na huko Ni kwa kufikirika pia?
 
Mungu huyu huyu ambaye anaruhusu haya manyamwera watekaji,na watoa roho za watu waendelee kuvuta hewa safi ya dunia!
Pamoja na maelfu ya watoto na wanawake wanaoteseka na kufa kila siku kwa njaa, vita, magonjwa, majanga ya asili n.k
JamiiForums1832832046.jpeg

Huyo Mungu hajawahi kusaidia chochote licha ya watu kusali na kumuomba sana awasaidie na kuwalinda. Lakini Holaaaa!!!

Nothing happens.
 
Kukataa uwepo wa Mungu ni ugonjwa wa akili na kiburi kilichoshindikana. Akili kushindwa kujua Mungu ni nani, ni nini, alitoka wapi, anafanana je, aliumbaje ulimwengu - haimaanishi kuwa hayupo - ujinga sio sababu ya kukataa ukweli. Binadamu tutahangaika sana, tutajitutumua sana, tutaamini sana hizo bongo zetu ambazo mwisho wa siku zitaoza..lkn ndani mwetu kila mtu anajua Mungu yupo. Hata kitendo cha kuanza kupata mawazo kinzani kuwa yupo au hayupo ujue tayari yupo...asingekuwepo pasingekuwa na mawazo ya kujustfy kutokuwepo kwake.
Mtu huwezi ukaanza kudebate whether nguo ni nyeupe wakati unaona kabisa na nyeupe...watu mtaanza kubishana nguo ni nyeupe sababu wote hamjui rangi nyeupe ni ipi au hiyo rangi mnayoibishia hamuielewi na hakuna mtu abayeijua..room ya ubishi inaanza pamoja na kuweka misimamo ya kujitia matumaini.
 
Angani kwenye magalaxy
Hakuna umbali usio na mwisho, Kuna umbali kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Dunia ni sehemu ya Universe.

Universe is everything, It includes Time, all of the space, all of the matter and energy that space contains. It even includes me and you.

Vyombo mbalimbali vya wana anga zikiwemo Satellites, spaceships Vinatumwa kila mara kwenda huko kwenye Anga za juu, kuchunguza na vinasafiri umbali mrefu sana na vinafika na vingine hurudi.

Kwa hivyo kwenye universe hii hii, umbali upo kutoka point moja kwenda nyingine.

Hakuna umbali usio na mwisho.

Umbali upo kutoka point moja kwenda nyingine kwenye universe hii hii iliyopo.
 
Jibu swali tuendelee mbele na mada mbona Mimi nilikuwa nakujibu? Yaani kaswali kadogo tu hoi utaweza yanayokuja?
Hakuna umbali usio na mwisho, Umbali upo kutoka point moja kwenda nyingine kwenye universe.
 
Pamoja na maelfu ya watoto na wanawake wanaoteseka na kufa kila siku kwa njaa, vita, magonjwa, majanga ya asili n.kView attachment 3092122

Huyo Mungu hajawahi kusaidia chochote licha ya watu kusali na kumuomba sana awasaidie na kuwalinda. Lakini Holaaaa!!!

Nothing happens.
Unajaribu kumuweka Mungu katika hisia za kibinadamu naona.Kwani wewe nani alikuambia kifo ni adhabu??Mtu akifa tunaumia sababu amekufa au tunaumia sababu hatutamuona tena?? Kifo ni nini hata kiingiliane na uwepo wa Mungu. Kama ukijua mtu akifa nini kinafuata then unahaki ya kumlaumu Mungu..lkn nina uhakika 1000% hujui kuna nini baada ya kufa , lkn unalaumu watu wanakufa.
Kifo tu kinaonesha how limited human beings are : unampenda mtu l, hutaki aondoke but huna cha kufanya au kuzuia..uwe na pesa usiwe na pesa, tajiri, Rais...HUNA cha kufanya - we are defenseless kabisa.Sasa kama tunashindwa kutatua hilo tatizo dogo tu ndo unafikiri akili hizohizo ndo zitamuelewa Mungu kweli???
 
Back
Top Bottom