Pre GE2025 Wasira: CHADEMA wakitaka kufanya fujo wanachukua vijana kutoka Tarime

Pre GE2025 Wasira: CHADEMA wakitaka kufanya fujo wanachukua vijana kutoka Tarime

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema ni marufuku kwa vyama upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.

Soma: Wasira: Watanzania hawana sababu ya kuichagua CHADEMA

Amesema CCM inamipango mizuri kuhakikisha vijana hao wanatumia nguvu zao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua dhidi ya umasikini.

Wasira aliyasema hayo leo Februari 9, 2025, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.

Tulipowaambia CCM hapa mmepotea mlishupaza shingo. Acha yawakute na huyu mwenye siasa za 2001.
 
Kwa maoni yako huyo Wasira ana ushahidi wa hayo anayoyasema?
Mkulu cjiu, labda uwatafute CCM uwaulize kuhusu ushahidi
Au mnataka kulifanya jeshi la polisi lionekane halijui wajibu wake?
Mnataka? Mm na nani? Kama kuna mtu alifanya hivyo ni Mbowe peke yake. Lissu haezi fanya hayo .
Mimi siamini kama kuna vijana wanachukuliwa tu bila malipo kisa wakaandamane mkoa mwingine
mm naamini, Mbowe mbona alishasema anaifanyia kazi CHADEMA bila ya Malipo bana? Kwamba haiwezekani mkulu?. kama hao vijana walijitolea je? wakalipiwa malazi chakula na usafiri?
Hiyo kazi ya kuchukua vijana kwingine ni ya ccm tu kwa vyama vingine ni ngumu mno!
Wale CCM wanaandamana? moaka hivi karibuni chama kilichoandamana barabarani ni CHADEMA. Itoshe kuna picha humu humu JF zikionyesha CHADEMA wakiwapandisha watu kwenda kwenye hayo maandamano.
 
Back
Top Bottom