Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Mkuu ni wapi hapo Wasomali wanapodai kua sio Waafrika? Suala la wao kutokutaka kuchanganyika ni la kiutamaduni zaidi na wala sio sheria kama ambavyo wewe Mmakonde au Mkwere au Mpogoro uende ndani kabisa wanapoishi Wamasai ukatake kumposa binti yao. Kutakua na ile sociala protest ya jamii inayowazunguuka pale lakini sio sheria kwamba ukioa hapa ndio atatengwa au hautatambulika na watu wakele Jamii iliyoko Africa ambayo inadai wenyewe siyo waafrika ni jamii tofauti na marufuku katika mila yao kuchanganyikana na wengine hata kama ni dini moja wamemjia binti yao juu na kumponda.
Wasomali kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa anzia Somalia Kwenye, ukanda wa Afrika mashariki, ulaya, Australia na Marekani wameonyesha kukasirishwa kwao waziwazi na binti yao huyo kukububujikwa na machozi baada ya kumuona diamond na kumkumbatia.
Ninachokiona kwenye uzi wako ni chuki dhidi ya Wasomali na mila zao, kwani wao ni miongozi mwa jamii chache zilizoendelea kushikilia mila zao kwa muda mrefu licha ya mabadiliko ya kiteknolojia yaliyopelekea mmomonyoko mkubwa wa kimaadili hasa kwa vijana dunia nzima
Wasomali wapo kila mahali na wanachanganyika vizuri tu na watu wengine ikiwemo wanawake wao kuolewa na watu wa tamaduni tofauti.Ndio maana kuna mtu amesema humu kwenye mchango wake kuwa wanawake wa Kisomali wanachukuliwa na Wakinga na wanaume wa makabila mengine. Ni kwamba hiyo ipo siku nyingi na wala sio jana au leo.
Hebu tuonyeshe hao Wasomali wanaopiga kelele dunia nzima kwa huyo msichana wa Kisomali kutaka kuolewa na Diamond. Pengine kama kuna kelele ni labda za kuhisi binti yao aliyelelewa kwenye maadili anapigana mabusu hadharani mbele ya kamera na mwanaume ambaye sio mumewe, na hilo linaweza likawakasirisha jamii yoyote yenye kujitambua. nadhani huyo binti angekua ni dada yako aua binti yako nawe pia usingeona fahari kwa alichokifanya sio kwa sababu ya ubaguzi au imani