Pre GE2025 Wasira: CHADEMA wakitaka kufanya fujo wanachukua vijana kutoka Tarime

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Namsikiliza huyu Mzee kazi yake Kuisema CHADEMA tu, kwahiyo watu wanakusanywa kusikiliza mambo ya CHADEMA badala ya Sera? Mzee huyu naye
 
Mzee kazeeka naonakajipa Kazi ya katibu mwenezi wa chadema
 
maskini vijana wa Mara,
wengi wao wana ulemavu wa kudumu baada kutumiwa kuleta fujo..

Inasikitisha sana na inafedhehesha sana aise 🐒
 
Ccm imepatwa na jua , alafu uyu mzee Wasira nywele zilikua nyeupe ,sikuizi naona zimekua nyeusi , so anaweka nywele dawa ili aonekane ni kijana wa miaka 18?

Hivi hawaoni wazee wenzake kama Mzee warioba na nywele nyeupe wanavyopendeza
 
Wana CHADEMA wenzangu, tuache kurikruti mercenaries kutoka TARIME.

Nao CCM waache kurikruti mercenaries kutoka chugga

Walahi huyu mzee kwa makavu bana hatare.

Tujipange tukawachuke vijana wa mbeya.
 
Hivi huwa hawqna sera za hao vijana ? Bida sio ajira waje na sera kuwatoa boda boda...vijana wanawake....viwanda kati na vikubwa .....sio CDM kila anapoenda...
 
Mpaka hapa uzi ulipofikia sijasikia hata mtu mmoja akisema, '

"Aliyoyasema sio kweli"

Hio inadhihirisha nn?
Kwamba anasema ukweli?

Badala ya CC wana CHADEMA kumtupia madongo huyu mbabu, tujiangalie cc kwanza. Maneno yake ni mazito na sio ya kupuuzwa tu.

Tujitathmini.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba maagizo hayo ya kuchukua vijana Tarime lazima yalipata baraka kutoka Juu? Ni nani alikuwa akihalalisha na kuwezesha hayo? Ndipo hela zetu za Join the chain zilipokwenda huko?

Yametufikisha wapi?

.. tutafute mbinu zingine za kuwafikia wananchi na hususan vijana.

Kuandamana peke yake haitoshi.

Yani hata baada ya maandamano na kushika vichwa vya habari vya ndani na kimataifa, bado tulishindwa kuitikisa CCM kwenye chaguzi zilizopita.

Kwa nn.
jitafakari kabla ya kuropoka hapa na kusema
" Watanzania ni wajinga 'hawajitambui' 'wanatawaliwa' na maneno mengine mengi ambayo ni dhihaka na dharau tu kuchochea hasira na taharuki hayatatupeleka kokote kule. at 0.003? Never Never Again

Hivo basi, tujitathmini, tutafute mbinu zingine, tuwe wabunifu tuwafikie vijana na Wananchi wote. Tukome kuwatia vijana ulemavu.

Nachelea kusema naafiki na mbabu Mh. Wasira.

Peoples✌️
 
Pointi

Inatubidi cc CHADEMA tuyaseme haya. Na Iwe sehemu za Sera zetu badala ya sera za kurushiana vijembe.

Kabisa, wananchi wanapaswa kuelewa madhira wanayopitia chanzo chake ni siasa mbovu na ujinga wa CCM.
Huyu anaongea utafikiri nchi imeanza kuongozwa na CCM jana.
Miaka yote CCMA imeshindwa kuwajali wachimbaji ije iwajali leo?
Huyu Mzee haoni chini ya CCM nchi imeingiliiwa na wachimbaji wadogo wadogo wa kichina na kihindi kila mahala.

CCM imewaona watanzania wajinga nakujikita Kwa wasanii, CCM imewekeza hela nyingi kwa wasanii wakapige domo huku inasahau watanzania walihitaji/wanahitaji vitendo vitakavyobadirisha maisha yao.
 

I agree.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…