Mpaka hapa uzi ulipofikia sijasikia hata mtu mmoja akisema, '
"Aliyoyasema sio kweli"
Hio inadhihirisha nn?
Kwamba anasema ukweli?
Badala ya CC wana CHADEMA kumtupia madongo huyu mbabu, tujiangalie cc kwanza. Maneno yake ni mazito na sio ya kupuuzwa tu.
Tujitathmini.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba maagizo hayo ya kuchukua vijana Tarime lazima yalipata baraka kutoka Juu? Ni nani alikuwa akihalalisha na kuwezesha hayo? Ndipo hela zetu za Join the chain zilipokwenda huko?
Yametufikisha wapi?
.. tutafute mbinu zingine za kuwafikia wananchi na hususan vijana.
Kuandamana peke yake haitoshi.
Yani hata baada ya maandamano na kushika vichwa vya habari vya ndani na kimataifa, bado tulishindwa kuitikisa CCM kwenye chaguzi zilizopita.
Kwa nn.
jitafakari kabla ya kuropoka hapa na kusema
" Watanzania ni wajinga 'hawajitambui' 'wanatawaliwa' na maneno mengine mengi ambayo ni dhihaka na dharau tu kuchochea hasira na taharuki hayatatupeleka kokote kule. at 0.003? Never Never Again
Hivo basi, tujitathmini, tutafute mbinu zingine, tuwe wabunifu tuwafikie vijana na Wananchi wote. Tukome kuwatia vijana ulemavu.
Nachelea kusema naafiki na mbabu Mh. Wasira.
Peoples✌️